Rais Samia chukua tahadhari kusuasua kwa TANROADS, utalaumiwa binafsi

Kuna ombwe kubwa sana la kiutendaji katika serikali hii!
Na inaonesha wazi kauli yake ya "chura kiziwi" ana apply hadi kwenye vitu visivyohitaji siasa..
Kama malengo na mawazo ni urais tu 2025 bila kudeal na kero zetu, lazma watanganyika tushtuke,sio Ccm sio upinzani,nchi inazama na hamna anaejali zaidi ya chawa " wazee wa maokoto" wachache.

Hali ni tete mno kwa wakandarasi, na mikopo wamechkulia mikataba hiyo hiyo ya serikali na dhamana zao,ila sasa hivi wako kimyaa,ni chawa na magazeti tu wanatetea uongo!
 
Mimi sina tatizo na mwanamke kuwa Rais.
Tatizo langu ni kwamba serikali anayoiendesha mama Samia kwa sasa inaua uchumi binafsi(nyumba yangu inauzwa) katika sekta ya ujenzi.
TANROADS mshirika wa wadau wengi katika sekta ya ujenzi imefilisika na inashindwa kutulipa wadau wake.
Kwa hilo asitegemee mimi kama mwana CCM kulichekea.
 
Kutokulipa wakandarasi si kufilisika..na wewe toka umeanza kufanya kazi na TANROADS hujajenga uwezo tu, kwamba hata malipo yakichelewa kampuni inaweza kutumia fedha za akiba kazi ikafanyika bila kwenda kukopa..! hayo makampuni yenu yana umuhimu gani kwenye uchumi km kila mnacholipwa mnakula chote??
 
Usitutingishe mkuu Bado tuna hangover ya Kizimkazi festival.
 
Ninachojua na kiasi Toka vyanzo vya vya TANROADS kwamba haina pesa. Ndio maana inashindwa kulipa.

Kitu kinachosikitisha ni bajeti tunazosomewa, ile bajeti ya 2024/25 wameandika miradi mingi ambayo wanafanya na kutarajia kufanya.
Hivi hawa wataalamu wetu hawawezi kuwa wa kweli kuhusu kuweka kwenye bajeti miradi onayotekelezeka kwa mwaka ule.
Kuna miradi inasogezwa zaidi ya miaka 5 bado haijafanyiwa kazi ingawa kila mwaka wa bajeti inakuwepo, huu si udanganyifu wa kutudanganya. Imefikia hatua wanasaini mikataba kwa ajili ya kutuonesha kwamba mradi huu utaanza karibuni, lakini mwaka mzima kimya.
Hivi serikali ya namna hii inafanya nini.
Kwanini Samia anaruhusu niite upumbavu huu wa namna hii kufanyika.
Unasaini mbele ya vyombo vya habari nchi inajua, halafu mpaka pesa ometumika kwa kusaini mkataba tu.
Mambo ambayo yangefanyika kwenye ofisi yakaisha.
Jamani tunakwenda wapi
Hivi CCM imelewa madaraka na kufanya watakavyo kwa kuwa wanajua hakuna wa kuwaondoa au?
 
Waambie wajinga wenzio kuwa miradi inajengwa kwa MIKATABA yenye malipo. Akili yako ikifikia kama ilipo ya wanasiasa wengine, ndiyo unapata mawazo ya kijinga kama yako.
 
Waambie wajinga wenzio kuwa miradi inajengwa kwa MIKATABA yenye malipo. Akili yako ikifikia kama ilipo ya wanasiasa wengine, ndiyo unapata mawazo ya kijinga kama yako.
Ujinga wa hiki nilichosema uko wapi..kwa hiyo kuchelewesha malipo ni kufilisika..na si kweli wakandarasi wanaopata kazi TANROADS wanapaswa kukua kufikia kutotegemea pesa za mkataba sababu zinaweza chelewa kulipwa kutokana na sababu nyingi..inajulikana sehemu nyingi duniani best standard za ufanyaji kazi na serikali ni mkandarasi kuwa na uwezo wa kuendelea na kazi pale malipo yanachelewa, kwa anayepata kazi kulingana na uwezo na size ya kampuni yake kuchelewa kulipwa hakuwezi kumfanya kulaumu km unavyofanya wakati sababu za kuchelewa zinajulikana..unalalama tu hata chanzo cha yanayokukuta husemi! lkn TANROADS haijafilisika na si mara ya kwanza kuchelewesha malipo kwa wakandarasi..usipoelewa ni sabab unasumbuliwa na ubinafsi!
 
