Rais Samia: Inashangaza kifo cha Kibao kimeibua wimbi kubwa, hii sio sawa, kifo ni kifo

Rais Samia: Inashangaza kifo cha Kibao kimeibua wimbi kubwa, hii sio sawa, kifo ni kifo

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
"Siku kadhaa zilizopita ndugu zangu nchi yetu imepata msiba wa kuuawa kwa mmoja wa kiongozi wa CHADEMA, kifo kilichosisimua miili na akili za Watanzania na kuibua hisia kali hasa kwa wawakilishi wa baadhi ya mataifa ya nje wanaowakilisha nchi zao hapa kwetu. Nataka niungane nao na niseme kwamba kwasababu yoyote ile mauaji haya hayakubaliki na ndio maana serikali tuliyalaani na kutaka uchunguzi wa haraka ufanyike na ndivyo inavyofanyika Duniani kote."

“Nadhani nyie ni Mashahidi kule kwa wenzetu kulikoendelea kuna Mwanasiasa amekoswa kuuawa mara mbili (Trump) lakini tulichokisikia ni Serikali kutaka uchunguzi ufanyike kwahiyo si ajabu na kwetu baada ya tukio kutaka uchunguzi ufanyike na kazi nimeambiwa inaendelea vizuri”

“Baada ya tukio la Mzee Kibao nimekuwa nikiangalia maoni ya Viongozi mbalimbali wa kisiasa, Viongozi wa Dini baadhi yao wakiniomba nikemee mambo hayo, maoni ya Wazee mashuhuri nimemsikia Mzee wetu Butiku nae kasema, Wawakilishi wa Mataifa ya Nje hapa Nchini nao wametoa tamko, Jumuiya za Kiraia na Wananchi kwa ujumla na wenyewe wamesema waliyosema “

“Hisia za makundi yote niliyotaja zikiibuliwa na kifo kimoja tu cha Ndugu yetu Kibao lakini kuna vifo vinasemwa muda baada ya muda, Watoto Albino wanauliwa, Watoto wadogo wanauliwa, sijui Mzee kahisiwa uchawi kauliwa mpaka leo Watoto watatu wamekutwa wameuliwa huko Dodoma”

“Inashangaza kifo cha Ndugu yetu kibao kimeibua wimbi kubwa, kulaani, kusikitika, kulaumu kuita Serikali ya wauaji, kufanyaje, hii sio sawa, kifo ni kifo, tunachotakiwa kufanya Watanzania wote tukemeeane, tusimame imara kukemea mambo haya, damu ya Mtanzania ituume tusiwe tunamwaga damu bila sababu”
—— Rais wa Tanzania, Dkt. Samia kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro leo September 17,2024

My Take
Mautekaji ni kama yamechochewa tu, kutoka "drama"" mpaka "mtu mmoja tu".

PIA SOMA
- TANZIA - Dar: Ali Mohamed Kibao, kiongozi wa CHADEMA auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana
 
Hata mtu mzima mpumbavu naye huzeeka.

Hivi Mwanasiasa, na Tena wa CHAMA kikubwa, Tena katika Nchi iliyoingia mikataba ya kimataifa kuhusu Siasa ,, AUWAWE, yaan ichukuliwe kua ni Kifo Cha kawaida tu??.

Mpumbavu anatolea mfano Trump, Trump si Dunia nzima kila Chombo Cha habari kilisimama kazi zake na kuanza kufatilia habari za Trump?.kwann wasingempuuza tu kua ni mtu wa kawaida??.

Anashangaa nini Kwa Mzee Kibao??.

Kwann Mataifa yasiingilie Kati katika bara hili la kijinga ambalo víongozi ni madikteta?.
 
“Inashangaza kifo cha Ndugu yetu kibao kimeibua wimbi kubwa, kulaani, kusikitika, kulaumu kuita Serikali ya wauaji, kufanyaje, hii sio sawa, kifo ni kifo, tunachotakiwa...
Mbona na yeye aliagiza uchunguzi ufanyike? Hata yeye alistushwa pia, hii inatoa picha kuwa alichokisema kipindi kile KUHUSU uchunguzi hakukimaanisha and if that's the case, hakuna uchunguzi wowote utafanyika.......till then goodbye
 
Watu wamevumilia na kuugulia maumivu kwa muda kwa vifo vinavyotokana na kuteka,kutesa na kuuwawa ukijumlisha na vingine vyenye utata.

Nyongo imewazidi na wameamua kutapika.Hakuna mtu mwenye imani na polisi&the coys kama ambavyo chombo huru kingetumika au usaidizi wa nchi zenye weledi na nia njema vingetumika.Aelewe hilo.
 
Huko anakosema uchunguzi unaendelea tayari wahusika wamekamatwa. Sativa kila siku anawataja wahusika lakini nini kinafanyika?

Ndugu zangu wa CCM najua hata tukipiga kura kiasi gani bado nyie ndio mnaochagua kiongozi. Basi angalau tuwekeeni mtu wa maana basi.
 
