Rais Samia hongera kwa kurekebisha makosa yaliyofanyika kwenye uteuzi wa Azza Hilal Hamad

Rais Samia hongera kwa kurekebisha makosa yaliyofanyika kwenye uteuzi wa Azza Hilal Hamad

Tunataka kujiaminisha zaidi kuwa makosa ni ya wapeleka majina peke yao, lakini anaeteuwa pia anatakiwa kuyapitia kwa kina kama kweli tunamlipa mshahara wa kodi zetu kwa kazi hizo...haya ni majina, vipi kuhusu vitu vingine ambavyo vyaweza hatarisha maisha ya watanzania,aweza pelekewa na hao tunaosema wanamhujumu,kwa kuwa havipitii kwa kina,atasaini tu ikaja kuleta shida alafu tuseme anahujumiwa
Yego mwamba!
 
Mkuu umeliona hilo!! laiti kama mama hangekuwa na mauzoefu ya kazi za kiofisi jamaa angekuwa RS. Kwa mapungufu haya 3 ningekuwa ndio mimi, huyo msaidizi wangu wa masuala ya documention ningemtumbua.
Siyo kumtumbua tu pia kumchukulia hatua kali.
Unaanzaje kumdanganya rais wa nchi na kuendelea kudunda mtaani?
 
Wanateuliwa kwahiyo kabla ya kula kiapo , mama ana nafasi ya kurekebisha pale panapoonekana panahitaji marekebisho!! Mama ni msikivu na hupokea ushauri kutoka kwa wananchi anaowaongoza!
 
vyombo vinavyo msaidia Mhe.Rais vinapaswa viongeze umakini.
Mbona kuna kiongozi alituaminisha kuwa wateuliwa huwa wanapitia kwenye machujio matatu? au inakuaje ?
 
Kama amerebisha ni sawa, lakini mimi binafsi nisingeona elimu yake kama ndio tatizo. Tanzania hii kwenye uongozi sijaona tofauti kati ya mwenye certificate, diploma, degree moja, degree 2, PhD wala Processor kwenye umahiri wa kutatua kero za watu.

Kuna watu ni maprofesa lakini mambo hayaendi na kuna watu Wa darasa LA saba lakni mambo ya wananchi na mambo yao yanakwenda. Rais anaweza kuzunguukwa na maprofessor waoga kutoa ushauri mzuri kwa rais wakihofia matumbo yao. Kuna wasomi wezi na wavivu.

Akili huwa tunazaliwa Nazo hizi za kusoma ni nyongeza tu, wanaotahili watoto huko vjijini ni mangaliba tu, wazee ambao hana elimu wamesomesha watoto wao hadi vyuo vikuu lakini wazazi wasomi kabisa ambao watoto wao wanavuta bangi, madawa ya kulenya na kushindwa kusoma.

Huko mataifa ya kiarabu hakuna PhD nyingi lakini maisha yao yanasonga.

Wakati huu Wa kurekebisha makofu ya ukabila, ukanda, udini, na jinsia kwenye nafasi tusiangalie saaaana kigezo cha degree kwenye ajira za uongozi, vigezo vya elimu vibaki zaidi kwenye taasisi za elimu, vyuo vyetu.

Kwani RAS anafanya Kazi gani kubwa mno inayohitaji kuwa na PhD? Kusema kijiji kile hakina maji twende tukawachimbie bwana kunahitaji elimu gani. Kazi yake si kuratibu watalaamu kama wahandisi, wahasibu na wenyengine wate kwenye mkoa watende kwa mujibu Wa taaluma na viapo vyao?
 
alikuwepo mtanzania mmoja (sasa ni hayati) yeye aliwahi sema alikuwa analala na mafaili kitandani,akiamka anayapitia kwa kina...labda tumshauri huyu Rais wetu nae ajenge utaratibu wa kusoma kwa kina( umesema watanzania hatupendi kusoma) labda na yeye yumo kwenye kundi letu la kutosoma vitu
Hiyo tabia ya kulala na mafaili sidhani kama ilitusaidia, labda ilimsaidia aliyekuwa nayo!
 
