Rais Samia, fanya mabadiliko ya wasaidizi wako hasa Kwenye hotuba; unaweza ukawa na wasomi ila siyo wataalam wala wazoefu

Rais Samia, fanya mabadiliko ya wasaidizi wako hasa Kwenye hotuba; unaweza ukawa na wasomi ila siyo wataalam wala wazoefu

Hotuba ni kitu personal. Kile unachotaka wewe ni cha kwako wewe na siyo Samia. Hata mimi ningetaka hotuba ya mwaka mpya ningeandika ya kwangu tofauti na hiyo ya kwako. All in all amefikisha ujumbe aliotaka uwafikie watanzania.

Still angeamua pia kutoongea. Acheni critique za kijinga
Wewe ndo unaleta ujinga! Huwezi kuchangia bila kutukana! Unaleta uchawa hapa! Yakiwepo mapungufu lazima tusema!
 
Unapokeaa mwakaa ukiwa wapi mkuu, embuu mwacheni mama afanye kwa nafasi yake aliyepewaa na MUNGU..
 
Nadhani Moja ya eneo lenye tatizo Kwenye safu ya Mhe. Rais niwasaidizi wake. Inawezekana amepelekewa Watu bila kujua uzoefu wao, amepelekewa Watu wenye sense ya utumishi wa umma ila siyo wabunifu, amepelekewa Watu waliokuzwa kwenye security na siyo watendaji wenye kuelewa sekta zinaendeshwaje.

Mhe. Rais hotuba Yako ya mwisho wa mwaka imekosa NGUVU, imekosa manjonjo, umeacha wananchi na kiu yakujua Nini kinatokea mwakani. Hotuba haisemi kinagaubaga mwakani tujipangeje? Naomba nikukumbushe kwamba hotuba hii ndiyo ilipaswa kutoa dira ya vipaombele vya bajeti mwaka 2022, ndiyo ilipaswa kuwa wimbo wa watendaji waliochini lakini waliokuandalia awakuona umuhimu wakujiridhisha kiu ya wananchi ni ipi? May be umewashtukiza ila hata kama umewashtukiza wanapaswa kuwa na versions kwenye kabati zao ili wakati wowote utakapotaka kuzungumza na wananchi wanakuletea different version unapitia the best or your choice.

Naomba niangazie maeneo machache ambayo tulipaswa kusikia mwelekeo kwa 2022
1. Ni upi mkakati katika eneo la viwanda

2. Uwekezaji wa aina gani unategemewa 2022 Ili wananchi waelekeze rasilimali zao huko?

3. Nishati, kumekuwepo na changamoto ya nishati inayopelekea Watu kusita kuwekeza nchini,unawahakikishia Nini wawekezaji 2022 Kuhusu nishati yakuaminika?

4. Mawasiliano na Serikali mtandao katika kupanua na kurahisisha huduma, miundombinu ya mawasiliano, gharama za mawasiliano na huduma zinaimarishwa vipi? Nini Wizara na idara zifanye?

5. Tatizo la ajira, wananchi wategemea ajira au wajiajiri. Serikali itaajiri watu wangapi? Hii ingewafanya vijana kuacha bahasha za CV na kuanza ujasiriamali.

Haya ni baadhi ya maeneo tulitegemea hotuba Yako ijielekeze, je wasaidizi wako walishindwa kuandaa hotuba Kwa kuzingatia Mpango wa maendeleo? Tafuta watu wazoefu wenye hadhi ya ukatibu mkuu wakae kuandaa hizo hotuba, tafuta waandishi kama Togolani wakae na chipukizi , tafuta wanahabari wa aina ya Tido muhando wape kazi. Utaiona kazi rahisi sana, na hii itapunguza ukosoaji unaoendelea
 
Shaban kissu alimuita magufuli kuwa ni hamnazo na bado yupo kwenye kuongoza (mc) kwenye mikutano ya Samia, tusubiri nae atapewa jina gani
 
Shida ni kwamba hamtaki kukubali kuwa mama yenu ni incompetent katika kila kitu, nyinyi kila anapofanya blunders mnasingizia wasaidizi wake inamaana yeye ni kondoo wa kukubali kila kitu anachopelekewa?

Akifanya kosa mnasema Sukuma gang ndo wanamhujumu, kaenda kukopa mahela kapeleka Zanzibar mnatafuta namna ya kumsafisha kwa kumsingizia Ngugai aliyehoji[emoji28].

Anapofanya makosa mwacheni awe accountable kama Rais wa nchi, unless otherwise mtuambie kama nchi inaongozwa na hao mnaowaita WASAIDIZI.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
29 December 2021
Bagamoyo, Tanzania

Wananchi wakata tamaa, wamechanganyikiwa hawajui serikali imejipanga vipi


Jamii ya wafugaji wa waishio kijiji cha Minduturieni wilayani bagamoyo nchini Tanzania bado wanaugulia maumivi ya ukame wa kati ya mwezi Septemba na Novemba 2021. Wafugaji wengi wamepoteza idadi kubwa ya mifugo na wana wasiwasi na hali yao ya chakula siku za usoni 2022 kwani wao wanategemea zaidi mifugo.
Source : BBC Swahili news
 
Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete walikuwa vipanga darasani.

Mwendazake na huyu sijajua historia zao za darasani zilikuwaje.

Hata kama unaandikiwa, inabidi personaly uwe vizuri kichwani, ukipitia ulichoandikiwa unapaswa kugundua nyufa mwenyewe.
Mwinyi alikuwa kipanga gani
 
Back
Top Bottom