Watu wamevumilia na kuugulia maumivu kwa muda kwa vifo vinavyotokana na kuteka,kutesa na kuuwawa ukijumlisha na vingine vyenye utata.Nyongo imewazidi na wameamua kutapika.Hakuna mtu mwenye imani na polisi&the coys kama ambavyo chombo huru kingetumika au usaidizi wa nchi zenye weledi na nia njema vingetumika.Aelewe hilo.
Chief Comforter anapogeuka Chief Mabezo na nadharau
 
Hapa naona tunapotoka kama Taifa.., Haipaswi mtu kushangaa kifo cha mtu kuibuia wimbi kubwa cha kushangaza ni kwanini na vifo vingine haviibui wimbi kubwa...,

Kwahio kila kifo cha Mtanzania hakipaswi kutokea na kifo chochote kiibue wimbi la watu kukemea sababu Damu yoyote ya mwenzetu (awe teja, mwanasiasa, mdangaji au asiye na mbele wa nyuma) inapaswa kukemewa wala hakipaswi kutokea... Na Kifo sio Kifo (natural cause is okay sababu ndio njia ya kila mmoja ila chenye mkono wa mtu au uzembe fulani hakifai kutokea)
 
Kifo ni kifo kama kimetokea kwa natural causes, sio kifo hiki cha mtu kunyakuliwa kwenye basi mchana kweupe na asubuhi yake maiti inaokotwa.

Hii kauli ya kifo ni kifo ina tia mashakla sana kwa ulinganifu wa vifo.... kwa kweli haikupaswa kutolewa kwa staili hii... hakikuwa ajali, hakikuwa ugonjwa, hakikuwa kujitakia kwa kunywa sumu, bali kilikuwa ni kwa baadhi ya ndugu zetu kujitwalia madaraka mikononi mwao na kudhurumu uhai wa msafiri yule wa basi.

Hivyo hakiwezi kuwa kwamba , kifo ni kifo, kamwe na kisilinganishwe kwa style hiyo... mjadara wa ulinganifu na makelele yote yanatokana na uhalari huo wa watu fulani kunyakua uhai wa wengine.. tatizo ndio hapo.
 
“Siku kadha zilizopita Ndugu zangu Nchi yetu imepata msiba wa kuuawa kwa mmoja wa Kiongozi wa CHADEMA, kifo kilichosisimua miili na akili za Watanzania na kuibua hisia kali hasa kwa Wafuasi wa Chama hicho, katika hali ya kushangaza kifo hicho kimeleta hisia kali pia kwa Wawakilishi wa baadhi ya Mataifa ya Nje wanaowakilisha Nchi zao hapa kwetu, nataka niungane nao na niseme kwamba kwasababu yoyote ile mauaji haya hayakubaliki na ndio maana Serikali tuliyalaani na kutaka uchunguzi wa haraka ufanyikke na ndivyo inavyofanyika Duniani kote”

“Nadhani nyie ni Mashahidi kule kwa wenzetu kulikoendelea kuna Mwanasiasa amekoswa kuuawa mara mbili (Trump) lakini tulichokisikia ni Serikali kutaka uchunguzi ufanyike kwahiyo si ajabu na kwetu baada ya tukio kutaka uchunguzi ufanyike na kazi nimeambiwa inaendelea vizuri”

“Baada ya tukio la Mzee Kibao nimekuwa nikiangalia maoni ya Viongozi mbalimbali wa kisiasa, Viongozi wa Dini baadhi yao wakiniomba nikemee mambo hayo, maoni ya Wazee mashuhuri nimemsikia Mzee wetu Butiku nae kasema, Wawakilishi wa Mataifa ya Nje hapa Nchini nao wametoa tamko, Jumuiya za Kiraia na Wananchi kwa ujumla na wenyewe wamesema waliyosema “

“Hisia za makundi yote niliyotaja zikiibuliwa na kifo kimoja tu cha Ndugu yetu Kibao lakini kuna vifo vinasemwa muda baada ya muda, Watoto Albino wanauliwa, Watoto wadogo wanauliwa, sijui Mzee kahisiwa uchawi kauliwa mpaka leo Watoto watatu wamekutwa wameuliwa huko Dodoma”

“Inashangaza kifo cha Ndugu yetu kibao kimeibua wimbi kubwa, kulaani, kusikitika, kulaumu kuita Serikali ya wauaji, kufanyaje, hii sio sawa, kifo ni kifo, tunachotakiwa kufanya Watanzania wote tukemeeane, tusimame imara kukemea mambo haya, damu ya Mtanzania ituume tusiwe tunamwaga damu bila sababu” —— Rais wa Tanzania, Dkt. Samia kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro leo September 17,2024
Dah! Kifo cha mzee Kibao ni cha kisiasa, CCM anaua CHADEMA hujui kama hilo ni hatari zaidi kwa amani ya nchi hii?.
 
Back
Top Bottom