Nenda kwenye mawizara, serikalini wasomi wenye Degree, Masters na PhD wamejaa tele wala huhitaji kuwasha tochi, fomu four anatoboa vipi kwenye nafasi ya RAS, yaani mtu mwenye qualifications za kufanya usafi maliwatoni anakuwa RAS, are we serious? mnataka kuua kabisa hii nchi..
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Moja kwa moja nimpe mama Samia hongera kwa kurekebisha makosa yaliyofanyika kwenye teuzi za makatibu tawala na zile za wakurugenzi wa mashirika mfano ile teuzi ya DG wa TPDC.

Ni wazi Kuna majina mama anayopewa ya teuzi yakiwa na makosa. Ieleweke mama Samia hawezi kuwajua watu wote hivyo ni wazi lazima wengine awe hajui historia zao. Juzi aliteua makatibu tawala na kwa bahati mbaya kulikuwa na jina la Azza Hilal Hamad ambae aliteuliwa kuwa katibu tawala mkoa wa simiyu.

Hapa kulikuwa na tatizo kwa kuwa elimu ya huyu Azza ni ndogo na isingekuwa vyema kwenda kuwa katibu tawala. Katibu Tawala mkoa ndio mtendaji, anahitaji mwenye elimu ni Bora ingekuwa nafasi ya mkuu wa mkoa au wilaya maana hizo hazihitaji Sana wasomi.

Mama Samia pia angalia kwa jicho la pili aina ya majina unayoletewa maana hii ikiendelea utawapa nafasi wapinzani wako wapate upenyo wa kukutukana Sana.

Nakupongeza sana kwa kurekebisha haya makosa mapema sana, maana wengeenda huko kazini ingekuwa ni kituko. Pia Kama Kuna wengine uliletewa majina na hawapo vizuri watengue tu, ni Bora lawama kuliko fedheha.

Kwa watu kama hawa ambao makosa ya kibinadamu yanafanyika kwenye teuzi zao na hatimaye kutenguliwa, nashauri kama raia wa JMT, baada ya kutenguliwa teuzi zao, wawe wanapozwa kwa kutafutiwa nafasi nyingine mbadala inayoendana na kiwango cha elimu yao, iwapo tu kutenguliwa huko kunakuwa hakujatokana na sababu zingine zaidi nje ya eimu yao; ili kukwepa kuya-frustrate maisha yao yaliyoko mbele yao, na familia zao
 
Nafikiri mama hatataka kuingizwa chaka kwenye hizi nafasi za kiutendaji ndo maana anabadirisha haraka sana akigundua jambo haliko sawa, na hata kwenye nafasi za kisiasa bado atataka kuwa na watu competent....kwa hiyo wachomekaji wasifikiri watafanikiwa na inaweza kuwagharimu wao wenyewe.
 
Moja kwa moja nimpe mama Samia hongera kwa kurekebisha makosa yaliyofanyika kwenye teuzi za makatibu tawala na zile za wakurugenzi wa mashirika mfano ile teuzi ya DG wa TPDC.

Ni wazi Kuna majina mama anayopewa ya teuzi yakiwa na makosa. Ieleweke mama Samia hawezi kuwajua watu wote hivyo ni wazi lazima wengine awe hajui historia zao. Juzi aliteua makatibu tawala na kwa bahati mbaya kulikuwa na jina la Azza Hilal Hamad ambae aliteuliwa kuwa katibu tawala mkoa wa simiyu.

Hapa kulikuwa na tatizo kwa kuwa elimu ya huyu Azza ni ndogo na isingekuwa vyema kwenda kuwa katibu tawala. Katibu Tawala mkoa ndio mtendaji, anahitaji mwenye elimu ni Bora ingekuwa nafasi ya mkuu wa mkoa au wilaya maana hizo hazihitaji Sana wasomi.

Mama Samia pia angalia kwa jicho la pili aina ya majina unayoletewa maana hii ikiendelea utawapa nafasi wapinzani wako wapate upenyo wa kukutukana Sana.

Nakupongeza sana kwa kurekebisha haya makosa mapema sana, maana wengeenda huko kazini ingekuwa ni kituko. Pia Kama Kuna wengine uliletewa majina na hawapo vizuri watengue tu, ni Bora lawama kuliko fedheha.

Nacheka kwa dharau! Aha! Aha! Ahaa!​
 
Hiyo tabia ya kulala na mafaili sidhani kama ilitusaidia, labda ilimsaidia aliyekuwa nayo!
Unalala Na mafaili we we ni kichaa? Ubongo wenye afya ni ule unaopata muda wa kutosha wa kupunzika.
 
Back
Top Bottom