Hayo ndiyo mawazo ya wanasiasa wengi wajinga wajinga na inakera.
Unapoingia mkataba fedha za mradi LAZIMA ziwepo.

Mtu anaongea na wanahanahabari kuwa mradi huu ni wa miaka miwili, mkandarasi afanye kazi usiku na mchana aumalize ama sivyo tutamchukulia hatua, huku nyuma serikali haina hela.
Kwa mkataba wowote wa ujenzi, mwenye mradi(serikali) asipolipa ndani ya siku 28, basi hatua za kuanza kulipa riba ya deni inaanza.
Kumlipa mkandarasi kwa wakati siyo fadhila , ni matakwa ya mkataba.
 
Usiongee tu kwa sababu ya maumiv uliyo nayo..nadhani unafahamu source ya fedha za miradi ya serikali, kodi na tozo za wananchi au mkopo/msaada..utakuwa mjinga km unaweweseka na briefings za kuongea na wanahabari ukaziamini! ukifahamu uhalisia hizo briefings huwezi kupoteza muda acha kuamini hata kuzisikiliza na hasa kwa aina ya viongozi wa ccm..fanya homework yako sawa sawa vile unapaswa kufanya na aina ya viongozi wa ccm, badala ya kuja hapa na lawama kwa taasisi ambayo nayo inapewa fedha kutekeleza miradi..!
 
Nyie ndo vilaza mnaokalia madeski na kutojua kinachoongelewa kwa sasa.
Kwa nini itokee Awamu hii. Kwani imegundulika ghafla kuwa fedha hazikusanywi, na miradi feki imeandaliwa sasa?
 
Nyie ndo vilaza mnaokalia madeski na kutojua kinachoongelewa kwa sasa.
Kwa nini itokee Awamu hii. Kwani imegundulika ghafla kuwa fedha hazikusanywi, na miradi feki imeandaliwa sasa?
Unasumbuliwa na uduni wa kufikiri kwa kina na upana mambo unayosikia na kuona..mipango yote na kiwango cha pesa inachotamka serikali kwenye bajeti ni nadharia..mfano fedha kutoka kwa wahisan n mikopo inaweza isipatikane na hivyo mambo mengi yanabadilika kulingana na vipaumbele vyao..mwaka huu kmekuwepo mgao wa umeme ambao haukutarajiwa, hata uchaguz huu unaofanyika kawaida part ya fedha hutolewa na wahisani, chama chako hawataki hilo kukwepa kusimamiwa na wanaotoa fedha sabb unazijua..sasa hizo fedha kwa mambo hayo mawili tu wanazitoa wapi km si kubana kwenye maeneo km ya TANROADS..bado ni ujinga kulinganisha hali ya jana na leo..ni vitu tofauti kila siku ina mambo yake na yanafanyika kulingana na hali inavyokuja, mahitaji ya jana si ya leo..punguza ubinafsi! nchi si barabara peke yake..!
 
Unachoongea ni ujinga mtupu.
Mtu mwenye akili hawezi ku engage miradi kwa fedha za kufikirika and wish all the best.
Huo ni ujinga wa kiwango cha lami.
 
Unachoongea ni ujinga mtupu.
Mtu mwenye akili hawezi ku engage miradi kwa fedha za kufikirika and wish all the best.
Huo ni ujinga wa kiwango cha lami.
Haya endelea kupiga domo wakusikie..TANROADS imefilisika hivyo wakuprintie pesa wakulipe madeni yako..maana akili uliyo nayo inaishia pale pua imeishia.
 
Wakandarasi WA ndani si ndio hao walichanga fedha bilioni kadhaa kwa ajili ya kununua helikopta ya Samia?
 
Ukipunguza upana wa barabara nchi tatu kila upande toka Mtwara mpaka Bukoba, Mchina atakupa mshiko kiasi gani?
 
Wajinga wanasema MitanoTena!
 
Wajinga wanasema MitanoTena!
 
On a setious note ni bora hizi barabara zilivyokuwa zinajengwa na wakandarasi kutoka nje. At least tulikuwa tunapata value for money.
Wakandarasi wazawa ni political toddies, wanatumia rushwa sana kupata project na kwa sababu cycle ya kuhonga ni kubwa akija site anajenga chini ya kiwango. Tanroads kukosa fedha ni sawa kabisa kwa sababu projects nyingi zinakuwa za kurudiarudia,
 
Mama ameiua nchi yetu.
 
Hatutafika kwa majungu.
Zitaje hizo barabara na mkandarasi husika.
Na kama hiyo ni imani yako basi tatizo unalo wewe katika kuamini kuwa kila nkandarasi ni rushwa tupu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…