Rais Samia, hili la wagonjwa kulipa wakati wa matibabu litasababisha vifo vingi

Rais Samia, hili la wagonjwa kulipa wakati wa matibabu litasababisha vifo vingi

Bila shaka Rais anayo nia njema...,

Lakini anazungumzia jambo ambalo ni 'complex' sana.

Itasaidia kitu gani kujuwa gharama za matibabu siku baada ya siku kwa hali ya kipato cha wananchi kilivyo sasa.

Mgonjwa kaletwa mahututi, wahudumu wamefanya kila liwezekanalo kumhudumia, kafariki siku hiyo hiyo..., hawa wahudumu mara moja wawe wametoa gharama zote zilizotumika siku hiyo hiyo ili maiti akazikwe?

Katika jambo hili hakuna jibu rahisi. Serikali inabidi ikae chini na kuangalia njia bora inayoweza kuwasaidia wananchi. Kwa vyovyote uhusika wa serikali hauwezi kuepukika kwenye maswala haya yanayohusu jumuia.
 
Hujamuelewa Rais alichomaanisha

Ni kwamba bill zitolewe mapema na isisubiliwe hadi mgonjwa afe!
Kwa maana nyingine ukiona bili unajua jamaa wameshafahamu nakufa.
Tumushauri rais kwamba hata ukiwa rais, siyo kila jambo unalifahamu. Kama ataendelea na mtindo huu, hana tofauti na mtangulizi wake. Urais siyo kujua saaana!
 
Wengi wamekufa Sana kwa utaratibu huu.Ugonjwa haupigi hodi.
Utaratibu huu mbovu uliletwa na mwendazake pasipo kujali hali ya wanyonge.
 
Back
Top Bottom