Rais Samia, fanya mabadiliko ya wasaidizi wako hasa Kwenye hotuba; unaweza ukawa na wasomi ila siyo wataalam wala wazoefu

Basi kwa kuwa mama kwa kinywa chake kasema taifa lina akiba ya pesa za kigeni dola za marekani zaidi ya elfu 6 bilioni basi tulipe deni letu la dola bilioni 30 halafu zingine tutajua namna ya kuzitumia.
#rais hakosei.
Poropaganda hana hiyo hela huyo kaipata wali?
 
Kipenzi chako wewe!
 
... kwa mfano, maelfu tuliotimuliwa kwenye biashara zetu kwa kisingizio cha umachinga tulitarajia kusikia neno la serikali kutoka kwa Mkuu wa nchi.

Kisingizio? We umetimiliwa maana umevamia eneo la barabara hakuna lolote ataambiwa zaidi ya "marufuku kufanya biashara hapa"
 
Usimpangie rais nini cha kusema,kama unaona vipi kahutubue familia yako

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Ni kweli kwa hotuba ya mwaka kuwa dkk 18-20 ,ni hotuba fupi sana ambayo haiwezi kutoa fafanuzi mbalimbali kama tulivyotaarifiwa na barua ya ikulu. Nami nashauri kwakuwa kumeonekana kipindi hiki kuna upotoshaji mwingi unaofanywa mpaka na viongozi wakubwa dhidi ya uongozi wa Mama, basi wasaidizi wake wanaomuandalia nondo, wajaribu kuingia in details ili Mama akizungumza basi mjadala unafungwa.kwamfano matumizi ya trilioni 1.3 Mama ameupiga mwingi sana kwa kujenga madarasa 15,000, vituo vya afya ambulance etc, so wananchi wanataka kuskia data za namna hiyo.Mambo ni mengi sana, kulipa wastaafu tuliona juzi katoa trillioni 2.7 kati ya 4, kulipa wakandarasi, miradi inaendelea etc. Mbona kipindi cha mwendazake chochote kinachofanyika kilikuwa kinaelezwa kinagaubaga hivyo kujipatia umaarufu mkubwa na wananchi kuwa na uelewa mkubwa wa namna serikali inavyowahudumia. so ni vizuri twende na mfumo huo huo kwa Mama ili awe branded vizuri kwa wananchi.Tunamuombea aendelee na trend hii hasa kusaidia maendeleo ya jamii (watu) .asalaam aleykum
 
Amina mkuu!
 
Wengi walishaacha kumsikiliza, wanaomsikiliza ni wale wenye upeo kama wake.
Mimi naamini kwamba tumpe muda Mh Rais na tuendelee kutoa maoni yetu kwa nia njema kwa ajili ya ustawi wa taifa na si kwa ustawi wa vikundi vya upigaji ambavyo vitakuwa vitakuwa vinasifu hata vile visivyostahili kusifu, na pia vikundi vingine ambavyo vimebaniwa upigaji vitakuwa vinaponda kila kitu anachofanya Mh Rais hata kama ni vya manufaa kwa taifa, Sisi wengine tupo neutral hatupo team A wala team B, NAWATAKIA WATANZANIA WOTE HERI YA MWAKA MPYA "
 
Jamani EEE nilisema hapa huyu mama aache mtindo wa kusoma hotuba atalemaa Sasa mmesikia kaandikiwa hotuba kwamba nchi Ina akiba ya US $ Dola 6000 bilion Sasa hapo hata Deni la Taifa lingelipwa mama kubali tu kazi hii kwako ni overloaded kwako .
 
TATIZO HAWAKUWA WAMEJIPANGA KUHUTUBIA TAIFA, WALIKURUPUKA BAADA YA KUPATA TAARIFA KUWA TUNDU LISU ATATOA HOTUBA YA MWISHO WA MWAKA
 
Jamani EEE nilisema hapa huyu mama aache mtindo wa kusoma hotuba atalemaa Sasa mmesikia kaandikiwa hotuba kwamba nchi Ina akiba ya US $ Dola 6000 bilion Sasa hapo hata Deni la Taifa lingelipwa mama kubali tu kazi hii kwako ni overloaded kwako .
yaani tuna akiba ya ths 1,426,934,600,000,000/=
 
Hakuna anayefundisha kazi mtu natoa ushauri maana tulitarajia ufafanuzi wa mambo nyeti kama demikrasia na uhuru,tozo,deni la taifa nk
Aliyetamka kuikandamiza atolee ufafanuzi gani.
 
WEWE UMESOMEA CHUO GANI CHA KUWEZA KUWASHAURI MAZUZU WAANZE KUTUMIA AKILI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…