PreGE2025 Rais Samia hataki Wabunge wa CCM wanaomchalenji? apaniki baada ya Luhaga Mpina kumwambia ''Kisesa tunakudai''

PreGE2025 Rais Samia hataki Wabunge wa CCM wanaomchalenji? apaniki baada ya Luhaga Mpina kumwambia ''Kisesa tunakudai''

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Nimegundua Mpina anapendwa sana na wapiga kura wake.Maana Rais alipokuwa anamponda hakuna aliyeshangilia.
Na tuwaombe wabaki hivyo hivyo.
Hili ni geni kwa wengi, lakini ingependeza zaidi wakaanza kusambaa na kuondoka kwenye mkutano huo na kumwacha yeye na chawa wake waendelee na ujuha wao.
 
Hicho ni kibali rasmi kwa Kamati za siasa za jimbo,wilaya na mkoa kumuengua mbunge bora kabisa katika awamu hii ya sita.
Na bahati mbaya sasa hivi hata aende upinzani atashinda lakini hatatangazwa.
Huo ndio ubovu na upumbavu wa miundo hiyo ya CCM. Hizo KAMATI za SIASA kuwa kama zinaendeshwa na misukule isiyokuwa na akili vichwani mwao.
 
Na kweli wanamdai kwakua kauza bandari yetu sote.
KAZI ni kipimo cha utu
 
Watu kama Mwashambwa ndo wanapendwa na system wazee wa mapambio kusifu na kuabudu
 
Mama amejiweka kwenye Kona ngumu sana kisiasa. Inabidi atumie majeshi peke yake kushinda.
 
Mimi mpaka Sasa najiuliza kama hataki kusikia na kupokea changamoto za wananchi Sasa anazunguka kufanya nini huko majimboni?
Imagine mbunge anaeleza shida za wananchi halafu Rais anajibu maneno kama Yale ...daah hii nchi aisee tuna safari ndefu sana
Anatafuta kusifiwa tu
 
Hivi ndio mnazalisha wanafiki , unataka watu wote mil 60 wakusifie wewe, Yesu Kristo bwana na mwokozi mwenyewe hasifiwi na watu wote , hata muhammad ibn abd’llah kunawanao m-challenge, wewe nani?
 
Rais Samia katika ziara zake anazofanya amezoea kusifiwa kila anakopita, hali inayojenga taswira kuwa hapendi kuchalenjiwa au kuulizwa maswali magumu kuhusu utekelezaji wa maendeleo. Katika hali ya kushangaza leo, Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina, amevunja utaratibu huo wa kusifia sifia kwa kuamua kuweka ukweli wazi mbele ya Rais, akieleza kuwa wananchi wa Kisesa bado wanateseka kwa kukosa baadhi ya huduma muhimu. Bila kupepesa macho wala kupindisha, amemwambia Rais moja kwa moja kuwa “Kisesa tunakudai,” na kuongeza kuwa kama kuna maeneo mengine yanayodai kuwa hayana madai, basi pesa zao zielekezwe Kisesa.

Pia soma > Mpina: Rais Samia jimboni Kisesa tunakudai, wanaosema 'hatukudai' fedha zao zihamishiwe Kisesa

Kauli hizo za Mpina zimeonekana kumkera Rais Samia, ambaye mara moja alijibu kwa kuonyesha kutoridhishwa na namna Mbunge huyo anavyoendesha majukumu yake bungeni. Amedai kuwa Mpina ameshindwa kusema mambo hayo bungeni, na kwa hiyo wananchi wake wamekosa uwakilishi bora. Hivyo, Rais amewataka wananchi wa Kisesa kumchagua mbunge mwingine “makini” ambaye ataweza kueleza shida zao bungeni kauli inayodhihirisha kuwa Rais hapokei kwa urahisi ukosoaji wa moja kwa moja kutoka kwa viongozi waliopo madarakani.

Soma zaidi: Rais Samia amchana Mpina: Mbunge wa Kisesa ni kuruka ruka kwamba Kisesa tunakudai, Kisesa iko kama mwanamke aliyesuka Nywele

Acha kupaniki sikiliza ukweli, mbele hakuna taarabu kuna uwajibikaji. Samia kama kazi imekushinda jiudhuru unusuru taifa , pia uepushe familia yako majanga baada ya wewe kuanguka.
 
Sasa Utawasikia CCM Oohs Alitakiwa Asimuulize Hadharani Tuna Vikao Vyetu Wakati Ni Unafki Mtupu Kwenye Magenge Yao
Mpina Kapasua Mbarika Hadharani
Kisesa Wanamdai
 
Back
Top Bottom