Rais Samia: Demokrasia ni kuheshimu Sheria, heshima ya Mtu inakuja kwa kuheshimu Sheria za Nchi, ombi la Zitto kuhusu kesi ya Mbowe lajibiwa

Rais Samia: Demokrasia ni kuheshimu Sheria, heshima ya Mtu inakuja kwa kuheshimu Sheria za Nchi, ombi la Zitto kuhusu kesi ya Mbowe lajibiwa

idawa

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2012
Posts
25,284
Reaction score
38,364
Akijibu ombi la Mheshimiwa Zitto leo kuhusu ombi la kumwachilia Mbowe ili kuweka nchi kwenye mshikamano wa Kitaifa, Mh. Samia amesema kwanza afuate sheria pili awe na heshima.

Tofauti na tuhuma alizosema huko nyuma wakati akihojiwa na BBC kuwa Mbowe ana tuhuma za ugaidi.

KWA UFUPI:

Zitto anasema hajamuombea Mbowe Msamaha, Rais Samia anadai Zitto kaomba msamaha.

Lissu anasema Mbowe hawezi samehewa sababu hana hatia na hajahukumiwa; wadau wa CHADEMA wanalalamika kwanini Zitto aombe msamaha? Msamaha wa kosa lipi?

========

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewakumbusha viongozi wa vyama vya siasa kuzingatia na kutii sheria ili kuepuka heshima zao kuondoka.

Rais Samia ameeleza hilo leo wakati akijibu ombi la Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo Ndugu Zitto Kabwe ambaye alimuomba awasaidie kumsamehe Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe.

''Nataka nizungumzie kidogo aliloniomba mwanangu Zitto, kwamba yule mwenzetu msamehe basi aje awe na sisi. Demokrasia ni kuheshimu sheria, heshima ya mtu inakuja kwa kuheshimu sheria za nchi.,'' ameeleza Rais Samia Suluhu.

Ameendelea,’’Isingekuwa uvunjifu wa sheria leo isingemlazimu Zitto kuomba hapa kwamba yule mwenzetu muachie lakini unapovunja sheria unajivunjia heshima

“Naomba tufanye kazi kwa kuheshimu sheria, waswahili wanasema mtaka nyingi nasaba hupata mingi misiba, ingawa kusameheana nako kupo,” amesema Samia.

Aidha Rais Samia amesisitiza kuwa kuna taifa moja tu ambalo raia wote wanawajibika kulilinda.

====

Zaidi soma;

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Zitto Kabwe amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kusaidia kuachiwa kwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.

Zitto ambaye pia ni kiongozi wa Chama Cha ACT-Wazalendo ametoa ombi hilo leo wakati wa mkutano wa wadau wa kujadili hali ya demokrasia ya vyama vingi nchini.

Mbowe na wenzake watatu wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 16/2021 yenye mashtaka sita yakiwemo ya kula njama na kufadhili vitendo vya kigaidi, inayoendelea katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.

Akizungumza kwa sauti ya upole Zitto amesema, “Sisi viongozi wa vyama tupo hapa na wengine hawapo kwa sababu zao lakini kuna mwenzetu hayupo hapa kwa sababu ya changamoto za kisheria.

Tuna utamaduni wa kumaliza haya mambo na haitakuwa mara ya kwanza, tunakuomba sana kwa mujibu wa sheria na kufuata taratibu tusaidie mwenzetu tuwe naye ili tuweze kufanya kazi kwa pamoja na kuunganisha nchi yetu, tufanye siasa za tija na maslahi kwa nchi yetu,”. Amesema Zitto nakuongeza

“Ni dhahiri kuna changamoto za hapa na pale na wewe ndio Rais wetu, tunakuomba sana kama ambavyo uliahidi katika hotuba yako ya kwanza wakati unazindua Bunge.

“Utuunganishe, tumepalanganyika, uliweke taifa pamoja na nina amini una uwezo wa kuliweka taifa pamoja na utaliweka taifa pamoja tunakuomba sana mama,”

Kuhusu mkutano huo wa wadau kujadili hali ya demokrasia nchini, Zitto amesema ni hatua kubwa katika kuelekea kuwa na majadiliano ya kisiasa.

“Sisi tunachukulia kuwa hii ni hatua muhimu katika kuelekea kuwa na majadiliano ya kisiasa katika nchi yetu, huu ni mwanzo mwema.

“Kila jambo lina mwanzo na huu ni mwanzo mwema, ninaamini Mungu atatuongoza kuwa na utaratibu wa kujadiliana na kutatua changamoto zetu kwa majadiliano,” amesema Zitto.

