Rais Samia hapaswi kuitwa Daktari

Rais Samia hapaswi kuitwa Daktari

Dr ukiwa pale mlimani tu lakini ukifika maeneoya mwenge wewe ni mjasiriamali uliochangamka
 
Sio Udaktari Kama Anatibu Watu Kapewa Udaktar Wa Heshimu Unalijua Ila Bado Unalalamika,kuitwa Daktari Kwani Kunazuia Kujengwa Shule?Mimi Naona Kunaipa Credit Nchi.Kulalamika Bila Sababu Za Msingi Ni Uhaini
 
Kuna gia ya angani ilipigwa hapa katikati, shwaaaaaa tukashtukia mtu anaitwa Daktari.

Kutoka form four mpaka kuwa Daktari ni gia kubwa. Hii ni gia ya SCANIA, unapiga mpaka msuli wa kiwiko unavimba.

Utaratibu wa Doctorates ni kwamba, mtu anayetakiwa kuitwa Daktari ni yule tu ambaye aliusomea huo Udaktari darasani (PhD), mfano Dr. Magufuli au Dr. Tulia.

Mtu aliyetunukiwa Udaktari wa heshima hapaswi kabisa kuitwa au kujiita Daktari. Udaktari wake unabaki kuwa wa heshima na sio Udaktari wa Title. Hizi ni kanuni za utoaji wa Doctorates.

Samia hapaswi kuitwa Dr. SAMIA kwa sababu hakusomea Udaktari (PhD). Alitunukiwa tu.

Hili swala lazima litangazwe watu waelewe ili kuepusha matapeli.

Tutakuja kupigishwa gia za mwendokasi mpaka tuombe poo. Dr. Manyaunyau, Dr. Masantula.

Elimu izingatiwe!
Mkuu, ukiangalia wakuu wa mihimili mingine, yaani mahakama na bunge, wote wana sifa hizo za "academic titles". Makamu wake wa urais ana hizo pia. Akiwa kama mwanasiasa na kiongozi wa nchi, ikiwamo nguvu ya uongozi ndani ya mihimili hiyo pia (mhimili uliojichimbia), lazima itafutwe namna yoyote iliyokuwa rafiki ya.kumfanya naye anukie waridi pia, kwa kuwa amezungukwa miuwaridi.
 
Kuna hatari kubwa sana kwako ya kukumbwa na yaliyomkumba Ben Saanane.
Kumbuka; aliyekufa ni Mwendazake peke yake, wale watu wote aliokuwa akiwatumia kwenye missions zake za kuteka watu, kuwekea watu sumu, kutesa watu au hata kuwaua kikatili na kisha kutupa maiti zao zikiwa kwenye viroba, wote bado wapo hai. Na mbaya zaidi sasa hivi wamejitungia Sheria yao ili wasiweze kushitakiwa Mahakani kuhusiana na makosa yao yote ya jinai ambayo watatenda. Be Very Careful my dear, "Noah Nyeusi" hazitakauka nyumbani kwako na kazini kwako.
Ushauri wa bure kabisa aisee
 
Magufuli we ulisoma naye PhD? We bwege kweli, unajua kilichomwua Ben Saanane? Bora Samia anatunukiwa na vyuo vinavyotambulika, tena hadharani bila kificho. Tuambie huyo mfu wako alitunukiwa lini, we ulihudhuria akitunukiwa? Samia ana masters kutoka mojawapo ya chuo kikuu bora duniani "Manchester University" umesikia we bwege? Anayetoa degree yoyote ni chuo baada ya kuona umekamilisha vigezo. Hiyo chuki na wivu havitakuacha salama
Samia ana masters? Hebu lete humu CV zake
 
Hili ni tatizo la upinzani kukosa agenda. Kushika dola labda iwe mwaka 2300 kama hizi ndo agenda mlizo nazo. Wananchi hawawezi kuwa na imani na upinzani unaopoteza muda kuongelea elimu na hadhi ya Rais badala ya kuongelea mambo yanayowagusa kila siku.
Wewe ni mpumbavu sana inamaana kila anaemzungumzia kiongozi wa serikali basi ni mpinzani huna akili timamu
 
Kikwete alikuwa mheshimiwa rais halafu makamu wake dr. Shein. Jamaa wakasema haiwezekani wewe makamu aonekane amefanya assignment, test na tasnifu kushinda bosi, jamaa waka equalize ili ionekane both teams to score YES.
 
Si angeukataa sasa?
Wivu ni kitu kibaya sana! hivi mtu ambaye tayari ana'occupy the highest office on land unadhani udaktari wa heshima unamuongezea chochote katika katika na mambo yake?
 
True, naunga mkono hoja, PhD za Honoria Causa, sio official title ya kuitwa Dr, ila kwenye social gatherings na kwenye events ni sawa kumu address as Dr. na ndio maana kwenye press release za ikulu, huwezi kuona Rais Samia akiandikwa Dr.

Hili niliwahi kushauri Kuongezeka Ph.D za Heshima: Kuna haja TCU watoe ufafanuzi wa matumizi ya title ya Dr. kwa Ph.D za heshima na Ph.D za ukweli?
P
Nimesoma mahali mfano unaitwa Juma Shaban, kama ulipata kwa kusomea utaitwa Dr. Juma Shaban, lakini kama wa heshima utaitwa Juma Shaban (Dr) ili kuwa tofautisha..... hivyo haitakiwi kuanza na Dr kama hujasomea.. I stand to be corrected.
 
Kuna gia ya angani ilipigwa hapa katikati, shwaaaaaa tukashtukia mtu anaitwa Daktari.

Kutoka form four mpaka kuwa Daktari ni gia kubwa. Hii ni gia ya SCANIA, unapiga mpaka msuli wa kiwiko unavimba.

Utaratibu wa Doctorates ni kwamba, mtu anayetakiwa kuitwa Daktari ni yule tu ambaye aliusomea huo Udaktari darasani (PhD), mfano Dr. Magufuli au Dr. Tulia.

Mtu aliyetunukiwa Udaktari wa heshima hapaswi kabisa kuitwa au kujiita Daktari. Udaktari wake unabaki kuwa wa heshima na sio Udaktari wa Title. Hizi ni kanuni za utoaji wa Doctorates.

Samia hapaswi kuitwa Dr. SAMIA kwa sababu hakusomea Udaktari (PhD). Alitunukiwa tu.

Hili swala lazima litangazwe watu waelewe ili kuepusha matapeli.

Tutakuja kupigishwa gia za mwendokasi mpaka tuombe poo. Dr. Manyaunyau, Dr. Masantula.

Elimu izingatiwe!
Mfumo wetu wa elimu uliochezewa ndo umezalisha wasomi walamba viatu.

Waliotoa hiyo PhD award ni wasomi waliosotea haswaa.

Ni Tanzania pekee tuna huo uzuzu wa kujipendekeza kwa marais waliopo madarakani
 
Lissu alishaweka mambo wazi. Wanaotumia hiyo title huenda hawaelewi.
Sio kutokuelewa tuu, bali hata kujipendekeza kumekuwa kwa kiwango cha Tanesco mbovu.
Acha mie nicheke tuu, ona huyu waziri wa Zanzibar anavyotapika!
b7b889d915a3443a9035bf4b55a9abf5_412946506_18407636848057742_887300527410898313_n.jpg


Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom