Bila shaka Rais anayo nia njema...,
Lakini anazungumzia jambo ambalo ni 'complex' sana.
Itasaidia kitu gani kujuwa gharama za matibabu siku baada ya siku kwa hali ya kipato cha wananchi kilivyo sasa.
Mgonjwa kaletwa mahututi, wahudumu wamefanya kila liwezekanalo kumhudumia, kafariki siku hiyo hiyo..., hawa wahudumu mara moja wawe wametoa gharama zote zilizotumika siku hiyo hiyo ili maiti akazikwe?
Katika jambo hili hakuna jibu rahisi. Serikali inabidi ikae chini na kuangalia njia bora inayoweza kuwasaidia wananchi. Kwa vyovyote uhusika wa serikali hauwezi kuepukika kwenye maswala haya yanayohusu jumuia.