Pre GE2025 Rais Samia: Hakuna Uhuru wa Habari usio mipaka yake

Pre GE2025 Rais Samia: Hakuna Uhuru wa Habari usio mipaka yake

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Nchi yetu sijui kwa nini huwa ina deal na vitu ordinary sana...

Leo hii Mh. Rais akiulizwa kwambaaliyekuwa Waziri wa Ardhi Bw Jerry Slaa kaacha msingi/mfumo gani ambao utaendelea kutumiwa na Wizara ya Ardhi kuepuka migogoro ya ardhi ambayo Waziri alipambana kuitatua, sidhani kama Mh Rais atakuwa na majibu...
 
Mipaka inapatikana kama Mtu kuingia nyumbani kwako kama Mulewa atajuwa hapa mimi sitakiwi kufika na Mingine kama Unaakili timamu utapima wewe mwenyewe
Mipaka inatakiwa ieleweke, siyo inapatikana kama unavyopiga ramli hapa.

Wewe ni mganga wa kienyeji?
 
Hiyo mipaka ni ipi, na nani a ayeamua kuwa kwa habari hii, mpaka wake ni huu?

Vyombo vya habari vikumbushwe kutoandika uwongo. Uwongo kama ule wa kusema kuwa Rais Samia ametoa bilioni kadhaa kwaajili ya hiki na kile, wakati ukweli ni kuwa Samia hajawahi kutoa hata shilingi moja kwaajili ya mradi wowote, sana sana, yeye ni mtumiaji wa kodi za wananchi.
EEEeeeenHEEEeeeee!

Hiyo habari inanikumbusha mambo ya kutumia "lugha ya staha". Utaeleza vipi kwa lugha ya staha matendo ya kijambazi inayofanyiwa nchi?
Jambo lolote wasilotaka kulisikia wao, hata ulembe vipi, hiyo itakuwa lugha itakayo waudhi wao.
 
Rais Samia ameyasema hayo akiwaapisha Mawaziri, amesema kuwa Wizara ya Habari ni muhimu sana katika utekelezaji wa ile falsafa yetu ya R4, uhuru wa habari lazima uendelee kusimamiwa kikamilifu. Hakuna uhuru wa habari usio mipaka yake "Uhuru wa Habari with mipaka ya uhuru huo".

Amemtaka Waziri wa Habari, Jerry Silaa kwenda kushirikiana na wadau wa sekta ya habari, ameongeza kuwa watu wa sekta ni muhimu sana kwa taifa hili.
View attachment 3052850


Pia soma

View: https://m.youtube.com/watch?v=TmbbANwpujQ
 
Uhuru wa kuzungumza ni indicator mojawapo ya Demokrasia, mataifa yote yalioendelea yanatoa uhuru wa watu kuongea ili waweze kuchota maoni ya wananchi , lakini ikumbukwe hakuna uhuru usio na mipaka , kusema / kukosoa ni haki ya kila mwananchi kuzungumza akiona mambo hayaendi sawa.

Lakini kusema huko kusiende mbali kuhatarisha usalama wa Taifa au kuzua taharuki miongoni mwa watu au kukosoa huko kusivuke mipaka ya kutukana kwa lugha isiyofaa ya matusi kudhalilisha mtu , hio sio desturi yetu

Tuwakemee watu wote wanaofanya siasa za fujo / matusi mitandaoni hao ni wahuni kama wahuni wengine

Mungu ibariki Tanzania na serikali yake
 
Ukichunguza sana wanaotukana utakuta wana shida fulani kisaikolojia. Kuanzia makuzi yao na maisha wanayoyapitia.
Afya ya akili inapokua na mushkeli ndio tatizo linaanza.
 
Back
Top Bottom