LGE2024 Rais Samia: Dhamira ya Serikali ni kuona Uchaguzi unafanyika kwa Haki

LGE2024 Rais Samia: Dhamira ya Serikali ni kuona Uchaguzi unafanyika kwa Haki

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,


Kupata taarifa na matukio ya kimkoa kuhusu Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Ndugu Wananchi kesho Jumatano (Novemba 27, 2024) ni siku ambayo tutaendeleza utamaduni wetu wa kupata viongozi wetu kwa njia ya Uchaguzi. Tutakwenda kuchagua viongozi wetu wa mtaa vijiji na Vitongoji kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Hii ni fursa muhimu ya kupiga kura kuchagia maendeleo ya nchi kwa njia ya Kidemokrasia kwa kuchagua viongozi wenye sifa. Serikali za Mitaa ni msingi wa ujenzi wa Taifa Imara na lenye maendeleo endelevu kupitia viongozi tunaowachagua tunaweka mazingira thabiti ya uwajibikaji, utoaji wa huduma bora kwa Wananchi na Wasimamizi wa mali za umma.

Ni fursa ya kuhakikisha kuwa maamuzi yanayohusu jamii zetu yanatokana na mahitaji halisi ya Wananchi, kila kura inayopigwa ina maana na itasaidia kufanikisha azma yetu ya kujenga jamii yenye haki, usawa na maendeleo kwa wote.

Ndugu zangu Uchaguzi ni haki yetu na ni jukumu letu kuhakikisha tunatumia haki hiyo kwa amani na utulivu. Hivyo, niwasihi Wananchi wajiepushe na vitendo vya uchochezi, vurugu au uvunjifu wa sheria. Amani ni urithi wetu wa thamani na ni wajibu wetu kuilinda kwa gharama yoyote ile. Aidha, ni muhimu kuheshimu maamuzi ya Wapiga Kura kwani Demokrasia yenye nguvu hujengwa kwa misingi ya heshima.

Natumia Fursa hii kuwakumbusha Wananchi wote waliojiandikisha kupiga kura kuhakikisha Wanajitokeza haki yao ya kikatiba, niwasihi mtumie fursa hiyo kuchagua Viongozi waadilifu wenye ubunifu na wenye maono ya kuendeleza jamii zetu. kumbukeni kila kura ina umuhimu mkubwa katika kuamua mustakabali wa maendeleo yetu na taifa kwa ujumla.

Viongozi wa Vyama vya siasa, wagombea na Mawakala wa Uchaguzi niwakumbushe uzingatia na kuheshimu sheria na kanuni za uchaguzi. Aidha, nawasihi wasimamizi wa Uchaguzi na wote wanaohusika wahakikishe uchaguzi unafanyika kwa haki uwazi na kuzingatia taratibu zilizokubaliwa na Wadau

Ni matumaini yangu kuwa mtaendelea kutekeleza jukumu langu kwa weledi, kulinda haki za Wananchi na kudumisha utulivu tunapoelekea mwisho wa mchakato huu. Ndugu Wananchi ni dhamira ya Serikali kuhakikisha Uchaguzi unafanyika kwa uwazi na kuzingatia kanuni za Uchaguzi zilizopo. Nito rai kwa kila mdau wa Uchaguzi huu kutoa ushirikino ili kuhaiisha uchaguzi huu unakuwa wa amani na unaoakisi taswira yetu kama taifa lenye mshikamano na Demokrasia imara

Niwakumbushe kuwa vituo vya kupigia kura vipo kwenye mitaa yote nchini, kwenye majimbo ya umma na vituo hivyo vitafunguliwa saa mbili asubuhi na kufungwa saa 10 jioni. Napenda kuwahakikishia kuwa maamuzi yenu katika sanduku la kura yataheshimiwa.

Nawatakia uchaguzi mwema wenye mafanikio, amani na mshikamano.

Asanteni kwa kunisikiliza
 
Alipo sema viongozi wa serikali za mitaa ndio msingi wa maendeleo ya taifa najaribu kufikiria vipi inakuwa hivyo maana mimi binfsi zaidi ya kupata mhuri wa mwenyekiti wa mtaa na wajumbe wake sijawahi kuona hao viongozi wakijishughulisha na shughuli zozote hapa mtaani miaka mitano yote iliyo pita.
 
Hii ndio Kauli aliyoitoa Rais wa Tanzania, Mh.DKT Samia Suluhu Hassan kuelekea Siku ya Uchaguzi wa Wenyeviti wa serikali za Mitaa, kama alivyonukuliwa na Vyombo vya Habari.

Screenshot_2024-11-26-19-41-45-1.png


Toa Maoni Yako
 
Hii ndio Kauli aliyoitoa Rais wa Tanzania, Mh.DKT Samia Suluhu Hassan kuelekea Siku ya Uchaguzi wa Wenyeviti wa serikali za Mitaa, kama alivyonukuliwa na Vyombo vya Habari.

View attachment 3162417

Toa Maoni Yako
Kama hakusema lolote katika upuuzi uliofanyika katika kuandikisha, kuenguliwa , kukataa kuwaapisha leo, wapinzani , MSIMUAMINI! KESHO HAKUNA MPINZANI ATAKAYE TANGAZWA!
 
Back
Top Bottom