====

Pia soma;

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amevunja ukimya kuhusu kinachomkabili Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe akisema kuwa demokrasia ni kuheshimu sheria.

Akizungumza leo Jumanne Desemba 15, 2021 wakati akifungua mkutano wa wadau kujadili demokrasia ya vyama vingi, Rais Samia amesema ni muhimu kuzingatia sheria za nchi.

Mkuu huyo wa nchi ameyasema hayo akijibu ombi la Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) Zitto Kabwe aliyemuomba kusaida kuachiwa kwa Mbowe ambaye pamoja na wenzake watatu wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 16/2021 yenye mashtaka sita yakiwemo ya kula njama na kufadhili vitendo vya kigaidi, inayoendelea katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.

Rais Samia amesema, “Nataka nijibu lile ombi la mwanangu, iko hivi demokrasia ni kuheshimu sheria, unapoheshimu sheria ndipo demokrasia inapokua, lakini pia ndipo inapoleta heshima.

“Heshima ya mtu inakuja unapoheshimu sheria za nchi, unapovunja sheria za nchi heshima yako haitaheshimiwa, Serikali haitakuheshimu lakini lazima ujue kwamba unapotumia uhuru wako mwisho wa uhuru wako inaanza heshima ya mtu mwingine,”.

Ameendelea,’’Isingekuwa uvunjifu wa sheria leo isingemlazimu Zitto kuomba hapa kwamba yule mwenzetu muachie lakini unapovunja sheria unajivunjia heshima

“Naomba tufanye kazi kwa kuheshimu sheria, waswahili wanasema mtaka nyingi nasaba hupata mingi misiba, ingawa kusameheana nako kupo,” amesema Samia.

Chanzo cha cha habari ni Gazeti la Mwananchi

]
 
Attachments

  • twitter_2021121-1639627759032.mp4
    7.2 MB
Akijibu ombi la Mheshimiwa Zitto leo kuhusu ombi la kumwachilia Mbowe ili kuweka nchi kwenye mshikamano wa Kitaifa.

Mh. Samia mesema kwanza afuate sheria pili awe na heshima.

Tofauti na tuhuma alizosema huko nyuma wakati akihojiwa na BBC kuwa Mbowe ana tuhuma za ugaidi.
Kuna maswali muhimu ya kujiuliza
Afuate sheria gani? Kavunja sheria gani?
Amheshimu nani? Ni nani kamkosea heshima?
Kwahiyo kesi yake sio ugaidi tena? Bali ni maswala ya sheria na heshima?
 
Kwanza afuate sheria
Pili awe na heshima
[emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji848][emoji848][emoji848][emoji2827][emoji2827][emoji2827][emoji2827]
Mama aliona Mbowe kama anataka kumpanda kichwani kwa kampeni yake ya katiba mpya.

Hapa inadhihirisha tuhuma za Mbowe ni za kubumba.... Na pia kumwonyesha tu kuwa huwezi kushindana na serikali
 
Akijibu ombi la Mheshimiwa Zitto leo kuhusu ombi la kumwachilia Mbowe ili kuweka nchi kwenye mshikamano wa Kitaifa.

Mh. Samia mesema kwanza afuate sheria pili awe na heshima.

Tofauti na tuhuma alizosema huko nyuma wakati akihojiwa na BBC kuwa Mbowe ana tuhuma za ugaidi.
Kwa wenye akili timamu hili tulilijua toka mwanzo!!

Mbowe kusimamia msimamo wake wa harakati za upatikanaji wa katiba mpya , Rais katafsi ni kukosa adabu na kutofuata sheria za nchi!!

Rais pia kwa majibu yake katuonesha waziwazi kuwa majaji wake wanaosimamia kesi ya ile ya Ugaidi ni michongo mitupu na maelekezo kutoka kwake!
 
Hili amedhihirisha wazi pasi na shaka kuwa kosa la Mbowe ni kampeni yake ya kudai katiba mpya na sio ugaidi.
 
Akijibu ombi la Mheshimiwa Zitto leo kuhusu ombi la kumwachilia Mbowe ili kuweka nchi kwenye mshikamano wa Kitaifa.

Mh. Samia mesema kwanza afuate sheria pili awe na heshima.

Tofauti na tuhuma alizosema huko nyuma wakati akihojiwa na BBC kuwa Mbowe ana tuhuma za ugaidi.
Kumbe kutokuwa na Heshima kunazaa kesi ya Ugaidi hahahaha
 
Back
Top Bottom