Rais Samia, hili la wagonjwa kulipa wakati wa matibabu litasababisha vifo vingi

Rais Samia, hili la wagonjwa kulipa wakati wa matibabu litasababisha vifo vingi

JF Member

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2014
Posts
7,914
Reaction score
10,793
Rais Samia ameshauri uwepo mpango mzuri ili kutozuia maiti kwenda kuzikwa.

Ameenda mbali na kushauri kwamba wagojwa walipe gharama wakati wa matibabu ili kupunguza mzigo akifariki.

Naomba nimshauri Rais wetu:
1. Wagonjwa watibiwe tu ili wapone. Ukiaamrishwa walipe wakati wakitibiwa kutawafanya wafe wengi maana pesa ya kulipa papo kwa papo haipo.

2. Mtu akifa mara nyingi ndugu hushirikiana kwa pamoja kulipa gharama zote, na ndio maana malalamiko ya kuchukua miili ni machache. Chonde chonde Matibabu yafanyike bila kuangalia ghalama za badae.

3. Serikali ilete BIMA kwa watu wote.

Karibuni kwa ushauri.
 
Tuwekeane mkataba wa mgonjwa na hospitali kwamba ugonjwa huo unauweza au hapana! Siwezi kutibiwa mwezi mzima bila mafanikio, halafu nikielekea kufa naletewa bili. Sikwenda hospitali kutalii!
 
Hiyo kauli katoa Rais Samia huyu huyu wa TZ, ama Rais Samia wa wapi? Maana haifananii kutolewa na Rais wa Tz.
 
Rais Samia ameshauri uwepo mpango mzuri ili kutozuia maiti kwenaa kuzikwa.

Ameenda mbali na kushauri kwamba wangojwa walipe ghalama wakati wa matibabu ili kupunguza mzigo akifariki...
Tupe chanzo tufuatilie habari hiyo wenyewe,usitulishe maneno.
 
Hiyo kauli katoa Rais Samia huyu huyu wa TZ, ama Rais Samia wa wapi? Maana haifananii kutolewa na Rais wa Tz.
Wasipo tuletea chanzo halisi cha taarifa yao,nitaendelea kuwaita wakwamia awamu yao ama wanachama wa gang yao.
 
.
Screenshot_20210608-160627.jpg
 
Huyu mama ni kituko naona anataka kuifanya Jamhuri ya Tanzania Nchi ya kiislamu, tutegemee maboko zaidi kutoka kwake.
 
Huyu mama ni kituko naona anataka kuifanya Jamhuri ya Tanzania Nchi ya kiislamu, tutegemee maboko zaidi kutoka kwake.
We lofa usimuingize huyo mama yenu ktk uislamu,
Unaijua jamhuri ya kiislamu wewee au unapayuka tu kama kiranja wa mirembe
 
Ila sisi tuna shida sana....

Ukienda hospital ukakosa huduma dawa na vifaa tiba hakuna tunalalamika.

Haya vipo hivo hivo, umeenda umepata huduma zote na dawa umetumia bahati mbaya ukivuta ndugu walalamike, sasa usipolipa bill hospitali zinajiendeshaje?

Tukate bima za afya, kwa uwezo wa chini sana kuna msamaha taratibu zifuatwe watu waombe (msahama) kupunguziwa gharama za matibabu. Usingoje mambo yawe mengi maiti izuiliwe....
Na mama kishaliweka sawa bill zitolewe mapema.

Poleni kwa wote waliopatwa na hiyo shida.
 
Back
Top Bottom