mwanamichakato
JF-Expert Member
- Mar 20, 2015
- 1,188
- 1,090
Pongezi kwako Mh Rais wetu kwa mageuzi yenye tija ktk nyanja kadhaa.
Maendeleo ni mchakato endelevu na wenye kuhitaji dira imara na maamuzi thabiti ya kimapinduzi.
Tunajenga miundombinu (Barabara,Viwanja vya ndege, Bandari, Vyuo, mifumo ya umwagiliaji,usambazaji maji na kadhalika gharama kubwa zinatumika kugaramia ujenzi husika lengo likiwa kuchochea maendeleo ya wananchi wetu na taifa kwa ujumla.
Nadhani tuangalie uwezekano wa serikali kuwekeza zaidi kwenye kilimo kwa malengo ya kuhakikisha nchi ikijitegemea ndani ya miaka 5 ijayo na kuepuka kuagiza chakula ,Mafuta, Sukari na bidhaa zingine mtambuka..
Uwekezaji husika ufanywe kwa ubia kati ya taasisi za umma+sekta binafsi ()..Mathalani tuna wakulima wamethubutu kulima ekari 500,1000,5000 hawa wapewe mitaji ya kimkakati (utaalamu ,mitambo na fedha ). Wawezeshwe wakulima waliopo field tayari sio vijana waliokosa dira kimaisha na wenye tamaa ya kutajirika ndani ya muda mfupi.
Mantiki ya uwekezaji sawia ktk kilimo ni kuchochea uanzishwaji wa karakana na viwanda vidogo na vya kazi.
Kilimo ni sekta chochezi ktk kuamka ,ubunifu na uanzishwaji viwanda duniani kote..Mapinduzi ya kilimo ndio chimbuko la mapinduzi ya viwanda (Ufaransa, Ujerumani, Urusi, India, China, Marekani n.k)..
Pende mapinduzi ya kilimo kuna matumizi yakinifu ya miundombinu. Hatupaswi kugharamia (Tilioni zote) ujenzi wa miundombinu kama SGR kwa ajili ya Rwanda, Burundi, Congo au Uganda. Focus iwe mapinduzi ya kiuchumi ndani ya nchi yetu. Majirani iwe plus..Kilimo kikubwa Kagera, Mwanza, Kigoma, Shinyanga, Tabora, Dodoma, Simiyu, Morogoro N.K..
Kilimo chenye kulenga kulisha dunia kama ilivyo Ukraine (Kabla ya Vita). Tuweke kusudio la kuwa Ukraine ya Africa.
Uzalishaji mkubwa na wa kisasa.
Sambamba na hili vyuo vya kilimo viongezwe, Mafunzo maalumu ya JKT na mengineo yaweke mkazo na msisitizo ktk kukuza wajasiliamali wa kilimo..
Unaweza,Tunaweza
Pamoja tuijenge Tanzania ya thamani