LGE2024 Rais Samia: Dhamira ya Serikali ni kuona Uchaguzi unafanyika kwa Haki

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Mambo ya hovyo sana yanafanyika hapa nchini. Huku mawakala wananyimww viapo kule wakubwa wao wanahubiri haki feki.
 



Mama anaongea wa vitoto vyake! Yaani kila mtu amekuwa kama vitoto siku hizi tunacho ambiwa sawa Mama hata uongo. Nchi inaenda pabaya. Sasa hiyo mikataba kuna ukweli huko kama tunadanganywa kitoto kitoto hivi
 
Unaota?

Mama tushampa 5 mingine kabla ya 2025. Hulijuwi hilo?
Kwa wizi huu wa kura na kuenguana hakuna hata haja ya chaguzi fake ni kupeteza pesa tu. Ni bora tungebadilisha katiba kuliko kuwa na mfumo fake na serikali fake hivi kwa mawazo yangu
 
Natamani kuandika tusi lkn nashindwa kwasabb mwanasheria wangu naye kawa chawa wake.
 
Na hiyo ndio furaha ya watawala kuona watawaliwa hawajali mambo yanayoamua hatma yao ya kesho.
Usiwe na hofu ndugu, hatma yako ya kesho anayo Muumba wako, ukiruhusu muumba wako kutawala maisha yako wala hawa kanyaboya hutawaona kikwazo kwa chochote, infact hutawaona kabisa.
 
chura kiziwi hana lolote,wapinzani wanaenguliwa wanapigwa wanatekwa yupo tu bila kusema kauli kama raisi wa nchi
 
Hana hata chembe ya aibu kusema dhamiri ya serikali ni kufanya uchaguzi wa haki?
 
Watanzania ni watu wavumilivu sana, siku tukipata watu tofauti wa kutuongoza zaidi ya CCM ya sasa tutapiga hatua tuwe kama Singapore kabisa...
CCM ya sasa sio ya zamani - hawa wa sasa ni chama kwanza, taifa na watu baadae..
 
Haya shime kura ni maisha yako!
 
Mwalimu Julius Nyerere kwenye moja ya hotuba zake anasema "huwezi kuniua kwa nia njema, halafu useme 'hukuniua'. Umeniua!" Dhamira njema ya serikali haitoshi. Inabidi kwenda mbali zaidi. Mchakato wa uchaguzi huu ungeweza kufanyika kwa namna bora, kama maoni ya wadau waliyotoa yangesikilizwa ili kupunguza malalamiko, na inawezekana kuwa na mchakato bora. Tutakuwa tukirudia matatizo/makosa yale yale, na hapa maneno ya Albert Einstein yanakuwa 'relevant'. "We cannot solve our problems with the same thinking we used when we created them."
 
Ninaamini kila kitu Afrika ni magumashi, hata nyumba za Ibada. Anaingiaje nyumba za Ibada halafu wanamuangalia tu bila kumuambia uovu wake? Huu ni uchaguzi kweli?
 
Usiwe na hofu ndugu, hatma yako ya kesho anayo Muumba wako, ukiruhusu muumba wako kutawala maisha yako wala hawa kanyaboya hutawaona kikwazo kwa chochote, infact hutawaona kabisa.
Kuna mambo Muumba alituachia tufanye wenyewe ndio maana hajatuumba kama mbuzi au ng'ombe.
 
Kuna mambo Muumba alituachia tufanye wenyewe ndio maana hajatuumba kama mbuzi au ng'ombe.
Basi fanya uwe raisi wewe, au muweke Mbowe au Lisu,...huko America kuna wanaotamani kuhama saizi kisa kaingia Trump... human systems have proven to be so inhuman... Mungu anatosha.
 
Kwa vipi?

Amandla...

..Raisi alisema falsafa yake ni 4R. Wateule wake wote wameipuuza, wanafanya yao.

..Raisi katoa amri uchaguzi uwe wa haki. Maagizo hayo nayo yamepuuzwa hata na Waziri ambaye ni mkwe wake.

..Kwa kifupi Samia Suluhu anadharauliwa na wateule wake. Kazi ya Uraisi imemshinda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…