Rais Samia hapaswi kuitwa Daktari

Dr musukuma
 
#HABARI: Wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM), kutoka Chanika, Buguruni, Tandika na Ukonga, wamevamia ofisi za CCM, Mkoa wa Dar es Salaam kwa madai ya kutaka uchaguzi urudiwe baada ya kutokea fujo na wizi wa kura katika uchaguzi wa ndani uliofanyika hivi karibuni.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.

#Follow RadioOneStereo
 
Wewe ndio unapaswa???
Disgusting.
 

Kama umengalia trend za wana siasa haswa wa CCM hii miaka ya karibuni. Waligundua kuwa Wadanganyika wakisikia wewe ni Daktari basi kura unapata za bure kwa kuhisiwa msomi. Basi hapo wote walienda kununua Phd za ujanja ujanja za kina Msukuma na wengine ndio huo udaktari wa heshima, lakini wanahakikisha kila akienda aandikwe na kuitwa hivyo wanajua kuna wajinga wengi hawatambui lolote.
 
Nchi hii ni ya matapeli makubwa sana! Hata Magu alisoma chuo Gani? Feki! Dk Jafo, unapataje PhD wakati ni mbunge na waziri unapata wapi muda wa kufanya research? Dr yule wa ngawira Singapore nae wa uchumi eti? Tozo Kila Mahali Hana vyanzo vingine vya mapato?
 
Waafrika hasa watanzania Hawa maccm wanapenda misifa sana kichwani ni Mazezeta!
 
Kwenye geti la chuo kikuu Cha Cape Town nchini Africa kusini kuna maandish yasemayo"
"Ukitaka kuangamiza taifa lolote duniani huhitaji kutumia silaha za nyuklia wala mabomu ya atomic. Njia nzuri ya kuangamiza taifa ni kuharibu mfumo wa elimu. "Ruhusu mbumbumbu waonekane wamefaulu na wasonge mbele.

Matokeo yake yatajionesha baada ya muda, "mbumbumbu" hao wakisha hitimu.
Wagonjwa watafia mikononi mwa madaktari, majengo yataanguka mikononi mwa wahandisi, pesa zitapotelea mikononi mwa wachumi, utu utapotea mikononi mwa viongozi wa dini, na haki itapotea mikononi mwa mahakimu.

#Kuchezea Elimu Ni Kuangamiza Taifa. ......✍️
 
Kwa staili hii ya CCM hata msoma mita wa dawasco nae apewe cheo cha Dr, maana Kuna mtu kasoma mita zaidi ya miaka 15
 
Huyu PS anayekaimu sasa nadhani ni kama tutusa fulani!, Press release zote za Zuhura Yunus, huwezi kuona popote akimuandika rais Dr!.
Siku hizi matutusa yamejaa kila kona!, hili tutusa halina hata nusu ya uwezo wa Venus!.
P
Mbon hakaimu tena ameshakuwa mkurugenzi yapata miezi 2 sasa na ni kimya kimya tu mambo yanajiendea sasa sijui ndio miongozo ya kazi.
 
Ni ujinga kupigana na majina yake sababu hata akifutiwa huo udr bado ni samia yule yule anayetuongoza. Yaaani shubiri kwa walamba shubiri na asali kwa walamba asali haibadilishwi kwa kumfutia au kumpachika udr.
Hii kukosa hoja ndugu yangu
 
Reactions: Tsh
Marekani Iko Hivyo Tanzania ndio Kuna ulimbukeni
Ni kama watanzania tupo na inferiority complex flani hivi. Watu tunapenda kujitambulisha/kutambuliwa kwa title za elimu tulizonazo kila sehemu tunapakuwa ili kuonesha usomi wetu bila kujali impact ya hizo title kwenye jamii ilivyo ya chini. Mfano, kila msomi mwenye kaelimu ka usanifu wa majengo, umeme etc au kama hizo PhD za kupewa utasikia wakijita 'engineer' fulani 'Doctor' fulani... Hizi title kubwa kubwa hizi, haziakisi kabisa hali ya maisha na maendeleo ya jamii yetu. Title zinatufanya kuonekana Tanzania ni Taifa la wasomi sana, LAKINI, kwenye uhalisia mambo yetu hayana viwango vinavyoendana na huo usomi wetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…