JABALI LA KARNE
JF-Expert Member
- Apr 19, 2021
- 3,090
- 5,876
Kama Huna PhD kaa kimyaPhD kutoka jalalani au?
😂😂😂
Kama Huna PhD kaa kimya
Unatafuta kupigwa na huo utu uzima shauli zako huo ni uchocheziAu alibadilishe tu jina na kuliita Jeshi la Kupokea Mlungula Tanzania JKMT!!
Sikupingi mkuu,nilicho maanisha ni watu kuelewa ili kupata watu wengi zaidi watakao upigia upatu mfumo unao upendekeza.Bila uelewa historia ni mwalimu mzuri.Wanasiasa wetu ni mahiri wa kudandia hoja bila kuelewa sawasawa ndio maana nikashauri uuchambue mfumo kwa kina japo kidogo
Nimecheka kweli.Siku kaza tu Mmesema watu waachiwe wamebambikiwa kesi wameachiwa ile wamerudi kitaa ujambazi umerudi.Sasa jiulize walibambikiwa au wanafanya siasa kwenye Ulinzi.Mheshimiwa Rais
Nianze kwa kukusalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Lengo ni lile lile la kazi iendee.
Tumekuwa na mijadala nchini mwetu kwa nyakati tofauti kuhusu namna Jeshi letu la Polisi linavyofanya kazi. Mara nyingi Jeshi limekuwa likishutumiwa kwa masuala kadhaa ikiwamo kujihusisha na vitendo vya Rushwa, kubambikia watu kesi, kushirikiana na wahalifu na masuala mengine kama hayo. Pengine sio rahisi sana kuthibitisha tuhuma hizi.
Hivyo basi, napenda nitumie fursa hii kupendekeza kwako ulifumue na kuliunda upya Jeshi la Polisi. Kwamba Polisi iwe ni huduma kama huduma za uhamiaji. Kwa mfano, badala ya kuwa na Jeshi la Polisi tuwe na Huduma ya Polisi. Vivyo hivyo tuwe na Huduma ya Magereza etc.
Mambo ya Kijeshi yabaki kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania. Imani yangu ni kwamba tukiwa na Huduma ya Polisi chombo hiki kitajikita kuelimisha Raia huku kikitekeleza majukumu ya ulinzi wa Raia na Mali zao. Kwenye jumuiya yetu ya SADC wenzetu wa Botswana hawana Jeshi la Polisi badala yake Wana huduma ya Polisi. Natumai tunaweza kujifunza kwao.
Hivyo basi ikikupendeza Mheshimiwa Rais waweza kuelekeza vyombo vyako vifanye uchunguzi na utafiti zaidi kuhusu hili kwa kuzingatia mazingira ya nchi yetu na maendeleo yetu. Kisha utujalie tupate chombo hiki cha Huduma ya Polisi.
Nawasilisha.
Tumepishana sana Mila na desturi .Bostwana ina Wandebele na Washona tu ila Bongo tunayo Makabila 120 kule umasaini na Ukurya ukiiba ng'ombe unaleta Nyumbani ukoo unakuwa tajiri wewe unaonekana tajiri ila kule Kwa Wadigo na Wapemba Hapo utatengwa hata na Mkeo.sasa usijifananishe.Kumbuka siasa zetu pale congo, Burundi,Msumbiji, bado wanaendelea na vita za wenyewe wakati huko Botswana kila kona kupo shwari.Police Service ni bora zaidi katika nchi yetu, mbona botswana wameweza sisi tunakwama wapi?
Ni kweli mkuu, kama kubadili tu jina na staff wakabakia ni wale wale, hakuna kitu kitakachokuwa kimefanyika.Wazo limetoka,kama ungeandika pia mfumo huo unafanyaje kazi,tofauti ya kuwa jeshi na huduma ni ipi japo umedokeza kidogo lakini ungeeleza zaidi hizo faida kulinganisha na changamoto zilizopo.Ukifanya hivyo hoja yako itapata mashiko hata na wale ambao wanatarajia kukupinga pasi na kujua unacho jengea hoja watakao kupinga ni wale majuao unacho simamia.Ngoja wakuu waje nami ntarudi....
MkuuTumepishana sana Mila na desturi .Bostwana ina Wandebele na Washona tu ila Bongo tunayo Makabila 120 kule umasaini na Ukurya ukiiba ng'ombe unaleta Nyumbani ukoo unakuwa tajiri wewe unaonekana tajiri ila kule Kwa Wadigo na Wapemba Hapo utatengwa hata na Mkeo.sasa usijifananishe.Kumbuka siasa zetu pale congo, Burundi,Msumbiji, bado wanaendelea na vita za wenyewe wakati huko Botswana kila kona kupo shwari.