Nadhani Moja ya eneo lenye tatizo Kwenye safu ya Mhe. Rais niwasaidizi wake. Inawezekana amepelekewa Watu bila kujua uzoefu wao, amepelekewa Watu wenye sense ya utumishi wa umma ila siyo wabunifu, amepelekewa Watu waliokuzwa kwenye security na siyo watendaji wenye kuelewa sekta zinaendeshwaje.
Mhe. Rais hotuba Yako ya mwisho wa mwaka imekosa NGUVU, imekosa manjonjo, umeacha wananchi na kiu yakujua Nini kinatokea mwakani. Hotuba haisemi kinagaubaga mwakani tujipangeje? Naomba nikukumbushe kwamba hotuba hii ndiyo ilipaswa kutoa dira ya vipaombele vya bajeti mwaka 2022, ndiyo ilipaswa kuwa wimbo wa watendaji waliochini lakini waliokuandalia awakuona umuhimu wakujiridhisha kiu ya wananchi ni ipi? May be umewashtukiza ila hata kama umewashtukiza wanapaswa kuwa na versions kwenye kabati zao ili wakati wowote utakapotaka kuzungumza na wananchi wanakuletea different version unapitia the best or your choice.
Naomba niangazie maeneo machache ambayo tulipaswa kusikia mwelekeo kwa 2022
1. Ni upi mkakati katika eneo la viwanda
2. Uwekezaji wa aina gani unategemewa 2022 Ili wananchi waelekeze rasilimali zao huko?
3. Nishati, kumekuwepo na changamoto ya nishati inayopelekea Watu kusita kuwekeza nchini,unawahakikishia Nini wawekezaji 2022 Kuhusu nishati yakuaminika?
4. Mawasiliano na Serikali mtandao katika kupanua na kurahisisha huduma, miundombinu ya mawasiliano, gharama za mawasiliano na huduma zinaimarishwa vipi? Nini Wizara na idara zifanye?
5. Tatizo la ajira, wananchi wategemea ajira au wajiajiri. Serikali itaajiri watu wangapi? Hii ingewafanya vijana kuacha bahasha za CV na kuanza ujasiriamali.
Haya ni baadhi ya maeneo tulitegemea hotuba Yako ijielekeze, je wasaidizi wako walishindwa kuandaa hotuba Kwa kuzingatia Mpango wa maendeleo? Tafuta watu wazoefu wenye hadhi ya ukatibu mkuu wakae kuandaa hizo hotuba, tafuta waandishi kama Togolani wakae na chipukizi , tafuta wanahabari wa aina ya Tido muhando wape kazi. Utaiona kazi rahisi sana, na hii itapunguza ukosoaji unaoendelea