Rais Samia hongera kwa kurekebisha makosa yaliyofanyika kwenye uteuzi wa Azza Hilal Hamad

Rais Samia hongera kwa kurekebisha makosa yaliyofanyika kwenye uteuzi wa Azza Hilal Hamad

Hao wanao mshauri rais wameonyesha udhaifu mkubwa na kumufanya rais aonekane siyo makini.

Hivyi si kuna sifa zimeanishwa kwa kila nafasi inayo tangazwa? Kama ni hivyo ni nani anamletea hao watu wasio na sifa?.Huyo anza naye.
Kabla ya uteuzi si wateule wote hufanyiwa vetting ya kutosha? Au wanaokwotwa tu?

Inasikitisha sana kosa lilianziwa kwa yule wa TPDC, akaja Kafulila, imekuja tena hili la katibu tawala.

Tumeona mpaka waraka toka Ikulu unatolewa umekosewa tarehe.

Watu wa Ikulu na wengine mnao husika msimvunjie heshima rais wetu.
Mkuu Kafulila naye kulikuwa na tatizo? Tatizo gani?
 
Umeandika kombora kubwa mkuu, nadhani akiiona hii komenti yako, hatakosea tena
Wewe naye unaunga unga mkono hoja bila kufikiri. Kateuwa watu 26 kuwa Ma-RAS. kati ya hao 1 tu ndiye kaonekana hastahili.

So, since our denominator in 1/26 is 26, we could adjust the fraction to make the denominator 100. To do that, we divide 100 by the denominator:

100 ÷ 26 = 3.8461538461538

Once we have that, we can multiple both the numerator and denominator by this multiple:

1 x 3.846153846153826 x 3.8461538461538 = 3.8461538461538100
Now we can see that our fraction is 3.8461538461538/100, which means that 1/26 as a percentage is 3.8462%.

3.8462% inakubalika na kuvumilika
 
Hata kama anapelekewa inaonekana kuna mapungufu kwa wanaopeleka haya majina. Haiwezekani ishu ndogo kama hii kuhusiana na elimu ya mtu isiweze kung'amuliwa ama kujilikana maana ni eneo muhimu sana katika kufanya uteuzi.
Inawezekana kuna mambo ya uchomekeaji katika michakato maana yanajirudia. Kama kuna watu wanamkwamisha no bora aachane nao kwani inatia doa kwenye upande wa umakini.
 
Umeandika kombora kubwa mkuu, nadhani akiiona hii komenti yako, hatakosea tena
Katibu wa Rais nakuomba sana uwe serious na wajibu wako, wewe ndio mtu wa mwisho kukagua hizi document sasa haya madudu huyaoni kweli, haya na kazi iendelee
 
aisee huyu alikuwa anachomekwa kijinga. hana qualification zozote zile. mtu kaishia secondary awe katib tawalam what the hell?

umakin unahitajika hapa
Mkuu umeliona hilo!! laiti kama mama hangekuwa na mauzoefu ya kazi za kiofisi jamaa angekuwa RS. Kwa mapungufu haya 3 ningekuwa ndio mimi, huyo msaidizi wangu wa masuala ya documention ningemtumbua.
 
Dah kwa wasifu/cv alioweka mdau hapo juu hastahili kabisa nafasi ya katibu tawala wa mkoa.
Aendelee kubaki hukohuko ambako inatakiwa ujue kusoma na kuandika tu.
 
vyombo vinavyo msaidia Mhe.Rais vinapaswa viongeze umakini.
Mbona kuna kiongozi alituaminisha kuwa wateuliwa huwa wanapitia kwenye machujio matatu? au inakuaje ?
Kwa Viongozi pia wana machujio haya;

Viongozi vipofu, wenye kuchuja mbu na kumeza ngamia.
Mathayo 23:24
Wana screen vitu vya kijinga vidogo vidogo kama mama lishe asiuze karibu na barabara au boda kutovaa helmet, lkn wanaacha watu wanapiga hela mamia ya mils kwa siku, wanajilipa kazi hewa halafu wanasema iundwe tume wasimame kwa uchunguzi, jambo ambalo unaligundua kwa dk 5 tu ukimuuliza mhusika halafu wanampeleka mahakamani.
Shame on Us
 
Hao wanao mshauri rais wameonyesha udhaifu mkubwa na kumufanya rais aonekane siyo makini.

Hivyi si kuna sifa zimeanishwa kwa kila nafasi inayo tangazwa? Kama ni hivyo ni nani anamletea hao watu wasio na sifa?.Huyo anza naye.
Kabla ya uteuzi si wateule wote hufanyiwa vetting ya kutosha? Au wanaokwotwa tu?

