Rais Samia, haya mambo ya kupotea watu ni doa kwenye serikali yako

Rais Samia, haya mambo ya kupotea watu ni doa kwenye serikali yako

Acha upumbavu wako! Hata wakati wa kikwete watu walikuwa wanauliwa kama mwanahabari Mwangosi, Dr Mvungi,Mtikila pia alipata ajali ya ajabu ajabu pia Dr Ulimboka alitekwa,mauaji ya waandamanaji Arusha, Jeshi la polisi kuua wauza madini Morogoro na matukio ya ujambazi kila kona ya nchi! Wewempumbavu unakuja kuongea ujinga hapa! Huyo bibiako mbona kila siku misiba ya mauaji? Basi sema anawaua Rais Samia!
Pamoja na hayo yote, Magufuli was a beast!, angeendela kuwepo tungefika point ya "wabaya" wake kuuliwa mbele ya hadhara.....anakutenda kisha anazuia wengine wasi- sympathize nawe.
 
Watu mlisema Magufuli ndio alikua anapoteza watu, Magufuli alishakufa miezi 10 iliyopita lakini bado watu wanapotea, wanauwawa, miili inaokotwa hovyo , sijuo bado Magufuli ndio anawaua kutoka huko kuzimu ama lah.
Mauaji ya kutisha sasa ni nchi nzima...
Screenshot_20220122-001834.jpg
 
Watu mlisema Magufuli ndio alikua anapoteza watu, Magufuli alishakufa miezi 10 iliyopita lakini bado watu wanapotea, wanauwawa, miili inaokotwa hovyo , sijuo bado Magufuli ndio anawaua kutoka huko kuzimu ama lah.
Magufuli hayupo lakini wale watekelezaji wa mauaji bado wapo kwenye mifumo, serikali inapaswa kufanya uchunguzi huru dhidi ya huu upotevu na uuaji, wahusika wachukuliwe hatua kali
 
Chadema wapo kimya siku hizi kuhusu mauaji maana wao waliusika kutengeneza uongo wa kumsingizia JPM ,kikundi cha mafisadi wa mzee wa msoga ndiyo kilichokuwa kinausika na hayo mambo ya kuua kwa kuchafua serikali ya awamu ya 5 ndani yake kuna wafanya biashara mafisadi papa ,wauza ngada ,washirikina nguli, na kila aina ya WAHUNI
 
Ulipoingizia tu"unajifanya muislam safi nikajua tu huyu mnafki
 
Mheshimiwa Rais, naomba nichukue nafasi hii nikupongeze kwa mambo mengi mazuri unayoyafanya ila kwa hili la watu kuanza kupotea kwenye utawala wako tayari ni doa kwenye serikali yako. Wiki mbili zilizopita kuna habari zimetokea magazeti kuwa kuna vijana watano wamepotea wakiwa wanaenda kusherekea Krismasi kwenye fukwe hapa Dar es Salaam.

Kwa maelezo yao ni kuwa walikamatwa na Police na wakawa wanapelekwa central police, baada ya hapo hawakusikika tena hadi leo wiki ya tatu licha ya jitihada za kuwatafuta kwenye vituo vya police zote za Dar, kwenye mahospitali na mortuaries zote. Hii style tuliona wakati wa utawala wa awamu ya tano ya Magufuli na wewe ukiwa makamo wa rais, tumeona yaliyompata Azory Gwanda, Ben Saanane, Roma Mkatoliki na wengine wengi waliokuwa wakiokotwa kwenye magunia na viroba.

Mheshimiwa Samia, nikuulize swali moja. Je, bado unayaendeleza yale yale ya kupoteza watu na kuwatupa mtoni? Mbona wewe unajifanya muislamu safi? Je, dini yako inaruhusu uue na kupoteza watu?

Au unashindwa kuwakemea huyo Sirro na polisi wake? Haya ndiyo yale mambo yaliyofanyika miaka iliyopita ya akina Abdallah Zombe na wenzake walivyowauwa vijana wasio na makosa wafanyabiashara wa madini na kuwaibia pesa zao? Haya ndiyo yale yale ya kuwaua vijana wapatao 7 Arusha waliokamatwa na polisi kwa kushukiwa kuwa wanapanga kuvizia na kuiba kwenya gari la benki lililokuwa likipeleka pesa Kiteto?

