Rais Samia hakuna kurudi nyuma. Simamia hapo hapo, Hii nchi ukiwasikiliza watu haitaenda

Rais Samia hakuna kurudi nyuma. Simamia hapo hapo, Hii nchi ukiwasikiliza watu haitaenda

Kwanza kabisa nakupongeza kwa ukipofikia. 1. Kwenye chanjo
2. Kwenye Makato ya Kodi

Tanzania ilipokuwa imefikia ilikuwa ni pabaya sana. Watu waliaminishwa ujinga na wakaendelea kuishi kwenye ujinga. Tumepoteza watu wengi sana kutokana na kuaminishwa kuwa Tiba asili inatibu Corona badala ya njia za kisayansi. Mimi Pia nilipoteza rafiki yangu.

1. Kwenye Chanjo
Hapa usibadili msimamo. Aliyepita alidharau huu ugonjwa na kwa Kweli hata yeye mwenyewe ulimwondoa. Umeondoa wasaidizi wake na wananchi wengi Pia. Ni bora umeruhusu chanjo. Watu wachomwe wanaotaka na wasiotaka waachwe corona ideal nao. Mfano wa nchi zilizochukulia serious huu ugonjwa upo na sasa wameweza kuudhibiti na sasa wamerejea kwenye maisha yao na kuepusha vifo na kupoteza nguvu kazi

2. Kwenye Tozo
Hapa wala usirudi nyuma. Aliyepita hakupandisha wafanyakazi madaraja, hakuongeza mishahara. Wewe umepandisha wafanyakazi madaraja jambo lililosababisha mishahara yao kuongezeka. Aliyepita alikusanya kodi kwa nguvu na kukopa sana Hadi akawazidi maraisi wote kwa kukopa. Wewe hutaki kodi ya dhuruma na Pia unataka kupunguza kukopa sana.
Wewe unataka kufanya miradi kwa pesa za ndani kweli na sio kuwahadaa wananchi unafanya miradi kwa pesa za ndani kumbe unakopa sana na kuhatarisha uchumi kwa kuongeza deni la taifa.

Tunahitaji miradi ya kimkakati. Maji yawepo kwa wananchi wote, barabara za lami vijijini na mijini na Pia miradi mikubwa iliyoanza kukamilika.

Kwa malengo haya Mama Samia usirudi Nyuma. Zaidi naomba tu haya pia yafanyike

1. Wabunge nao waanze kutozwa kodi

2. Wale wote wasiotozwa kodi( Hasa kwenye utumishi) nao waanze kutozwa kodi.

Mama Samia, China unayoiona Leo ni kutokana na maamuzi magumu kwenye maendeleo yaliyofanywa na Mao Zedong na Deng Xiaoping.

Ulaya unayoiona Leo kuna kodi kwenye kila kitu na wananchi wanalipa Kweli.

Rais Samia namaliza kwa kukwambia, usife moyo wala usirudi nyuma. Hayo ndo maamuzi magumu.
Unataka Akamue beberu ana maziwa??
Hataacha kupiga kelele na hata ukamueje maziwa hutapata!
 
Hakuna maamuzi muhimu sikuzote kama maamuzi magumu.. Kwenye Tozo arekebishe kidogo na kwenye chanjo hoja yako ina mashiko.. ila ishu za ubadhilifu, ufisadi , rushwa na Katiba Mpya pia azishughulikie maana tunataka kodi zetu zitumike kihalali, sio kunufaisha watu wachache wenye mlengo flani wa kisiasa.. NB: Punguza kisebengo na kiherehere
 
Sukuma peoplr leo wanalala na viatu
 
Mh Samia alikuwa Makamu wa Rais - nisehemu yamaendeleo ya utawala ulee ..unaanzaje kumuona mpya .. Magreat thinker tunakalia akili !?
 
Binafsi napenda ishindikane kabisa ukitumiwa Elfu 10.Unaingalia tu kwenye simu,haitoki na zaidi uinunulie muda wa mongezi.
Mafuta hapo yalipo yaende mpaka 3,000/= hapa tutapata barabara kwa haraka sana.
 
Hujui China wamefanikiwa kuicontrol baada ya kuchanja watu wengi??

hujui Taiwan, Singapore, Israel nao wamefanikiwa baada ya kuchanja watu wao wengi sana??? Sasa hivi wana cases chache sana ambazo zote zinahimilika!
Safi kabisa. China wamechanja watu kibao.....nilipenda chanjo yao pia.
 
Hujui China wamefanikiwa kuicontrol baada ya kuchanja watu wengi??

hujui Taiwan, Singapore, Israel nao wamefanikiwa baada ya kuchanja watu wao wengi sana??? Sasa hivi wana cases chache sana ambazo zote zinahimilika!
Hahaha unawaamini wachina wewe? Seychelles si ndo ilikuwa inaongoza kwa kuchanjwa ulisikia mlipuko uliotokea?
 
Hoja yako ya pili unasema mama hataki mikopo wakati amewaapisha watu na amewahimiza waombe mikopo huko wanakoenda????
 
Hoja yako ya pili unasema mama hataki mikopo wakati amewaapisha watu na amewahimiza waombe mikopo huko wanakoenda????
Wapi alisema mikopo? Alisema misaada inayohusiana na corona
 
Ujuaji umekuwa mwingi mno. Naunga mkono Tozo mpya binafsi sioni hizi tozo zinaathiri vipi hayo maendeleo ya mtu ambayo wajuaji humu wamekuwa wakitukana kila mara. Unajiuliza wanataka tuchukuliwe pesa zetu Benki kwa nguvu au tuongezewe kodi kwenye mapato yetu ili wajue kwamba serikali ipo serious inahitaji pesa
 
Back
Top Bottom