Pre GE2025 Rais Samia: Hakuna Uhuru wa Habari usio mipaka yake

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Nchi yetu sijui kwa nini huwa ina deal na vitu ordinary sana...

Leo hii Mh. Rais akiulizwa kwambaaliyekuwa Waziri wa Ardhi Bw Jerry Slaa kaacha msingi/mfumo gani ambao utaendelea kutumiwa na Wizara ya Ardhi kuepuka migogoro ya ardhi ambayo Waziri alipambana kuitatua, sidhani kama Mh Rais atakuwa na majibu...
 
Mipaka inapatikana kama Mtu kuingia nyumbani kwako kama Mulewa atajuwa hapa mimi sitakiwi kufika na Mingine kama Unaakili timamu utapima wewe mwenyewe
Mipaka inatakiwa ieleweke, siyo inapatikana kama unavyopiga ramli hapa.

Wewe ni mganga wa kienyeji?
 
EEEeeeenHEEEeeeee!

Hiyo habari inanikumbusha mambo ya kutumia "lugha ya staha". Utaeleza vipi kwa lugha ya staha matendo ya kijambazi inayofanyiwa nchi?
Jambo lolote wasilotaka kulisikia wao, hata ulembe vipi, hiyo itakuwa lugha itakayo waudhi wao.
 

View: https://m.youtube.com/watch?v=TmbbANwpujQ
 
Uhuru wa kuzungumza ni indicator mojawapo ya Demokrasia, mataifa yote yalioendelea yanatoa uhuru wa watu kuongea ili waweze kuchota maoni ya wananchi , lakini ikumbukwe hakuna uhuru usio na mipaka , kusema / kukosoa ni haki ya kila mwananchi kuzungumza akiona mambo hayaendi sawa.

Lakini kusema huko kusiende mbali kuhatarisha usalama wa Taifa au kuzua taharuki miongoni mwa watu au kukosoa huko kusivuke mipaka ya kutukana kwa lugha isiyofaa ya matusi kudhalilisha mtu , hio sio desturi yetu

Tuwakemee watu wote wanaofanya siasa za fujo / matusi mitandaoni hao ni wahuni kama wahuni wengine

Mungu ibariki Tanzania na serikali yake
 
Ukichunguza sana wanaotukana utakuta wana shida fulani kisaikolojia. Kuanzia makuzi yao na maisha wanayoyapitia.
Afya ya akili inapokua na mushkeli ndio tatizo linaanza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…