Kinyungu
JF-Expert Member
- Apr 6, 2008
- 19,484
- 38,416
Jidu La Mabambasi hela za mfuko wa Road Fund zinaelekezwa wapi? Maana bado zinakusanywa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yule jamaa fiksi, si mkandarasi wala injinia anayefahamika.Wakandarasi WA ndani si ndio hao walichanga fedha bilioni kadhaa kwa ajili ya kununua helikopta ya Samia?
Mkuu hilo ndio swali gumu la kujiuliza.Jidu La Mabambasi hela za mfuko wa Road Fund zinaelekezwa wapi? Maana bado zinakusanywa
Wapumbavu tu nyie, si mliahidi kumuhonga Bi Chura kwa kumnunulia Chopper? Acha muonje joto la jiwe, bado tunawalipa Indiana ya AustraliaView attachment 3138786
View attachment 3139603
MODS naomba msiuunganishe mada hii na nyingine.
Mimi mmoja wa waathirika moja kwa moja wa kusuasua kwa TANROADS, na amana yangu inaelekea kuuzwa na benki kutokana na TANROADS kushindwa kutulipa.
Hali ya kusuasua na kuelekea kufa kwa TANROADS ni hali ambao haijawahi kutokea toka Taasisi hii ianzishwe mwaka 2000.
Kuanzishwa kwa TANROADS kulitokana na sera nzuri za serikali wakati huo kuwawezesha wazawa kushiriki moja kwa moja katika ujenzi wa hasa barabara.
Miaka ya 70, na 80 uujenzi wa barabara ukifikiriwa mara zote watu walikuwa wanawafikiria kina MOWLEM(walijenga Pugu Rd, sasa Nyerere rd), Stirling Astaldi(Italians), Fredericci (Italians),SOGEA (French), COGEFA SPA(Italians).
Makampuni mengi ya ujenzi wa barabara yalikuwa ya ki-Italiani.
Mpaka ukawepo msemo kati ya watu kuwa ulitaka barabara ijengeke mpe mtaliani.
Lakini kwa umakini Serikali iliona jinsi fedha zake zikienda nje kwa kasi ya ajabu maana fedha zote za ujenzi hata barabara ndogo zilikuwa zinaenda nje.
Rais Mkapa(Mungu amrehemu) ndiye aliyekuwa na ujasiri wa kuziweka sera za ujenzi kwa kutumia fedha zetu wenyewe kwa kuanzia namna ya kukusanya fedha na jinsi ya kuzitumia kiamilifu ili kujenga barabara nchini
Mkapa alizanisha utaratibu wa kukusanya fedha kwa kutumia ROAD FUND ambayo ilikusanya fedha kupitia mauzo ya mafuta.
Mkapa vile vile alianzisha TANROADS, taasisi ambayo ingekuwa ya kitaalam kubuni, kusimamia zabuni na kusimamia kitaalam miradi ya ujenzi na kuwasimamia makandarasi.
Yes, makandarasi.
Na hapo ndipo ninaingia.
Makandarasi wazawa walijiandikisha kwa wingi kuingia zabuni za ujenzi wa miundombini na hata matengenezo ya miundombinu iliyoharibika.
Makandarasi wengi wameichukulia TANROADS kama ndiyo sekta rasmi ya serikali kufanya nayo kazi, na kwa miaka zaidi ya 40.
Fedha hizo wanazopata makandarasi wazawa, ni lazima zingeenda kwa waItaliani.
Lakini sasa wazawa wamejijenga na familia zao na kuwekeza nchini mambo mengi ambayo yameongeza mzunguko wa fedha za ujenzi nchini.
Tukumbuke kuwa sekta ya ujenzi inachangia GDP over 13.5%(2015) ya uchumi wa nchi.
Hivyo basi hii Awamu ya 6 kwa sasa imefanya vibaya katika sekta hii ya ujenzi kuwashirikisha wazawa.
Kwa sasa hivi makandarasi wengi nyumba zao ziko sokoni, wengine zimeuzwa tayari. Kufanya kazi na serikali kumekuwa kuchungu mno.
Hali hii hatujaiona zaidi ya liaka 30.
Hatumung'unyi maneno na hili si suala la kichama wa kisiasa pamoja na kwamba wengine sisi ni makada wa chama.
Toka rais Mkapa aanzishe TANROADS, akaj Kikwete,Magufuli mambo yalikuwa shwari, Serikali ilitekeleza majukumu yake kisawasawa kupitia Taasisis hii.
Kufa kwa TANROADS Mama Samia na Awamu ya 6, hamtakosa lawama.
Majungu vipi mkuu, barabara ipi ya lami iliyojengwa na mkandarasi mzawa na ikadumu kama zilivyodumu za hao wakandarasi wa nje?, iyovi hadi mafinga kipande kinaenda mwaka wa 15 na bado kipo imara, nenda barabara ya lindi mtwara uone viojaHatutafika kwa majungu.
Zitaje hizo barabara na mkandarasi husika.
Na kama hiyo ni imani yako basi tatizo unalo wewe katika kuamini kuwa kila nkandarasi ni rushwa tupu.
Mpumbavu mama yako na yule aliyeambatana naye kutoa zawadi ya choppee.Wapumbavu tu nyie, si mliahidi kumuhonga Bi Chura kwa kumnunulia Chopper? Acha muonje joto la jiwe, bado tunawalipa Indiana ya Australia
Jamaa lile igizo na wewe uliingia mkenge kuamini? Kaulizie jina la hao wakandarasi kama utalipata hata 1Wapumbavu tu nyie, si mliahidi kumuhonga Bi Chura kwa kumnunulia Chopper? Acha muonje joto la jiwe, bado tunawalipa Indiana ya Australia
Duniani kuna mambo!Usikute ye mwenyewe kajichotea, kujianda na shughuli ya ndoa ya mwakani, ananunua zawadi za washenga kuwahonga wakamtongozee, baiskeli laki 3, pikipiki za kutosha, kila kata 3 tatu.