Akijibu ombi la Mheshimiwa Zitto leo kuhusu ombi la kumwachilia Mbowe ili kuweka nchi kwenye mshikamano wa Kitaifa, Mh. Samia amesema kwanza afuate sheria pili awe na heshima.
Tofauti na tuhuma alizosema huko nyuma wakati akihojiwa na BBC kuwa Mbowe ana tuhuma za ugaidi.
Lissu anasema Mbowe hawezi samehewa sababu hana hatia na hajahukumiwa; wadau wa CHADEMA wanalalamika kwanini Zitto aombe msamaha? Msamaha wa kosa lipi?
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewakumbusha viongozi wa vyama vya siasa kuzingatia na kutii sheria ili kuepuka heshima zao kuondoka.
Rais Samia ameeleza hilo leo wakati akijibu ombi la Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo Ndugu Zitto Kabwe ambaye alimuomba awasaidie kumsamehe Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe.
''Nataka nizungumzie kidogo aliloniomba mwanangu Zitto, kwamba yule mwenzetu msamehe basi aje awe na sisi. Demokrasia ni kuheshimu sheria, heshima ya mtu inakuja kwa kuheshimu sheria za nchi.,'' ameeleza Rais Samia Suluhu.
Ameendelea,’’Isingekuwa uvunjifu wa sheria leo isingemlazimu Zitto kuomba hapa kwamba yule mwenzetu muachie lakini unapovunja sheria unajivunjia heshima
“Naomba tufanye kazi kwa kuheshimu sheria, waswahili wanasema mtaka nyingi nasaba hupata mingi misiba, ingawa kusameheana nako kupo,” amesema Samia.
Aidha Rais Samia amesisitiza kuwa kuna taifa moja tu ambalo raia wote wanawajibika kulilinda.
====
Zaidi soma;
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Zitto Kabwe amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kusaidia kuachiwa kwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.
Zitto ambaye pia ni kiongozi wa Chama Cha ACT-Wazalendo ametoa ombi hilo leo wakati wa mkutano wa wadau wa kujadili hali ya demokrasia ya vyama vingi nchini.
Mbowe na wenzake watatu wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 16/2021 yenye mashtaka sita yakiwemo ya kula njama na kufadhili vitendo vya kigaidi, inayoendelea katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.
Akizungumza kwa sauti ya upole Zitto amesema, “Sisi viongozi wa vyama tupo hapa na wengine hawapo kwa sababu zao lakini kuna mwenzetu hayupo hapa kwa sababu ya changamoto za kisheria.
Tuna utamaduni wa kumaliza haya mambo na haitakuwa mara ya kwanza, tunakuomba sana kwa mujibu wa sheria na kufuata taratibu tusaidie mwenzetu tuwe naye ili tuweze kufanya kazi kwa pamoja na kuunganisha nchi yetu, tufanye siasa za tija na maslahi kwa nchi yetu,”. Amesema Zitto nakuongeza
“Ni dhahiri kuna changamoto za hapa na pale na wewe ndio Rais wetu, tunakuomba sana kama ambavyo uliahidi katika hotuba yako ya kwanza wakati unazindua Bunge.
“Utuunganishe, tumepalanganyika, uliweke taifa pamoja na nina amini una uwezo wa kuliweka taifa pamoja na utaliweka taifa pamoja tunakuomba sana mama,”
Kuhusu mkutano huo wa wadau kujadili hali ya demokrasia nchini, Zitto amesema ni hatua kubwa katika kuelekea kuwa na majadiliano ya kisiasa.
“Sisi tunachukulia kuwa hii ni hatua muhimu katika kuelekea kuwa na majadiliano ya kisiasa katika nchi yetu, huu ni mwanzo mwema.
“Kila jambo lina mwanzo na huu ni mwanzo mwema, ninaamini Mungu atatuongoza kuwa na utaratibu wa kujadiliana na kutatua changamoto zetu kwa majadiliano,” amesema Zitto.
====
Pia soma;
Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amevunja ukimya kuhusu kinachomkabili Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe akisema kuwa demokrasia ni kuheshimu sheria.
Akizungumza leo Jumanne Desemba 15, 2021 wakati akifungua mkutano wa wadau kujadili demokrasia ya vyama vingi, Rais Samia amesema ni muhimu kuzingatia sheria za nchi.
Mkuu huyo wa nchi ameyasema hayo akijibu ombi la Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) Zitto Kabwe aliyemuomba kusaida kuachiwa kwa Mbowe ambaye pamoja na wenzake watatu wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 16/2021 yenye mashtaka sita yakiwemo ya kula njama na kufadhili vitendo vya kigaidi, inayoendelea katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.
Rais Samia amesema, “Nataka nijibu lile ombi la mwanangu, iko hivi demokrasia ni kuheshimu sheria, unapoheshimu sheria ndipo demokrasia inapokua, lakini pia ndipo inapoleta heshima.
“Heshima ya mtu inakuja unapoheshimu sheria za nchi, unapovunja sheria za nchi heshima yako haitaheshimiwa, Serikali haitakuheshimu lakini lazima ujue kwamba unapotumia uhuru wako mwisho wa uhuru wako inaanza heshima ya mtu mwingine,”.
Ameendelea,’’Isingekuwa uvunjifu wa sheria leo isingemlazimu Zitto kuomba hapa kwamba yule mwenzetu muachie lakini unapovunja sheria unajivunjia heshima
“Naomba tufanye kazi kwa kuheshimu sheria, waswahili wanasema mtaka nyingi nasaba hupata mingi misiba, ingawa kusameheana nako kupo,” amesema Samia.
Kwanza afuate sheria
Pili awe na heshima
[emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji848][emoji848][emoji848][emoji2827][emoji2827][emoji2827][emoji2827]
Kuna maswali muhimu ya kujiuliza
Afuate sheria gani? Kavunja sheria gani?
Amheshimu nani? Ni nani kamkosea heshima?
Kwahiyo kesi yake sio ugaidi tena? Bali ni maswala ya sheria na heshima?
Mbowe hayupo juu ya sheria, ameshtakiwa kisheria atahukumiwa kwa sheria na kama akishinda ni kwa sheria. Sio kwamba akishinda alikuwa kaonewa ni kwa sababu ametumia udhaifu wa sheria
Kwanza afuate sheria
Pili awe na heshima
[emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji848][emoji848][emoji848][emoji2827][emoji2827][emoji2827][emoji2827]
Mimi ningependa Mbowe afungwe jela na kifungo chake ndicho kitapelekea Watanzania kwa wingi kukiondoa chama changu cha CCM madarakani kwenye uchaguzi ujao wa mwaka 2025.
Kwanza afuate sheria
Pili awe na heshima
[emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji848][emoji848][emoji848][emoji2827][emoji2827][emoji2827][emoji2827]
kwa hiyo ugaidi wa Mbowe ni kukosa heshima kwa kudai katiba.
usikute Mbowe alipigiwa simu na mama kuombwa aache harakati za katiba,akamwambia mama acha ufala 🤣🤣🤣🤣
Kuna maswali muhimu ya kujiuliza
Afuate sheria gani? Kavunja sheria gani?
Amheshimu nani? Ni nani kamkosea heshima?
Kwahiyo kesi yake sio ugaidi tena? Bali ni maswala ya sheria na heshima?