Nchi yangu TANZANIA imepitia wakati mgumu sana ktk siasa zake, Chama Dola pia kimegawanyika makundi makundi,bt yenye nguvu ni makubwa mawili.
KATIBA mpya ndio njia pekee ya kuondoa mpasuko huo ndani ya CHAMA. In other way naeza Sema CCM wanahitaji Katiba mpya kuliko hata vyama vya upinzani na makundi mengine.
Mwl Nyerere alikuwa na uwezo mkubwa wa kuona ya MBELENI kuliko viongozi wengi waliopo sasa.
Kuingia ktk Uchaguzi mamlaka ya Rais yakiwa pale pale Kwa mlango wa tume kuwa huru, wakati huo huo matokeo ya urais hayahojiwi mahakamani, na Rais hashtakiwi Kwa makosa yoyote aliyofanya akiwa madarakani ni tunajidanganya, yaani tuendelee kuitumbukiza Nchi SHIMONI bila kujali vizazi vijavyo.
Nawasihi Kwa la MUNGU Alie hai, msiwaze vyeo vya kisiasa pekee, Amani muionayo ilitengenezwa, zamani viongozi walichukia RUSHWA Kutoka moyoni, Msisubiri mabaya yatokee ndo mrekebishe, fanyeni sasa NCHI ISIANGAMIE. Amen