Inasikitisha kuona wananchi wanatoka majumbani mwao lakini hawarudi. HATA KAMA NI WASHUKIWA NA WAMEKAMATWA, KUNA TARATIBU ZAKE ZA KUPELEKWA MAHAKAMA NA FAMILIA ZAO KUFAHAMISHWA. Wewe mheshimiwa Rais Samia kwenye hotuba moja ulisema ulikamatwa kwa kosa la taa ya gari kutokuwaka. Je, ungewekwa mahabusu au kuumizwa, je familia yako ingefanyaje? Haingekuwa simanzi? Usifurahie mkuki kwa nguruwe ila kwa binadamu uchungu!

Hivi rais Samia unaona raha gani raia wako wakipotezwa au wakiuawa? Kweli una roho ngumu kiasi hiki kama Adolf Hitler! Onea huruma raia wako. Usifurahie unayoyaona, kama unafurahia ujue kuna KARMA.

HADI LINI WATU WATAENDELEA KUPOTEA?
Ujinga ni kuamini kila mtu anayepotea eti ni serikali inahusika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kitu kimoja tu Ambacho nina uhakika nacho LEGACY ALIYOIACHA MAGUFULI hakuna rais anaweza fika hata nusu yake...!!! Alivyothamini watu wenye vipato vya hali ya chini ilikuwa namna ya kipekee sana.. Leo tunakatwa buku buku kila kona na bado mtu akiongelea kuhusu Kukopa anaonekana ni Adui.. Safari ni ndefu sana bado yani tutafika hoiii
kwahiyo matajiri siyo watu?
 
Nilidhani Magufuli amefufuka maana mlidai ndo alikuwa mtekaji na muuaji
Watu mlisema Magufuli ndio alikua anapoteza watu, Magufuli alishakufa miezi 10 iliyopita lakini bado watu wanapotea, wanauwawa, miili inaokotwa hovyo , sijuo bado Magufuli ndio anawaua kutoka huko kuzimu ama lah.
Si mlisema ni Magufuli ndio anaua na kuteka watu?
Kuna wapumbavu humu walikuwa wanadai alikuwa anaya watu! Vipi kashafufuka? Maana kila kona ya nchi watu wanauana na sasa wameanza kupotea! Yaani kuna watu wajinga sana kazi kushabikia kisaunachuki na mtu!
Mambo vipi jamaa zangu, wafuasi wa hayati Mzilankende!
 
Unavosema extreme, utadhani una evidences zote, kumbe ni mboyoyo tu na hearsays. Woi
List ya wahanga wa Magufuli ipo na itawatesa sana walinda legacy (sukuma gang).

Yeye mwenyewe alitangaza hadharani kuwa angewapoteza robo ya wajumbe wa NEC walioimba wana imani na Lowasa.

Yeye kwa mdomo wake alitoa amri kwa vyombo vya usalama kumuua mpinzani wa kisiasa Mh. Tundu Lissu.

Kupitia wanajeshi wa JWTZ alipora korosho za wakulima mikoa ya kusini.

Kupitia lile kundi aliloliasisi la utekaji, waliteka, kuua na kupora mali za watu, kuanzia kuchukua fedha kwenye akaunti bila maelezo, kubambikia kodi, n.k.

Mtu maarufu kabisa aliyetekwa na kunusurika kuuliwa alikuwa Mo. Sote tunajua.
 
Jiangalie dogo utapigwa para soon! Naona unakosa adabu

Huyo mnae bishana nae ndio picha halisi ya wanao mtukana magu kila siku humu then pima akilizao ndio utajua niwatu wa namna gani.

Niwalopokaji tu na wanafaa kupuuzwa.
 
Kikwete hajawahi kuua mtu.
Wewe kweli ni kichaa hivi mauaji ya aldino na kipindupindu ,na kufukiwa kwa wachimbaji wadogo wa madini ,na kijiji kumwakiwa tindikali za sumu ili beberu achukue ardhi yao hayo yote wewe ulikuwa wapi ? Labda ujui kwanini wakati wa magufuli ujambazi ulipungua kwa 90% na mauaji ya aldino yakakoma
 
Back
Top Bottom