Rais Samia hongera kwa kurekebisha makosa yaliyofanyika kwenye uteuzi wa Azza Hilal Hamad

Yego mwamba!
 
Mkuu umeliona hilo!! laiti kama mama hangekuwa na mauzoefu ya kazi za kiofisi jamaa angekuwa RS. Kwa mapungufu haya 3 ningekuwa ndio mimi, huyo msaidizi wangu wa masuala ya documention ningemtumbua.
Siyo kumtumbua tu pia kumchukulia hatua kali.
Unaanzaje kumdanganya rais wa nchi na kuendelea kudunda mtaani?
 
Wanateuliwa kwahiyo kabla ya kula kiapo , mama ana nafasi ya kurekebisha pale panapoonekana panahitaji marekebisho!! Mama ni msikivu na hupokea ushauri kutoka kwa wananchi anaowaongoza!
 
vyombo vinavyo msaidia Mhe.Rais vinapaswa viongeze umakini.
Mbona kuna kiongozi alituaminisha kuwa wateuliwa huwa wanapitia kwenye machujio matatu? au inakuaje ?
 
Kama amerebisha ni sawa, lakini mimi binafsi nisingeona elimu yake kama ndio tatizo. Tanzania hii kwenye uongozi sijaona tofauti kati ya mwenye certificate, diploma, degree moja, degree 2, PhD wala Processor kwenye umahiri wa kutatua kero za watu.

Kuna watu ni maprofesa lakini mambo hayaendi na kuna watu Wa darasa LA saba lakni mambo ya wananchi na mambo yao yanakwenda. Rais anaweza kuzunguukwa na maprofessor waoga kutoa ushauri mzuri kwa rais wakihofia matumbo yao. Kuna wasomi wezi na wavivu.

Akili huwa tunazaliwa Nazo hizi za kusoma ni nyongeza tu, wanaotahili watoto huko vjijini ni mangaliba tu, wazee ambao hana elimu wamesomesha watoto wao hadi vyuo vikuu lakini wazazi wasomi kabisa ambao watoto wao wanavuta bangi, madawa ya kulenya na kushindwa kusoma.

Huko mataifa ya kiarabu hakuna PhD nyingi lakini maisha yao yanasonga.

Wakati huu Wa kurekebisha makofu ya ukabila, ukanda, udini, na jinsia kwenye nafasi tusiangalie saaaana kigezo cha degree kwenye ajira za uongozi, vigezo vya elimu vibaki zaidi kwenye taasisi za elimu, vyuo vyetu.

Kwani RAS anafanya Kazi gani kubwa mno inayohitaji kuwa na PhD? Kusema kijiji kile hakina maji twende tukawachimbie bwana kunahitaji elimu gani. Kazi yake si kuratibu watalaamu kama wahandisi, wahasibu na wenyengine wate kwenye mkoa watende kwa mujibu Wa taaluma na viapo vyao?
 
Hiyo tabia ya kulala na mafaili sidhani kama ilitusaidia, labda ilimsaidia aliyekuwa nayo!
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwa watu kama hawa ambao makosa ya kibinadamu yanafanyika kwenye teuzi zao na hatimaye kutenguliwa, nashauri kama raia wa JMT, baada ya kutenguliwa teuzi zao, wawe wanapozwa kwa kutafutiwa nafasi nyingine mbadala inayoendana na kiwango cha elimu yao, iwapo tu kutenguliwa huko kunakuwa hakujatokana na sababu zingine zaidi nje ya eimu yao; ili kukwepa kuya-frustrate maisha yao yaliyoko mbele yao, na familia zao
 
Nafikiri mama hatataka kuingizwa chaka kwenye hizi nafasi za kiutendaji ndo maana anabadirisha haraka sana akigundua jambo haliko sawa, na hata kwenye nafasi za kisiasa bado atataka kuwa na watu competent....kwa hiyo wachomekaji wasifikiri watafanikiwa na inaweza kuwagharimu wao wenyewe.
 


Nacheka kwa dharau! Aha! Aha! Ahaa!​
 
Hiyo tabia ya kulala na mafaili sidhani kama ilitusaidia, labda ilimsaidia aliyekuwa nayo!
Unalala Na mafaili we we ni kichaa? Ubongo wenye afya ni ule unaopata muda wa kutosha wa kupunzika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…