Rais Samia funga mipaka haraka, huu ni mwaka wa ukame, hatuwezi kupiga kura na njaa tumboni

Rais Samia funga mipaka haraka, huu ni mwaka wa ukame, hatuwezi kupiga kura na njaa tumboni

Kujua bei ya mazao huwa haitoshelezi taarifa kuhusu mazao. Lazima ijulikane ni wapi? Pia gharama za usafirishaji kwenye canter au fuso au semi trela scania kutoka eneo lenye mazao kama mahindi,mpunga kuelekea kwenye mikoa mingine kama Dar, Mwanza, Dodoma, Pwani n.k
Oooh kumbe bas sawa.
 
Uzi huu ukipuuzwa msije sema hamkujua

Mahindi kidogo yaliyopatikana yanatoroshwa nchi jirani,mavuno hayakuwa mazuri,tutegemee njaa.

Huwezi kupiga kampeni au upige kura na njaa tumboni.
Mioaka ifungwe haraka kwa usalama wetu

Bashe yupo bize na kampeni hana habari
Mama anakula mema ya nchi hana habari.
Kama pesa yupo hakunaga kitu inaitwa njaa Acha uoga mkuu
 
Hii ni dalili kuwa huu mwaka njaa ipo
Wala bila ubishi, pembejeo zimekua ghali, na kilimo kinasua sua, mvua hakuna, mazao yanakauka bila hata kukomaa wala kuzaa.

Huu mwaka kazi ipoo.
 
Kwani hao wakulima wanamiliki mahindi ya Serekali? Hapa kwetu Songea serekali yenyewe inapeleka Mahindi Zambia
Yanasafiri ma canter kwa ma canter, kupitia njia ya Muhukuru - to border.

Haya cheki jua linavopiga sahivi, mazao yanakauka shambani hata hayazaa, itakuaje Kiangazi? Lol
 
Nimepita huku Simiyu ndani ndani huku vijiji vya Gasuma, Byuna, Nkindwabiye, Halawa, Nkololo, Gibishi, Bubale na Ng'washagata kuna Scania semi trela kutoka Kenya zinasomba mahindi balaa. Wakulima hawa masikini wanauza haya mahindi wakati wakijua hali ya mavuno siyo nzuri mwaka huu. Na serikali ipo inaangalia tu. Bongo! Kichwa cha Mwendawazimu! 😭
 
Shauri serikali inunue mahindi, mpunga yanayowadodea wakulima na siyo kufunga mipaka. Watu tuna magunia ya mahindi, mpunga na hatuna soko wewe unaleta habari za vijiwe vya kahawa.
Soko si lipo Kenya hapo kaka tembea kwanza kujua utauza wapi ili usitapeliwe mbona rahisi tu na Kenya mzigo wa mahindi unashusha kiwandani unalipwa hela yako unaondoka ila lazima upitie kwa agent wao..
 
Mwaka huu kutakua na njaa, mvua mizinguo sana
Dah basi Serikali inabidi ijiandae mapema ikabiliane na hii hali asee. Nakumbuka mwaka juzi kama siyo 2021 ama 2022 nilikuwa likizo Arusha wamasai Arusha walikuwa wanakuja mjini na kugonga hodi kabisa kuomba chakula hiyo hali ilinitia simanzi sana kulikuwa na ukame mbaya sana mifugo ilikufa.

Nyau de adriz
 
Bongo nchi ya ajabu,

Binafsi nashauri serikali iache mipaka wazi, ambae hawez kula ugali atakula ndizi na maji,

Bei za mazao ziwe juu kuvutia uwekezaji kwenye kilimo
 
Wazo zuri ila umechelewa mkuu, kuna mamia ya matruck ya kizambia pale songea yanabebelea mahindi to zambia kama haya akili nzuri.
Mkuu mkulima hayupo kushinda juani na kwenye mvua akilima ili kukupatia urahisi wa maisha ww na familia yako.

Hilo ni jukumu la serikali kununua mazao kwa wakulima na kukuuzia ww kwa bei nafuu unayo itaka ww.
 
Umemshauri vizuri. Nami pia naongezea. Wakati ambao kuna rais muislamu,hao marais wawe wanateua mawaziri wa maji ambao ni wakristu maana kiroho, roho za waislamu huwa ni kavu hazina chemchemi na roho za wakristu ni kama mto wenye chemchemi hai,mto unaotiririka. Wakristu tuna baraka za mvua na baraka nyinginezo nyingi.

