PreGE2025 Rais Samia hataki Wabunge wa CCM wanaomchalenji? apaniki baada ya Luhaga Mpina kumwambia ''Kisesa tunakudai''

PreGE2025 Rais Samia hataki Wabunge wa CCM wanaomchalenji? apaniki baada ya Luhaga Mpina kumwambia ''Kisesa tunakudai''

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Rais Samia katika ziara zake anazofanya amezoea kusifiwa kila anakopita, hali inayojenga taswira kuwa hapendi kuchalenjiwa au kuulizwa maswali magumu kuhusu utekelezaji wa maendeleo. Katika hali ya kushangaza leo, Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina, amevunja utaratibu huo wa kusifia sifia kwa kuamua kuweka ukweli wazi mbele ya Rais, akieleza kuwa wananchi wa Kisesa bado wanateseka kwa kukosa baadhi ya huduma muhimu. Bila kupepesa macho wala kupindisha, amemwambia Rais moja kwa moja kuwa “Kisesa tunakudai,” na kuongeza kuwa kama kuna maeneo mengine yanayodai kuwa hayana madai, basi pesa zao zielekezwe Kisesa.

Pia soma > Mpina: Rais Samia jimboni Kisesa tunakudai, wanaosema 'hatukudai' fedha zao zihamishiwe Kisesa

Kauli hizo za Mpina zimeonekana kumkera Rais Samia, ambaye mara moja alijibu kwa kuonyesha kutoridhishwa na namna Mbunge huyo anavyoendesha majukumu yake bungeni. Amedai kuwa Mpina ameshindwa kusema mambo hayo bungeni, na kwa hiyo wananchi wake wamekosa uwakilishi bora. Hivyo, Rais amewataka wananchi wa Kisesa kumchagua mbunge mwingine “makini” ambaye ataweza kueleza shida zao bungeni kauli inayodhihirisha kuwa Rais hapokei kwa urahisi ukosoaji wa moja kwa moja kutoka kwa viongozi waliopo madarakani.

Soma zaidi: Rais Samia amchana Mpina: Mbunge wa Kisesa ni kuruka ruka kwamba Kisesa tunakudai, Kisesa iko kama mwanamke aliyesuka Nywele
Navyoona Amejibu kama machawa wa CCM wanavyojibu Maswali ambayo hawana majibu Nadhani angeweza kumtukana angemtukana kwa kumchallenge hadharani Hapendi Kusifiwa Anapenda "KUOGOPWA" ukimuogopa anajua utamsifia Tu ndio sababu anajibu Anavyopenda Kwani Kuna Nani Wakumfanya Nini!!! mpaka siku Citizen wa Tz waamue kwenda Ikulu kuuongea nae sijui itakuwa Lini
 
Naona huyu Mama sasa hivi Kama ana matatizo kwa kupenda Sana kuwaongelea Watu binafsi wanaomkosoa kwa kuwasakama badala ya kuongelea kuhusu suala la Maendeleo ya Nchi.

Akumbuke kwamba yeye ni Rais wa Watu wote, wale wanaomsifia na wale wanaomkosoa, wale wanaompebda na wale wasio mpenda. Kamwe, huwezi kupendwa na Watu wote kabisa katika Jamii, kamwe haiwezekani.

Barrack Obama wakati akiwa madarakani akiwa bado Rais wa Marekani aliwahi kusema kwamba "maendeleo ya kweli ni Matokeo yatokanayo na changamoto za wakosoaji, wala siyo wingi wa Wafuasi."
Matatizo ni yetu sote watanzania kwa kukubali kuongozwa na mtu mjinga.
 
Psychology inadai kiumbe mwanamke hapendi challenges kuanzia akiwa mtoto.Ila,akifika deteriorating stage huwa anakuwa maradufu ambapo jamii kwa tafsiri kengeufu humchukulia kama mpenda maadili na mnyoosha mapito.
 
Hicho ni kibali rasmi kwa Kamati za siasa za jimbo,wilaya na mkoa kumuengua mbunge bora kabisa katika awamu hii ya sita.
Na bahati mbaya sasa hivi hata aende upinzani atashinda lakini hatatangazwa.
Ndiomana watu wanasonga na NO REFORMS NO ELECRION mkuu. Tunahitaji wawakilishi bora wenye guts hata za kumuuliza maswali rais anapotembelea kwenye majimbo yao kama hajatimiza yale aliyowaahidi wakati wa uchaguzi. Tunahitaji viongozi na si watawala
 
Rais Samia katika ziara zake anazofanya amezoea kusifiwa kila anakopita, hali inayojenga taswira kuwa hapendi kuchalenjiwa au kuulizwa maswali magumu kuhusu utekelezaji wa maendeleo. Katika hali ya kushangaza leo, Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina, amevunja utaratibu huo wa kusifia sifia kwa kuamua kuweka ukweli wazi mbele ya Rais, akieleza kuwa wananchi wa Kisesa bado wanateseka kwa kukosa baadhi ya huduma muhimu. Bila kupepesa macho wala kupindisha, amemwambia Rais moja kwa moja kuwa “Kisesa tunakudai,” na kuongeza kuwa kama kuna maeneo mengine yanayodai kuwa hayana madai, basi pesa zao zielekezwe Kisesa.

Pia soma > Mpina: Rais Samia jimboni Kisesa tunakudai, wanaosema 'hatukudai' fedha zao zihamishiwe Kisesa

Kauli hizo za Mpina zimeonekana kumkera Rais Samia, ambaye mara moja alijibu kwa kuonyesha kutoridhishwa na namna Mbunge huyo anavyoendesha majukumu yake bungeni. Amedai kuwa Mpina ameshindwa kusema mambo hayo bungeni, na kwa hiyo wananchi wake wamekosa uwakilishi bora. Hivyo, Rais amewataka wananchi wa Kisesa kumchagua mbunge mwingine “makini” ambaye ataweza kueleza shida zao bungeni kauli inayodhihirisha kuwa Rais hapokei kwa urahisi ukosoaji wa moja kwa moja kutoka kwa viongozi waliopo madarakani.

Soma zaidi: Rais Samia amchana Mpina: Mbunge wa Kisesa ni kuruka ruka kwamba Kisesa tunakudai, Kisesa iko kama mwanamke aliyesuka Nywele

Mm sijamuona Rais hapo Eti ninyi mmemuona ndugu zangu? Tuchague wanaume kusimamia mambo magumu CCM mnatufanyia mambo ya kishenzi sana ndani ya nchi hii,yaani mmeshindwa kumpima Samia kwa miaka aliyoongoza na kujua kwamba kaprove failure,Alafu mseme kuna watanzania wanaihitaji CCM,your not serious at all.
 
Jiwe alikubali kukosolewa? Mwalimu Je?
Mm nashangaa tunazungumzia kukosolewa kwa mpina amemkosoa Samia yy anahitaji maendeleo zaidi ktk Jimbo lake,ambaye hajaelewa ni SAMIA slow learner,mpina Hana kosa ila Samia amembeba Mpina kifuani siku nyingi hasa kwa kusema ukweli bungeni,angalia tu Samia anavyojibu,sio kwa sababu mpina kaongea pale la hasha sio kweli.
 
Ulikiweka kando yakakupita mambooooo......kiwasheeeeee.....🎶
 
Jiwe alikubali kukosolewa? Mwalimu Je?
Hebu eleza ya Mwalimu yalivyokuwa; tutaanzia hapo kulinganisha hao viongozi.

Nikutahadhalishe tu kwamba ni muhimu ujue maana ya "ukosoaji" kabla ya kujifanya wewe ni mjuaji.
 
Back
Top Bottom