Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,604
- 22,722
Rais Samia katika ziara zake anazofanya amezoea kusifiwa kila anakopita, hali inayojenga taswira kuwa hapendi kuchalenjiwa au kuulizwa maswali magumu kuhusu utekelezaji wa maendeleo. Katika hali ya kushangaza leo, Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina, amevunja utaratibu huo wa kusifia sifia kwa kuamua kuweka ukweli wazi mbele ya Rais, akieleza kuwa wananchi wa Kisesa bado wanateseka kwa kukosa baadhi ya huduma muhimu. Bila kupepesa macho wala kupindisha, amemwambia Rais moja kwa moja kuwa “Kisesa tunakudai,” na kuongeza kuwa kama kuna maeneo mengine yanayodai kuwa hayana madai, basi pesa zao zielekezwe Kisesa.
Pia soma > Mpina: Rais Samia jimboni Kisesa tunakudai, wanaosema 'hatukudai' fedha zao zihamishiwe Kisesa
Kauli hizo za Mpina zimeonekana kumkera Rais Samia, ambaye mara moja alijibu kwa kuonyesha kutoridhishwa na namna Mbunge huyo anavyoendesha majukumu yake bungeni. Amedai kuwa Mpina ameshindwa kusema mambo hayo bungeni, na kwa hiyo wananchi wake wamekosa uwakilishi bora. Hivyo, Rais amewataka wananchi wa Kisesa kumchagua mbunge mwingine “makini” ambaye ataweza kueleza shida zao bungeni kauli inayodhihirisha kuwa Rais hapokei kwa urahisi ukosoaji wa moja kwa moja kutoka kwa viongozi waliopo madarakani.
Soma zaidi: Rais Samia amchana Mpina: Mbunge wa Kisesa ni kuruka ruka kwamba Kisesa tunakudai, Kisesa iko kama mwanamke aliyesuka Nywele