Mluu ni mambo gani ambayo yakiondolewa itafanya polisi isiwe jeshi badala yake iwe huduma ?
Wananchi watawatandika kama hawana akili nzuri maana wanahasira nao sana hao waduduNdio wavuliwe Bunduki na mabomu ya machozi na ma-tankers za majiwasha.
Yaani hilo jeshi usiliguse ndugu. Tunalitegemea mno chama chetu wakati wa uchaguziMheshimiwa Rais
Nianze kwa kukusalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Lengo ni lile lile la kazi iendee.
Tumekuwa na mijadala nchini mwetu kwa nyakati tofauti kuhusu namna Jeshi letu la Polisi linavyofanya kazi. Mara nyingi Jeshi limekuwa likishutumiwa kwa masuala kadhaa ikiwamo kujihusisha na vitendo vya Rushwa, kubambikia watu kesi, kushirikiana na wahalifu na masuala mengine kama hayo. Pengine sio rahisi sana kuthibitisha tuhuma hizi.
Hivyo basi, napenda nitumie fursa hii kupendekeza kwako ulifumue na kuliunda upya Jeshi la Polisi. Kwamba Polisi iwe ni huduma kama huduma za uhamiaji. Kwa mfano, badala ya kuwa na Jeshi la Polisi tuwe na Huduma ya Polisi. Vivyo hivyo tuwe na Huduma ya Magereza etc.
Mambo ya Kijeshi yabaki kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania. Imani yangu ni kwamba tukiwa na Huduma ya Polisi chombo hiki kitajikita kuelimisha Raia huku kikitekeleza majukumu ya ulinzi wa Raia na Mali zao. Kwenye jumuiya yetu ya SADC wenzetu wa Botswana hawana Jeshi la Polisi badala yake Wana huduma ya Polisi. Natumai tunaweza kujifunza kwao.
Hivyo basi ikikupendeza Mheshimiwa Rais waweza kuelekeza vyombo vyako vifanye uchunguzi na utafiti zaidi kuhusu hili kwa kuzingatia mazingira ya nchi yetu na maendeleo yetu. Kisha utujalie tupate chombo hiki cha Huduma ya Polisi.
Nawasilisha.
Una PhD?Naunga mkono hoja !
Ila jiandae kwa povu kutoka kwa afande chacha!
Unataka kuniambia kuwa kurekebisha huu mwelekeo lazima jeshi livunje ili iwe huduma hapo ndo wataweza kurekebisha mwelekeo ?Mwelekeo uwe kuelimisha Raia zaidi badala ya ilivyo sasa kwamba ukiwa mikononi mwa Polisi uhai wako unakuwa mashakani. Badala yake uwe salama ukiwa mikononi mwa Polisi.
Sio kwamba ukiwa mikononi mwa Polisi kesho yake tukute umekufa.
Mandate ya Jeshi ni mwendo wa Kijeshi.Unataka kuniambia kuwa kurekebisha huu mwelekeo lazima jeshi livunje ili iwe huduma hapo ndo wataweza kurekebisha mwelekeo ?
Au inawezekana kurekebisha mwelekeo huu wakati polisi likiwa bado jeshi na huduma bado zikapatikana ?
Haya maneno yako tafsiri yake ni kuwa lazima jeshi livunje ili iwe huduma hapo ndo wataweza kurekebisha mwelekeo na kuwa huduma.Mandate ya Jeshi ni mwendo wa Kijeshi.
Mandate ya Huduma ni mwendo wa Huduma.
PhD kutoka jalalani au?Una PhD?
Green Guards jeshi la Nape Nauye ila alipotishiwa bastola hatukuliona.Jeshi la polisi
Jeshi la wananchi wa Tanzania
Jeshi la akiba
[emoji1787][emoji1787]Majeshi ni mengi kwakweli, tuwe na huduma ya wananchi wa Tanzania sasa