Bulelaa
JF-Expert Member
- Jun 28, 2024
- 1,342
- 3,247
Watanzania kinachowashinda kuongea hadharani, ni ule uoga wa kufungwa jela miaka kadhaa kama kilichompata kijana Shadrack wa Mbeya.
Wana CCM, nawatahadharisha, ni vyema muwe wakweli, maana hata huko kwenu, mnajivunga kuonyesha mpo pamoja na mama ilihali mko mbali naye kwa hatua milioni.
Tangu nimekuwa kijana na sasa naelekea uzee, sjawahi kusikia manung'uniko ya watu wengi, si wanawake, vijana na hata wazee ingawa wapo wanaomuunga mkono Rais kwenye kada ya kilimo nao si wengi.
Lakini kwa ujumla wake, wananchi wameuchoka kabisa uongozi huu.
Laiti kungelikuwa na kinasa sauti kinachonasa mawimbi ya sauti kutoka pande zote za nchi.
Kuna wakati kwa hali ya ubinadamu, Unaweza kuchomoka ukaziacha ofis ukaenda Oman kula bata, vinginevyo, ukiwa huna huruma, unawasweka ndani wananchi wako karibu asilimia 80.
Narudia tena kwa ushauri, ili kuepuka dhahama ya CCM kudhalilishwa, wekeni mgombea mwingine.
La hamtaki, kitakachowaponya, ni ule ujasiri wenu wa kutojali maisha ya wengine, basi mjipange kisawasawa kuiba kura kwa kuchota na siyo kwa kudonoa donoa.
cc: Tlaatlaah