Rais Samia hotuba yako imejitoshela ila naomba nikosoe maeneo mawili Kwa kesho nzuri ya Tanzania

Rais Samia hotuba yako imejitoshela ila naomba nikosoe maeneo mawili Kwa kesho nzuri ya Tanzania

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Naomba kukupongeza Kwa hotuba nzuri inayoeleza kinaga ubaga umefanini na unategemea kufanya Nini huku ukiweka wazi vyanzo vyote vya fedha Kwa Kila mradi, nimependa umekuwa wazi kuonyesha namna tunavyohitaji mahusiano yakimataita kujenga uchumi

Pamoja na hotuba nzuri nimejisikia vibaya kusikia mambo yafuatayo
1. Umeeleza Kwamba umeagiza china meza na viti zaidi ya elfu thelasini; Mhe. RAIS Kwa tatizo la ajira tulilonalo na Kwa ukwasi uliopo sikutegemea kama Bado mnawaza kuagiza nje bidhaa zinazotengenezwa hapa nchini.

Ungetoa tenda Kwa karakana za hapa nchini bara na visiwani, ungetoa tenda Kwa mafundi wetu hapa nchini aidha Kwa kutumia mbao au chuma naamini ungetoa ajira,fedha ingebaki ndani na ungekuza uchumi. Huko china wangewekeza kuagiaza Ulaya wasingetajirika na wala wasinge kuwa na viwanda Leo.

Nikuombe kama aujalipia rudisha fedha zitumike nchini wapo mafundi wengi sana wamekosa KAZI. Na Hii nitoe Rai Kwa RAIS wa Muungano, yawezekana hata majengo yetu ya idara na Wizara Dodoma tumepanga kupeleka fedha china, pls wapeni KAZI makampuni ya ndani na ikiwezekana tupige marufuku kuagiza furniture za Serikali nje.

2. Nimekusikia unasema uwanja wa ndege Zanzibar mmekodishwa kwa kampuni ya Uatmrabuni waendeshe. Pls tumeona kilichotokea Zambia na Entebe, kwanini maeneo haya nyeti tunakabidhi wageni watusaidie kuendesha? Are we safe?

3. Mwisho, nimesikia miradi mingi Fedha zinatoka kwenye mikopo; je uwezo wa Zanzibar kulipa upoje? Tusinogewe kukopa tukauza kisiwa chetu.

Mwisho nikupongeze Kwa uwazi na nikuombe ujitahidi sana kupunguza kukopa na kuhakikisha tunafanya manunuzi ndani kukuza ujuzi na utaalamu wa WATU wetu.
 
Inakuwaje Mzanzibari awe mbunge was Mkuranga wakati Zanzibar sisi hata kisehemu Cha kupanda us moja hupati?
 
Hivi mfano mikopo kungekuwa hakuna nchi icnge weza kujenga miundo mbinu au kujiendeleza sindo maana yke
 
Beatrice Kamugisha ni nani?

Hongera kwa kuwa na uwezo wa kuikosoa serikali pale inapoenda mrama.

Kama utakuwa under 45 wewe ni mmojawapo kati ya wale vijana Nyerere aliokuwa akiwataka na kuwatabiri " tunataka Tanzania yenye vijana wasubutu jeuri wanaoweza kuihojo serikali na kuikosoa" siyo Tanzania ya ndiyo mama.

Nirudi kwenye mada no 2. Nidalili za nchi kuuzwa naona wameamua kuanza na zenji waarabu wakifika bei watanunua tena icho kisiwa.
 
Ila wabongo kwa siasa hatujambo sana. Sasa hotuba imejitosheleza unakosoa nini. Ni either haijajitosheleza au usikosoe kitu
 
Viti na meza from China!! Tunakwama wap
Asante kwa uzi makini hujawah kosea
 
Ila wabongo kwa siasa hatujambo sana. Sasa hotuba imejitosheleza unakosoa nini. Ni either haijajitosheleza au usikosoe kitu
Mkuu kuna namna bora ya kumkosoa mtu bila kumkwaza,mchangiaji kaitumia namna hio....Ni kama kupiga hodi kabla hujaingia ndani!!..
 
Wanaakopewa kupitia Tanganyika kwa koti la JMT ila kulipa hawalipi hawa kupe..halafu mali na vitega uchumi wanawapa waarabu..mbao zimejaa iringa na njombe..hawataki kuagiza fanicha Tanganyika..hawa ni kupe tena zaidi..

Parasitic muungano.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom