Rais Samia: Demokrasia siyo Cocacola

Rais Samia: Demokrasia siyo Cocacola

akisema kila eneo lina demokrasia yake, mila na desturi zetu hazimtambui mwanamke kama kiongozi.

Mwambieni huyu mtu hii nchi sio kikundi cha kikoba ajifunze kuweka akiba ya maneno.
Utamaduni gani haumtambui mwanamke kama kiongozi, wa waarabu au wa kabila lenu?
 
Hapo umesema kitu. Sasa mwambie dpp asiendelee na kesi ya mwanamapinduzi Sabaya maana alikua anatekeleza kazi maaluum alizopewa na mtangulizi wako kupambana na ufisadi.
Ataachiwa tu siku sio nyingi. Alitaka afanye fair angalau kuwafuta machozi wapinzani, kumbe wapinzani wenyewe ndo akina Mbowe, joka ambalo kamwe halifugiki litaishia kukumeza na kukuangamiza.
 
Umeshawahi kumuona Sheikh wa kike?

Au kwenye ukoo wenu kiongozi wa ukoo ni wa kike??
Ndo maana nimekwambia utamaduni wa waarabu? Kama ni dini tumeipenda tutai adopt alaf tutaifanya iendane na tamaduni zet.

Kabila langu au ukoo wangu kuna wanawake ambao ni viongozi na viungo muhimu kweny familia na ukoo.
 
Sasa kama sio cocacola yeye nani aliyemwambia 2025 ni zamu ya wanawake.

Kuwa sasa ni fanta?
 
Kabisa, mfano sisi tuna jamukaya tu jambo drinks fulani amazing
 
na 2025 atapita kwa kishindo tu hatakama atapiga kampeni mikoa 3 tu
 
HII YA KWETU KAMA SIYO COCACOLA, INAITWAJE???

au mnaonaje tukaiita mirinda nyeusi!!
 
Ni sahihi, msingi wa demokrasia utabaki kuwa wananchi wafanye maamuzi kwaajili ya mambo yao/ushirikishwaji wa wananchi.

Tatizo liko hapo kwenye ushirikishwaji wa wananchi ,na hii ni pale tunapochagua watu wa kutuwakilisha kwenye maamuzi.

Tukikosa watu sahihi ni dhahiri uwakilishwaji pia hautakuwa mzuri.

Sanduku la kura halitakiwi kuchezewa hata kidogo kwa ustawi wa jamii yetu.

Kazi iendelee [emoji120][emoji120]
 
Back
Top Bottom