Rais Samia hurumia wazee waliolitumikia taifa kwa uaminifu leo wanalipwa Tsh 3,000 kwa siku

Rais Samia hurumia wazee waliolitumikia taifa kwa uaminifu leo wanalipwa Tsh 3,000 kwa siku

ccm ingepumzika kwa muda wananchi wangeheshimika. shida tunaonekana kama manyani, tukirushiwa mkate tunakenua.
haiwezekani kila sekta kuna malalamiko na bado mnaimba tunaimani na hicho chama.
 
Je wazee wasiokuwa waajiriwa serikali 'HAWAJALITUMIKIA' Taifa? na vipi ushafikiria hao nao wanaishi vipi bila pesa ya mwezi?
Inaonekana wewe ni mgeni kwenye mambo ya ajira, unapoajiriwa Kila mwezi unakatwa kwenye mshahara wako, hela hiyo inatunzwa/kuwekezwa ili unapostaafu na huna nguvu ya kutafuta unapewa kidogo mpakà mwisho wa maisha yako. Hao unaosema walitumia muda wao wakifanya shughuli binafsi
 
Inaonekana wewe ni mgeni kwenye mambo ya ajira, unapoajiriwa Kila mwezi unakatwa kwenye mshahara wako, hela hiyo inatunzwa/kuwekezwa ili unapostaafu na huna nguvu ya kutafuta unapewa kidogo mpakà mwisho wa maisha yako. Hao unaosema walitumia muda wao wakifanya shughuli binafsi
Kama unalijua hilo, hicho wanachopewa ndo haki yao kwa kipato walichokuwa wanapata.
Kila kundi likitaka kupewa 'special' treatment nchi haitopiga hatua.
 
Pana wastaafu wa shirika la reli Tanzania wanapigwa danadana tu malipo ya tuzo licha ya maamuzi ya mahakama.
 
Raisi wangu Samia naandika post hii nikiamini kwa huwa unapitia jukwaa hili kama siku moja ulivyotwambia. kama siyo wewe kuusoma mwenyewe basi naomba wasaidizi wako wakufikishie ujumbe huu.

Kuna wazee wastaafu waliolitumikia taifa hili kwa uaminifu, na unajua kuwa huko myuma hapakuwepo ujanja ujanja unaofanywa na waajiriwa wa siku hizi.

Mshahara ulikuwa mdogo na bado waajiriwa walikuwa waaminifu. mpaka mtu anastaafu hana nyumba wala shamba, mategemeo ni kuwa atakapo staafu atalipwa pension itakayomtunza mpaka kufa. Lakini wastaafu wa namna hiyo (waliostaafu miaka mingi ya nyuma) sasa hivi wanalipwa sh 100,000 kwa mwezi.

Hii ilipandishwa (kama sikosei) miaka zaidi ya 5 iliyopita. Toka wakati huo bei za vitu zimepanda bei mara dufu. Wanalipwa hela kwa siku ambayo haiwezi hata kununua kilo ya sukari au mchele. Mahitaji ya wazee ni mengi na nguvu ya kufanyakazi hawana. Wataishije hawa?

Hawa wazee hawana mtetezi. Mfanyakazi anapostaafu, vyama vya wafanyakazi ukoma kumtetea. Wastaafu hawana mtetezi bungeni kama walivyo wanawake. Wabuge wanaangalia masilahi yao tu. Mara moja niliwahi kumsikia mbunge mmoja (Mwijage ) akiongea juu ya hili. Wazee hawa wakati mwingine wanazidiwa na wanaopata hela ya TASAFU.

Wazee hawa nina imani siyo wengi kiasi cha kushindwa kulipwa vizuri na mifuko ya Pension. Juzi mfuko mmoja ulikuwa unajinadi kuwa na kiasi cha ma-trilion za hela za Kitanzania. Kwa hesabu za haraka haraka, hata wangekuwa na idadi ya 100,000 tuseme walipwe sh 200,000 kwa mwezi, watalipwa kama 20 billion. Ni kitu kidogo sana ambacho serikali inaweza.

