Halmashauri inafanya nini? Una mbunge, diwani na Baraza la madiwani (Halmashauri) ambao ndo wawakilishi wako, umefanya jitihada gani kuwawajibisha kabla ya kurukia kwa mkuu wa wilaya? Unayajua majukumu na mipaka ya mkuu wa wilaya? Unataja akuletee maji kwa bajeti ipi?
Una chuki zako nje ya hizo kero.
Kweli kabisa .
Kumshambulia Magoti peke yake ni chuki binafsi .
Mimi kwa mtizamo wangu wakuu wote wa mikoa na wilaya wamefeli Sana hawstahili kukalia hizo nafasi .
Nafasi za Ukuu wa Wilaya na Mikoa zinastahili kupewa wanajeshi ,Polisi na usalama wa Taifa basi ((Usalama wa Taifa waliosomea medani za kivita na usalama wa nchi kwa ujumla sio wapambe kama wale wahuni wa Green Guard na red Guard 😂😂😂)).
Nafasi za Ukurugenzi wanatakiwa Wapewe Walimu hasa Mahead master waliofanya vizuri kwenye mashule ya serikali kwenye usimamizi ndani ya Halmashuri zao au Maafisa Elimu waliosimamia vizuri kazi za maendeleo ya Elimu kwenye Halmashuri zao . Lakini Pia Wakurugenzi wanatakiwa wawe ni maofisa ndani ya Halmashauri kama Vile maafisa kilimo ,mdaktari na mafisa wazoefu ndani ya Halmashuri .
Kwa Tangu Kikwete hizo nafasi zimekua za kupeana kama zawadi au ushkaji na hata nyumba ndogo .
Hali inayosababisha usimamizi toka juu unakua mgumu sana.
Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi Wengi wapo kama Machawa wa Rais na sio wawakilishi wa Rais .
Matokeo yake miradi ya serikali inajengwa kwa kiwango cha chini sana . Rais anazindua jengo leo na bada ya miaka mitatu lina nyufa kama Chekecheke wakati mkuu wa Wilaya yupo .
Yote ni kwa sababu ya dharau kubwa ya wanasiasa kwa majeshi yetu na pia kupandikiza Machawa ndani ya majeshi hivyo kuyaona sio chochote sio lolote .
Watu wote wanaokua chini ya Rais wanatakiwa wawe ni wawakilishi wa Rais na wanaopokea amri ya Rais na kuisimamia kama yeye mwenyewe kwa usahihi na kwa utii.
Ndio maana wakati wa Mwalimu walikua na Elimu ya kawaida lakini walisimamia miradi ya maendeleo kwa uzalendo mkubwa . Hata ukiangalia miradi ya enzi za mwalimu zilijengwa kwa ubora zaidi japo Bajeti ilikua finyu na teknolojia ndogo na mawasiliano madogo.
Mtu hajawahi kuwa hata Afisa mtendaji wa kata leo anakua mkuu wa Wilaya .!!