Rais Samia fahamu kwamba Wakurugenzi wa Halmashauri, Maafisa elimu, Wakuu wa wilaya na walimu wakuu wana mtandao wa wizi wa pesa za madarasa

Rais Samia fahamu kwamba Wakurugenzi wa Halmashauri, Maafisa elimu, Wakuu wa wilaya na walimu wakuu wana mtandao wa wizi wa pesa za madarasa

robinson crusoe

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2020
Posts
762
Reaction score
1,236
Mimi ni mwalimu wa miaka mingi. Nina mates wangu wengi ktk taaluma ya ualimu mikoa mingi ya nchi hii. Hii siyo mara ya kwanza kuwa na ujenzi wa madarasa, tatizo ni ubora duni unaotokana na wizi wa watendaji wakuu wilayani na halmashauri. Wizi mkubwa ni wa Sementi, mbao na mabati kiasi kwamba sakafu hugeuka vumbi ktk kipindi cha mwaka mmoja tu!

Sasa wizi umeanza, Ninapowasiliana na waalimu wenzangu ktk mikoa 10 ambayo nina mawasiliano nao; Kigoma, Mwanza, Mara, Singida, Lindi, Morogoro, Manyara, Singida, simiyu na Katavi wote wanaeleza kupigiwa simu na maafisa elimu na tayari pesa zimeliwa wakisema pia zinahitajika na wakuu wa wilaya. Mkoa wa kigoma wameanzisha mtindo wa kuziba pengo kwa kuwatumia wanafunzi kama vibarua wa ujenzi huo hadi kuponda kokoto na kukoroga zege.

Mwanza wao wanadai nguvu ya wananchi itumike ili kuunga mkono msaada wa serikali. Kwa mtindo huu rais usitegemee lolote la maana. Huku wilayani huna wasimamizi, ni wezi tu!
 
Nakumbuka kipindi cha MMEM watu walipiga hela sana.mama anipe ukuu wa wilaya moja wapo.nikasimamie.najua mbinu zote wanazotumia kuiba.jiulize swali rahisi.hela za madarasa ya MMEM na MEbado tuna sha ya madarasa.id
 
Kuna wilaya moja mkoa wa pwani qamwpanga kufisadi Kama milioni 100 hivi.
 
Acha waongeze mzunguko wa pesa mtaani.... Mama amefungua nchi,...

Chawa wa mama wanakuja utawasikia...."sukuma gang awamu yenu imeisha.."
 
Hakuna watu wezi kama maafisa elimu wilaya,wengi wao ni wabinafsi sana
 
Jua ya kwamba upigaji ni ngumu sana kuutokomeza.
 
Back
Top Bottom