Kusaini nyaraka bila kuzisoma ni tabia ya watanzania wengi, sio wa serikalini tu. Mifano:
- ule wosia maarufu wa tajiri hayati Reginald Mengi, wale waliousaini kama mashahidi walikiri baadaye mahakamani kuwa hawakuwa wameusoma. Na ndio waliochangia kumwangusha Klynn wao kwenye kesi ya mirathi
- Uliza watu waliochukua mikopo benki kama huwa wanasoma chochote kwenye ile mikataba zaidi ya kiasi cha pesa wanayokopa. Baadaye madalali wakija kuuza nyumba zao ndio wanaanza kuzunguka kutafuta mawakili
- Wewe mwenyewe hizo Apps na mambo mengine unayojiunga ya mitandaoni, ni mara ngapi umesoma ile mikataba mirefu unayowekewa? Mara nyingi kama sio zote unatafuta tu kile kitufe cha ACCEPT unabofya maisha yanaendelea.
Ni desturi yetu watanzania. Labda tuanze leo kujirekebisha