Na hata sasa samia anatakiwa ambadilishe waziri wa maji aliyepo aweke mkristo, vinginevyo hali itazidi kuendelea kuwa mbaya nchi inaweza kuja kukumbwa na baa la njaa huko mbeleni.
Baba yako alifanya kosa kubwa sana kutonunua condom siku mama yako anatungwa mimba na wewe ukazaliwa.It was a wastage of time and space.Tungeepuka huu ujinga ulioandika.
 
Nimepita huku Simiyu ndani ndani huku vijiji vya Gasuma, Byuna, Nkindwabiye, Halawa, Nkololo, Gibishi, Bubale na Ng'washagata kuna Scania semi trela kutoka Kenya zinasomba mahindi balaa. Wakulima hawa masikini wanauza haya mahindi wakati wakijua hali ya mavuno siyo nzuri mwaka huu. Na serikali ipo inaangalia tu. Bongo! Kichwa cha Mwendawazimu! 😭
Ya kwamba serikali iwakataze watu kuuza mazao yao?
Hivi nyinyi watz mbona huwa hamueleweki mnataka nini?
Yaani mnataka gunia la mahindi liuzwe 50,000 na kilo ya mchele iuzwe 1000 alafu wakati huo mnataka vijana wajiajili kupitia kilimo.
 
Shauri serikali inunue mahindi, mpunga yanayowadodea wakulima na siyo kufunga mipaka. Watu tuna magunia ya mahindi, mpunga na hatuna soko wewe unaleta habari za vijiwe vya kahawa.
Naunga hoja asilimia mia
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Nenda nawewe songea ukalime Ili matruck hayo yabebe nayakwako!Waziri Bashe shikilia hapohapo mpaka mkulima naye atajirike
Huna unalolijua mkuu, hayo mahindi hauzi mkulima bali serikali.
 
Mavuno ya msimu wa 2023/2024 ni Tani milioni kumi na moja +, mahitaji ya ndani ya mwaka ni Tani milioni nane, kwa hiyo kuna bakaa ya Tani milioni tatu na akiba ya ghala la taifa la chakula huwa ni Tani Milioni moja laki mbili. Zambia walihitaji Tani 650,000 sidhani kama wamemaliza kuchukua Malawi walihitaji Tani 130,000 sidhani kama walilipia maana hata kuchukua hawajaanza. Kwa upande wa mkulima kulima heka moja ya mahindi na kuihudumia mpaka unavuna inahitaji wastani wa Tsh. 600,000 hapo anaweza akavuna wastani wa gunia 15 mpaka 25. Wastani wa bei ya mahindi ni 560-790 kwa kilo wastani wa chini ni Mkoa wa Geita(Nyawilimilwa, Nyehunge...) na wa kati ni Songwe, Songea na wastani wa juu ni Sumbawanga, Dar Es Salaam n.k.
Masoko ya Mahindi kutoka Tanzania.
-Congo kwa kilo 1,420Tsh. ( Kalemie, Lubumbashi n.k.)
-Malawi kwa kilo 960Tsh. ( Blantyre)
-Mozambique kwa kilo 1,000TshTsh. (Catandica)
-Zambia kwa kilo 883Tsh. (Lusaka, Kitwe, Ndola)
Pia kati ya hayo masoko baadhi yamejifunga kwa kuwa hayana faida na mengine sera za nchi husika hazijazuia ila wameweka bei ambazo ni ngumu kupeleka mizigo na changamoto ya mabadiliko ya fedha kutoka fedha za nchi hiyo kurejesha kwenye shilling ya Tanzania.
Kwa kifupi hata serikali yenyewe inauza mzigo kwenda nje kama unahitaji waone NFRA.
Suala la kuzuia chakula kwenda nje kwa hesabu za kistatistiki si sawa kwa kuwa hata mavuno ya 2024/2025 yakiwa asilimia 80% ya mavuno ya msimu uliopita bado nchi itakuwa na bakaa na hesabu ya mbolea zilizoenda kwa wakulima inaonyesha kuwa nchi itavuna sana na hii hali ya ukame kwa taarifa za TMA hawajatoa taarifa ya hatari kuhusu ukame ingawa kuna baadhi ya maeneo hakuna mvua za kuridhisha lakini haionyeshi inchi ikiingia kwenye majanga ya uhaba wa chakula.
 
Ni mikoa gani inazungumziwa, maana wakulima wakubwa wa mahindi ni nyanda za juu kusini, na wanavuna kuanzia mwezi wa tano, sasa hayo mavuno kidogo ni mkoa gani
 
Back
Top Bottom