LGE2024 Rais Samia: Dhamira ya Serikali ni kuona Uchaguzi unafanyika kwa Haki

LGE2024 Rais Samia: Dhamira ya Serikali ni kuona Uchaguzi unafanyika kwa Haki

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
..Raisi alisema falsafa yake ni 4R. Wateule wake wote wameipuuza, wanafanya yao.

..Raisi katoa amri uchaguzi uwe wa haki. Maagizo hayo nayo yamepuuzwa hata na Waziri ambaye ni mkwe wake.

..Kwa kifupi Samia Suluhu anadharauliwa na wateule wake. Kazi ya Uraisi imemshinda.
Labda kuna maelekezo ja jukwaani na ya kifamilia. Kufumbia macho ni kukubaliana na yanayoendelea. Huu uchaguzi unavyoendeshwa ndio uchaguzi wa haki waliokubaliana wote.

Amandla...
 
Labda kuna maelekezo ja jukwaani na ya kifamilia. Kufumbia macho ni kukubaliana na yanayoendelea. Huu uchaguzi unavyoendeshwa ndio uchaguzi wa haki waliokubaliana wote.

Amandla...

..sasa hapa Mama ajitenge na uchafu unaoendelea, au awe sehemu ya uchafu huo.
 
Wakuu,


Kupata taarifa na matukio ya kimkoa kuhusu Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Ndugu Wananchi kesho Jumatano (Novemba 27, 2024) ni siku ambayo tutaendeleza utamaduni wetu wa kupata viongozi wetu kwa njia ya Uchaguzi. Tutakwenda kuchagua viongozi wetu wa mtaa vijiji na Vitongoji kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Hii ni fursa muhimu ya kupiga kura kuchagia maendeleo ya nchi kwa njia ya Kidemokrasia kwa kuchagua viongozi wenye sifa. Serikali za Mitaa ni msingi wa ujenzi wa Taifa Imara na lenye maendeleo endelevu kupitia viongozi tunaowachagua tunaweka mazingira thabiti ya uwajibikaji, utoaji wa huduma bora kwa Wananchi na Wasimamizi wa mali za umma.

Ni fursa ya kuhakikisha kuwa maamuzi yanayohusu jamii zetu yanatokana na mahitaji halisi ya Wananchi, kila kura inayopigwa ina maana na itasaidia kufanikisha azma yetu ya kujenga jamii yenye haki, usawa na maendeleo kwa wote.

Ndugu zangu Uchaguzi ni haki yetu na ni jukumu letu kuhakikisha tunatumia haki hiyo kwa amani na utulivu. Hivyo, niwasihi Wananchi wajiepushe na vitendo vya uchochezi, vurugu au uvunjifu wa sheria. Amani ni urithi wetu wa thamani na ni wajibu wetu kuilinda kwa gharama yoyote ile. Aidha, ni muhimu kuheshimu maamuzi ya Wapiga Kura kwani Demokrasia yenye nguvu hujengwa kwa misingi ya heshima.

Natumia Fursa hii kuwakumbusha Wananchi wote waliojiandikisha kupiga kura kuhakikisha Wanajitokeza haki yao ya kikatiba, niwasihi mtumie fursa hiyo kuchagua Viongozi waadilifu wenye ubunifu na wenye maono ya kuendeleza jamii zetu. kumbukeni kila kura ina umuhimu mkubwa katika kuamua mustakabali wa maendeleo yetu na taifa kwa ujumla.

Viongozi wa Vyama vya siasa, wagombea na Mawakala wa Uchaguzi niwakumbushe uzingatia na kuheshimu sheria na kanuni za uchaguzi. Aidha, nawasihi wasimamizi wa Uchaguzi na wote wanaohusika wahakikishe uchaguzi unafanyika kwa haki uwazi na kuzingatia taratibu zilizokubaliwa na Wadau

Ni matumaini yangu kuwa mtaendelea kutekeleza jukumu langu kwa weledi, kulinda haki za Wananchi na kudumisha utulivu tunapoelekea mwisho wa mchakato huu. Ndugu Wananchi ni dhamira ya Serikali kuhakikisha Uchaguzi unafanyika kwa uwazi na kuzingatia kanuni za Uchaguzi zilizopo. Nito rai kwa kila mdau wa Uchaguzi huu kutoa ushirikino ili kuhaiisha uchaguzi huu unakuwa wa amani na unaoakisi taswira yetu kama taifa lenye mshikamano na Demokrasia imara

Niwakumbushe kuwa vituo vya kupigia kura vipo kwenye mitaa yote nchini, kwenye majimbo ya umma na vituo hivyo vitafunguliwa saa mbili asubuhi na kufungwa saa 10 jioni. Napenda kuwahakikishia kuwa maamuzi yenu katika sanduku la kura yataheshimiwa.

Nawatakia uchaguzi mwema wenye mafanikio, amani na mshikamano.

Asanteni kwa kunisikiliza

Haki gani wakati mpaka sasa umekuwa uchafu na sio uchaguzi tena
 
Rais anongea kama maiti. Hakuna dhamira ya vitendo hizi ni kauli mfu.
 
..sasa hapa Mama ajitenge na uchafu unaoendelea, au awe sehemu ya uchafu huo.
Kama nilivyosema awali, kama hapendezwi na yanayoendelea angeisha toa tamko na kuwachukulia hatua wahusika. Kama kiongozi, ni ama hapendezwi au anapendezwa. Hawezi kujitenga na kusema hayamhusu.

Amandla...
 
Back
Top Bottom