Na tuwaombe wabaki hivyo hivyo.Nimegundua Mpina anapendwa sana na wapiga kura wake.Maana Rais alipokuwa anamponda hakuna aliyeshangilia.
Huo ndio ubovu na upumbavu wa miundo hiyo ya CCM. Hizo KAMATI za SIASA kuwa kama zinaendeshwa na misukule isiyokuwa na akili vichwani mwao.Hicho ni kibali rasmi kwa Kamati za siasa za jimbo,wilaya na mkoa kumuengua mbunge bora kabisa katika awamu hii ya sita.
Na bahati mbaya sasa hivi hata aende upinzani atashinda lakini hatatangazwa.
Hakuna kunyamazaHaya ^mawe^ tuliyoahidiwa yanazidi kuongea.
Asee!
Anatafuta kusifiwa tuMimi mpaka Sasa najiuliza kama hataki kusikia na kupokea changamoto za wananchi Sasa anazunguka kufanya nini huko majimboni?
Imagine mbunge anaeleza shida za wananchi halafu Rais anajibu maneno kama Yale ...daah hii nchi aisee tuna safari ndefu sana
Mama Kasema ukweliChuki ya wazi kabisa imeonekana
Magu angekuwa kama huyu chizi,Makamba na Nape wasingerudi bungeniJiwe alikubali kukosolewa? Mwalimu Je?
Mtu yeyote dhaifu hapendi kukosolewa, kumbuka mh alipata zero form four!Atapaniki sana mwaka huu,anataka sifa asizokuwa nazo
Merciiiiii Mkuuu..Ukimfunga Lissu anachomoza Gwajima ,ukimpoteza Gwajima anaibuka Mpina
Tena huyu haiti press anakuambia macho kwa machoUkimfunga Lissu anachomoza Gwajima ,ukimpoteza Gwajima anaibuka Mpina
Acha kupaniki sikiliza ukweli, mbele hakuna taarabu kuna uwajibikaji. Samia kama kazi imekushinda jiudhuru unusuru taifa , pia uepushe familia yako majanga baada ya wewe kuanguka.Rais Samia katika ziara zake anazofanya amezoea kusifiwa kila anakopita, hali inayojenga taswira kuwa hapendi kuchalenjiwa au kuulizwa maswali magumu kuhusu utekelezaji wa maendeleo. Katika hali ya kushangaza leo, Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina, amevunja utaratibu huo wa kusifia sifia kwa kuamua kuweka ukweli wazi mbele ya Rais, akieleza kuwa wananchi wa Kisesa bado wanateseka kwa kukosa baadhi ya huduma muhimu. Bila kupepesa macho wala kupindisha, amemwambia Rais moja kwa moja kuwa “Kisesa tunakudai,” na kuongeza kuwa kama kuna maeneo mengine yanayodai kuwa hayana madai, basi pesa zao zielekezwe Kisesa.
Pia soma > Mpina: Rais Samia jimboni Kisesa tunakudai, wanaosema 'hatukudai' fedha zao zihamishiwe Kisesa
Kauli hizo za Mpina zimeonekana kumkera Rais Samia, ambaye mara moja alijibu kwa kuonyesha kutoridhishwa na namna Mbunge huyo anavyoendesha majukumu yake bungeni. Amedai kuwa Mpina ameshindwa kusema mambo hayo bungeni, na kwa hiyo wananchi wake wamekosa uwakilishi bora. Hivyo, Rais amewataka wananchi wa Kisesa kumchagua mbunge mwingine “makini” ambaye ataweza kueleza shida zao bungeni kauli inayodhihirisha kuwa Rais hapokei kwa urahisi ukosoaji wa moja kwa moja kutoka kwa viongozi waliopo madarakani.
Soma zaidi: Rais Samia amchana Mpina: Mbunge wa Kisesa ni kuruka ruka kwamba Kisesa tunakudai, Kisesa iko kama mwanamke aliyesuka Nywele