Rais Samia Gumzo Barani Afrika. Awa Kama chemchemi ya Maji Isiyokauka Midomoni Mwa Watu

Rais Samia Gumzo Barani Afrika. Awa Kama chemchemi ya Maji Isiyokauka Midomoni Mwa Watu

Sijui kateuliwa nafasi gani? Kwani Rais haoni anachofanya huyu bwana? Au anayoyafanya humu ndio ajira yake? Kweli, kuwa chawa lazima uwe hamnazo!
Acha tu ndugu yng,kama nchi bado tuna safari ndefu mno
 
Ndugu zangu Watanzania,

Unaweza kushindana na yeyote yule na ukafanikiwa kushinda vita yako. Lakini kamwe huwezi kushindana na mtu ambaye anapiganiwa,kutetewa na kulindwa na Mungu. Huwezi kushindana na mtu mwenye kibali na aliyeinuliwa na Mungu Mwenyewe. Huwezi kushindana na Mtu aliye na Mungu ndani yake.

Rais Samia ni Mama aliyeinuliwa na Mungu,Mwenye kibali cha Mungu mkononi Mwake na aliye na Mungu ndani yake. Waweza kusema kuwa Mungu amejifunua machoni pa Rais Samia na kumpatia njia na maarifa ya namna ya kuongoza Taifa hili katika namna inayogusa Maisha ya watu na kuwapatia matokeo Chanya yenye Matumaini.

Ni ngumu sana kuzuia hisia za upendo za watu kwa mtu fulani. Kwa sasa bila kuficha wala kupepesa macho kwa hakika Rais Samia amedhihirisha ni anapendwa na watu haijapata kutokea.Mama anakubalika kuwahi tokea kwa kiongozi yeyote yule. Mama ameiteka Mioyo ya watu utafikiri kainasa kwa Sumaku.

Ni Mama Samia katika vyombo vya habari,mitandao ya kijamii na mitaani. Mama anazungumzwa na watu kwa mazuri pasipo kukauka midomoni mwa watu utafikiri kuna chemchemi ya maji ibubushayo Maji yenye mlio wa Jina la Rais Samia midomoni Mwa watu muda Wote.

Rais Samia ndiye amekuwa habari ya mitaani na vilingeni na hata magengeni na kila Sehemu yenye mkusanyiko wa watu. Kinachozungumzwa na watu ni juu ya uchapakazi wake,uthubutu wake, umadhubuti, ushupavu,uimara na uhodari wake kiuongozi anao endelea kuuonyesha.

Amekuwa ndiye shujaa wa Afrika aliyebadilika kuwa habari kuu ya Afrika katika habari zote muhimu za Bara la Afrika. Kila mmoja anatamani Mama huyu angezaliwa katika Nchi yao ili awaongozo.

Watu wanastaajabu namna alivyo mbunifu ,mwenye Maono ,akili kubwa na upeo wa hali ya juu sana. Wanashangaa namna alivyo na mipango mikakati yenye uwezo ya kuliinua Bara la Afrika na kulifanya likajitegemea lenyewe kwa kila kitu pasipo kuhitaji misaada ya Wazungu yenye masharti ya kila aina.

Mama Samia analifungua Bara la Afrika kifikira na kilionyesha kuwa linaweza kutembea kwa miguu yake kwa kutumia utajiri uliojaa katika ardhi ya Bara la Afrika. Kwa hakika Rais Samia ni Mpango wa Mungu Mwenyewe kuja kuliinua Taifa letu na Bara zima la Afrika.View attachment 3216890cz

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili. ,
MM Samia ni shujaa wa kitu gani jamani, kwa ajali Tz ilopata 2021...! 66yr + 5 = 71yrs na nchi iongozwe na mm wa umri huo? Si mnamchosha tu mm wa watu. Nyerere alingatuka akiwa na miaka 63, Kikwete 65, Mkapa 66, Mwnyi 70. Magufuli naye angeondoka na 66yrs by 2025. Kila la kheri mm...
 
Wa kumshangaa ni aliyekuteua kuwa msemaji wa mungu. Hebu tueleze pia ni kwanini huyo mungu aliyempa kibali SSH akaongoza nchi kwa ufanisi unaoushadidia anaangalia tu kinachoendelea huko DRC pasipokuchukua hatua ilhali uwezo (na labda nia) anao.
Kwani Mama yetu Mpendwa ni Rais wa Congo Tangia lini? Au umechangayikiwa?
 
Waziri wa fedha wa Marekani anatumia public transport lakini DC wa Ikungi ana msafara wa magari kumi kwenda kukagua choo cha shule, akili za kipumbavu sn
Ni ujinga wa hali ya juu sana, choo kinachokaguliwa thamani milioni tatu, msafara wake thamani yake ni milioni ishirini! Naye anajiona ana akili timamu kabisa!!!
 
Back
Top Bottom