Hebu fikiria wabunge wanalipwa kiasi gani kwa siku pale Dodoma, hebu fikiria hela zinazofujwa na watumishi walioko kazini, hebu fikiria viongozi wastaafu wanaolipwa asilimia 80 za walioko kazini, hebu fikiria wake za viongozi wanavyolipwa, hebu fikiria hata wanavyuo wanaolipiwa na HESLB (10,000) kwa siku., hebu fikiria wafanyakazi wa mifuko ya jamii (NSSF, PSSSF nk) mishahara yao kwa mwezi

Kwanini hawa wazee wateswe hivyo, kwa nini waishi kama vile walikosea kutumia muda wao kulitumikia taifa lisilowakumbuka. Ni mawazo yangu kuwa kitendo cha kuwalipa wazee pension mbovu kinaweza kuwafanya wafanyakazi waliopo kazi kuiba hela za umma ili kujitengenezea maisha yao ya baadae yasije kuwa mabaya huko mbeleni.

Wewe ni mama na mzee pia. Hebu vaa viatu vya mzee mstaafu anayelipwa sh 100,000, piga bajeti ya namna ya kutumia pension. Unahitaji kununua sukari, mchele, mboga n.k, unahitaji kwenda hospital, matumizi ni mengi na hayaelezeki. Wengi wao wanakufa kwa mtimanyongo.

Wanaishi kwa masimango kwamba hawakuwa wajanja wa kutumia mali ya umma, walitumia muda wao vibaya walipokuwa kazini. Kwanini mtumishi mstaafu wa umma awe omba omba?

Mapendekezo yangu mawili:-
-Kima cha pension kipandishwa na kuwa sh 200,000 kwa mwezi.
-Kila unapopandishwa mshahara, angalau nao wape 80% ya kima cha chini, kama ilivyo kwa viongozi wastaafu,
-Vyama vya wafanyakazi (najua wapo humu wanasoma) wasikome kuwatetea waliokuwa wafanyakazi wao, Wajue na wao ipo siku watastaafu. Nani atawatetea?

Nawasilisha
Umeongea vema na mimi naongezea wazee wapo wengi Tanzania na wote wametumikia nchi hii lakini hawana pensheni mfano wakulima, wavuvi, wafugaji, n.k naomba Rais atoe pensheni kwa wazee wote kuanzia miaka 65 kwani wanateseka sana
 
Hawa wazee huwa ni hodari sana wa kuvaa kofia na Tshirt za ccm, hayo ni mambo ya familia, waachie wana familia, kama na wewe ni mwana familia yajadilini kwenye vikao vya ndani.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Wastaafu wa 2018 kuja juu wengi bado wanasotea mafao baada ya kupewa pungufu na pension ya kila mwezi wanapewa pungufu hadi kesho.

Huko kazini vijana pigine haswa mjenge muajiri hatokuthamini kamwe siku umestaafu.
 
Kama unalijua hilo, hicho wanachopewa ndo haki yao kwa kipato walichokuwa wanapata.
Kila kundi likitaka kupewa 'special' treatment nchi haitopiga hatua.
Kama unaweza tafuta Sheria ya pension uone matakwa yake. Pension itakuwa inarekebishwa mara kwa mara kulingana na inflation inavyokuwa. Kigezo kikubwa Cha inflation ni upandaji wa vyakula, angalia vyakula vinavyopanda Bei, angalia mafuta, nk.
Naomba niachie hapo nisiseme mengi na kuharibu lengo la Uzi huu. Nafikiri wewe ni mmoja wa watu wenye roho mbaya. Mbona hujasema lolote viongozi wastaafu wanapopewa asilimia 80 ya waliopo madarakani, mbona hujasema lolote kwa wanaopata hela ya TASAF, .......
 
Back
Top Bottom