Rais Samia ikukupendeza tuondolee DC Magoti hapa Kisarawe, amefeli kila kitu

USSR

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2015
Posts
10,904
Reaction score
26,184
Watu hatuna maji yeye analeta story za uchaguzi. Tuliambiwa kuwa hapo ikulu alikufelisha na wewe ukaamua kuturushia huku Kisarawe huku ni majanga kabisa .

Hapa Kisarawe wilaya nzima hatuna maji yeye yuko size na ishu za uchaguzi utadhani anagombea

Barabara mbovu kila sehemu yeye yupi size na uchaguzi tu na matamko .

Ikikupendeza muondoe tuletee anayeweza kazi

USSR
 
Halmashauri inafanya nini? Una mbunge, diwani na Baraza la madiwani (Halmashauri) ambao ndo wawakilishi wako, umefanya jitihada gani kuwawajibisha kabla ya kurukia kwa mkuu wa wilaya? Unayajua majukumu na mipaka ya mkuu wa wilaya? Unataja akuletee maji kwa bajeti ipi?
Una chuki zako nje ya hizo kero.
 
Nimepakumbuka Minaki boys enzi hizo.

Kulikuwa na maji ya fangasi sana ila Magufuli akaleta maji kutoka mto Ruvu.
 
Sasa maji na Barabara DC atafanya kitu gan yarabi?

Jafo anafanya kitu gani
 
Hujui majukumu ya DC? Mbunge wake anaitwa nani?
 
Hivi mbunge wenu anaitwa nani mkuu ila ni kweli maana juzi nilikuwa huko kweli Hali ni mbaya mitaa imekaa hovyo sana barabara za tabu mno poleni sana ndugu zangu
 
Mama na mtoto akili zinafanana. Kesi ya nyani unakwenda kumshtakia kwa Tumbuli, tegemea majibu yale yale.
 
Mnalo hilo wanakisarawe. Hangaikeni na zimwi lenu hilo. Mkiweza au ikiwapendeza mfungieni kwenye chupa mumtupe baharini.
 
Hivi mbunge wenu anaitwa nani mkuu ila ni kweli maana juzi nilikuwa huko kweli Hali ni mbaya mitaa imekaa hovyo sana barabara za tabu mno poleni sana ndugu zangu
Umefika morogoro mjini? Maji, barabara, uchafu, vumbi.. kumbe jehanamu iko hapa hapa duniani?
 
Hapo DC wala hahusiki, labda kama una chuki binafsi dhidi yake, kuna mamlaka ya maji safi, Mkurugenzi wa Halmashauri (DED) na hasa huyo mbunge wenu. Pambana nao hao watatu wakuletee maji achana na mkuu wa wilaya.
 
Aise ni dhahir kwamba kipaumbele kinapaswa kuwa maendeleo ya msingi kama maji, miundombinu, na huduma muhimu. Kina muda mwingine, siasa hufunika changamoto za kiuhalisia, na viongozi wanapaswa kuzingatia matatizo ya wananchi kuliko kushughulikia masuala ya uchaguzi pekee lakn ni vyema viongozi wasiofaa wasipewe kura kabisa.
 
Your browser is not able to display this video.

Your browser is not able to display this video.
 
Nimepakumbuka Minaki boys enzi hizo.

Kulikuwa na maji ya fangasi sana ila Magufuli akaleta maji kutoka mto Ruvu.
Mkuu wewe utakuwa umemaliza recently, kumbe mliletewa maji ya Ruvu?? Mi nakumbuka tulikuwa tunashuka kule pondi kwenyewe... aiseeee... Ilikuwa noma sana
 
Generally, Kisarawe ni wilaya yenye kila aina ya changamoto.. wakati mwingine najiuliza hivi criteria ya sehem kuwa wilaya ni ipi?
 
Kwa akili yako kweli DC ndo analeta maji?hakuna Ruwassa hapo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…