Rais Samia, hili la wamachinga litawapa umaarufu wanasiasa waliopoteza mvuto. Watasema "umepiga mchache"

Ndugu yangu hili gazeti lilichukuliwa hatua za kisheria kwa ajili ya huo upotoshaji. Na wenyewe waliomba radhi. Sasa unavyolisambaza ujue unafanya kosa.
Hamza ni CHADEMA, eti ehh.
Je mwenezi wa CCM alisemaje kwenye waraka wake? Je hakumtambua Hamza kwamba aliichangia CCM 200 mil? Je hakusema kwamba ni mwanachama mtiifu?
 
Katika mambo Rais SSH amefanya ya maana ni hili la kuondoa Machinga maeneo yasiyo rasmi miji imekuwa misafi na barabara zinapitika yaani tulikuwa kama wanyama, watu tusio na utaratibu wala usafi...Mungu kamuumba binadamu kamtofautisha na wanyama kwa sababu Binadamu ana utashi utashi wa kibinaadamu ulipoteana pale tuliporuhusu machinga waweke biashara zao popote; duniani kote hakuna serikali isiyofuata utaratibu...

By the way kwenye siasa hata machinga msipopiga kura Rais SSH ndiye rais wenu hadi 2030 hilo mkae mkilijua na mkae kwa kutulia tulii huko mlikohamishiwa. Hongera nyingi pia zimwendee Amosi Makalla kwa kusimamia vilivyo agizo la Rais sasa hivi Dar es salaam inapendeza.
 
Kwa hiyo wakisema anautwanga mchache utajifungia ndani uanze kujiliza?Akili zako kama tikiti-maji.
 
Kwanza kabisa naunga mkono mia kwa mia kuwaondowa wamachinga holela, maana wamachinga wa kweli wapo kama pale machinga complex kwa mfano tu.

Pili kwa sasa ccm haina shida ya kupigiwa kura na mtu ina mifumo yake dola ya kukaa madarakani kwa kipindi kirefu kijacho.

Hakuna hata mwenyekiti wa mtaa yeyote aliyechaguliwa na wananchi, hata serikali iliyopo haitokani na wananchi, kwahiyo mtulie tunyolewe wote.

Uzuri huu mchezo wala hautaki hasira, sasa kila nafsi itaonja radha na utamu wa ccm.

Tumpe ushirikiano mama anaupiga mwingi sana.
 
Si kweli hata kidogo. Mama anatakiwa arekebishe, kitu ambacho tayari kilichokosewa. Wamachinga ni watanzania na wanapaswa kusaidiwa kwa kuweka mazingira mazuri ili wapate kipato. Kuruhusu wafanye biashara kila sehemu ni mtaji wa wanasiasa waongo, wasio na maono mazuri kwa nchi yetu.
 
Hakuna chochote kibaya kitakachotokea kwa kuhamishwa machinga,ni uamuzi mzuri nacwao baadae wataufurahia sana

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…