Inasikitisha sana kosa lilianziwa kwa yule wa TPDC, akaja Kafulila, imekuja tena hili la katibu tawala.

Tumeona mpaka waraka toka Ikulu unatolewa umekosewa tarehe.

Watu wa Ikulu na wengine mnao husika msimvunjie heshima rais wetu.
Inasikitisha kosa la tatu hili looks like watu wananmchomekea mama as wanajua hasomi.
Too sad.
Sipati pich akianza kupangua DED na DC wale wako wengi si tutakesha kurekebisha
 
Nchi ngumu sana hii ndugu yangu.
Hakika kiongozi na tusipofanya marekebisho ya mambo (ikiwemo kupata katiba mpya) tunasafari ndefu sana.
Fikiria leo hii mtu darasa la saba (mjengoni kwa Ndugai) anadiriki kuuaminisha umma eti yeye ni bora kuliko Degree/Masters/PhD holders.
 
Hii ndo tabia ya kusaini mkataba kabla ya kuusoma na kuuelewa.

Rais hapaswi kukosea kirejareja namna hiyo. Ni vyema kukaa chini na kujiridhisha juu ya hizo vetting maana wengine ndo hupata mwanya wa kupitishia michepuko na ndugu zao.
Hata ule mkataba wa bomba sijui Kama ameusoma na kuuelewa usikute kasaini tu

Ndio Yale twaja pata 5% wakati 85%ya ardhi yetu imetumika katika Hilo bomba
 
Rais wetu ana mapungufu yakutopenda kusoma hasa vitu vya msingi kwake
 
Magufuli alipoambiwa kuhusu Elimu ya Bashite alizidi kumtukuza, huyu Mama ni Msikivu sijui aliwezaje kufanya kazi na Magufuli

Sent from my vivo 1915 using JamiiForums mobile app
 
Kusaini nyaraka bila kuzisoma ni tabia ya watanzania wengi, sio wa serikalini tu. Mifano:
  1. ule wosia maarufu wa tajiri hayati Reginald Mengi, wale waliousaini kama mashahidi walikiri baadaye mahakamani kuwa hawakuwa wameusoma. Na ndio waliochangia kumwangusha Klynn wao kwenye kesi ya mirathi
  2. Uliza watu waliochukua mikopo benki kama huwa wanasoma chochote kwenye ile mikataba zaidi ya kiasi cha pesa wanayokopa. Baadaye madalali wakija kuuza nyumba zao ndio wanaanza kuzunguka kutafuta mawakili
  3. Wewe mwenyewe hizo Apps na mambo mengine unayojiunga ya mitandaoni, ni mara ngapi umesoma ile mikataba mirefu unayowekewa? Mara nyingi kama sio zote unatafuta tu kile kitufe cha ACCEPT unabofya maisha yanaendelea.
Ni desturi yetu watanzania. Labda tuanze leo kujirekebisha
alikuwepo mtanzania mmoja (sasa ni hayati) yeye aliwahi sema alikuwa analala na mafaili kitandani,akiamka anayapitia kwa kina...labda tumshauri huyu Rais wetu nae ajenge utaratibu wa kusoma kwa kina( umesema watanzania hatupendi kusoma) labda na yeye yumo kwenye kundi letu la kutosoma vitu
 
Angedili vikali mno na hao wanaompelekea majina yasiyokuwa na sifa. kuna haja ya kuwa mkali sometimes!
Tunataka kujiaminisha zaidi kuwa makosa ni ya wapeleka majina peke yao, lakini anaeteuwa pia anatakiwa kuyapitia kwa kina kama kweli tunamlipa mshahara wa kodi zetu kwa kazi hizo...haya ni majina, vipi kuhusu vitu vingine ambavyo vyaweza hatarisha maisha ya watanzania,aweza pelekewa na hao tunaosema wanamhujumu,kwa kuwa havipitii kwa kina,atasaini tu ikaja kuleta shida alafu tuseme anahujumiwa
 
Nenda kwenye mawizara, serikalini wasomi wenye Degree, Masters na PhD wamejaa tele wala huhitaji kuwasha tochi, fomu four anatoboa vipi kwenye nafasi ya RAS, yaani mtu mwenye qualifications za kufanya usafi maliwatoni anakuwa RAS, are we serious? mnataka kuua kabisa hii nchi..
 
Kuongoza watu ni kazi ngumu sana. Namuombea mama apate hekima na asimame imara ili tuzidi kusonga mbele. Sasa inabidi aangalie kama kila teuzi inakidhi vigezo
 
Back
Top Bottom