Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Uuaji wa Mzee Kibao umeibua hisia kali sio kwa Waislamu tuu bali hata viongozi wa madhehebu mengine hasa ya Kikristo na balozi za nchi za Magharibu zisizokuwa za KiislamuWalibofya pabaya,marehemu angekuwa mgalatia hakuna ambaye angestuka
Kumuombea ili nini?Ni kwamba Rais wetu hatambui watu tunatofautiana 'hadhi' na umaarufu? Kifo ni kifo ndio, anataka kusema kifo cha M/kiti wa serikali ya mtaa kinaweza kupokelewa sawa na kifo cha Rais wa nchi?
Nafikiri tumuombee Rais wetu!
👆“Siku kadha zilizopita Ndugu zangu Nchi yetu imepata msiba wa kuuawa kwa mmoja wa Kiongozi wa CHADEMA, kifo kilichosisimua miili na akili za Watanzania na kuibua hisia kali hasa kwa Wafuasi wa Chama hicho, katika hali ya kushangaza kifo hicho kimeleta hisia kali pia kwa Wawakilishi wa baadhi ya Mataifa ya Nje wanaowakilisha Nchi zao hapa kwetu, nataka niungane nao na niseme kwamba kwasababu yoyote ile mauaji haya hayakubaliki na ndio maana Serikali tuliyalaani na kutaka uchunguzi wa haraka ufanyikke na ndivyo inavyofanyika Duniani kote”
“Nadhani nyie ni Mashahidi kule kwa wenzetu kulikoendelea kuna Mwanasiasa amekoswa kuuawa mara mbili (Trump) lakini tulichokisikia ni Serikali kutaka uchunguzi ufanyike kwahiyo si ajabu na kwetu baada ya tukio kutaka uchunguzi ufanyike na kazi nimeambiwa inaendelea vizuri”
“Baada ya tukio la Mzee Kibao nimekuwa nikiangalia maoni ya Viongozi mbalimbali wa kisiasa, Viongozi wa Dini baadhi yao wakiniomba nikemee mambo hayo, maoni ya Wazee mashuhuri nimemsikia Mzee wetu Butiku nae kasema, Wawakilishi wa Mataifa ya Nje hapa Nchini nao wametoa tamko, Jumuiya za Kiraia na Wananchi kwa ujumla na wenyewe wamesema waliyosema “
“Hisia za makundi yote niliyotaja zikiibuliwa na kifo kimoja tu cha Ndugu yetu Kibao lakini kuna vifo vinasemwa muda baada ya muda, Watoto Albino wanauliwa, Watoto wadogo wanauliwa, sijui Mzee kahisiwa uchawi kauliwa mpaka leo Watoto watatu wamekutwa wameuliwa huko Dodoma”
“Inashangaza kifo cha Ndugu yetu kibao kimeibua wimbi kubwa, kulaani, kusikitika, kulaumu kuita Serikali ya wauaji, kufanyaje, hii sio sawa, kifo ni kifo, tunachotakiwa kufanya Watanzania wote tukemeeane, tusimame imara kukemea mambo haya, damu ya Mtanzania ituume tusiwe tunamwaga damu bila sababu” —— Rais wa Tanzania, Dkt. Samia kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro leo September 17,2024
Tuondokane na CCM sasa hivi hapa!Hata mtu mzima mpumbavu naye huzeeka.
Hivi Mwanasiasa, na Tena wa CHAMA kikubwa, Tena katika Nchi iliyoingia mikataba ya kimataifa kuhusu Siasa ,, AUWAWE, yaan ichukuliwe kua ni Kifo Cha kawaida tu??.
Mpumbavu anatolea mfano Trump, Trump si Dunia nzima kila Chombo Cha habari kilisimama kazi zake na kuanza kufatilia habari za Trump?.kwann wasingempuuza tu kua ni mtu wa kawaida??.
Anashangaa nini Kwa Mzee Kibao??.
Kwann Mataifa yasiingilie Kati katika bara hili la kijinga ambalo víongozi ni madikteta?.
Kwa hiyo, kwa mantiki hii, Chadema alitaka wafanye jambo gani baada ya kuona mauaji yamezidi na yeye Rais wa nchi pamoja na wawakilishi wa wananchi hawaoneshi kulaani, kukemea wala kuguswa na uovu huo?“Siku kadha zilizopita Ndugu zangu Nchi yetu imepata msiba wa kuuawa kwa mmoja wa Kiongozi wa CHADEMA, kifo kilichosisimua miili na akili za Watanzania na kuibua hisia kali hasa kwa Wafuasi wa Chama hicho, katika hali ya kushangaza kifo hicho kimeleta hisia kali pia kwa Wawakilishi wa baadhi ya Mataifa ya Nje wanaowakilisha Nchi zao hapa kwetu, nataka niungane nao na niseme kwamba kwasababu yoyote ile mauaji haya hayakubaliki na ndio maana Serikali tuliyalaani na kutaka uchunguzi wa haraka ufanyikke na ndivyo inavyofanyika Duniani kote”
“Nadhani nyie ni Mashahidi kule kwa wenzetu kulikoendelea kuna Mwanasiasa amekoswa kuuawa mara mbili (Trump) lakini tulichokisikia ni Serikali kutaka uchunguzi ufanyike kwahiyo si ajabu na kwetu baada ya tukio kutaka uchunguzi ufanyike na kazi nimeambiwa inaendelea vizuri”
“Baada ya tukio la Mzee Kibao nimekuwa nikiangalia maoni ya Viongozi mbalimbali wa kisiasa, Viongozi wa Dini baadhi yao wakiniomba nikemee mambo hayo, maoni ya Wazee mashuhuri nimemsikia Mzee wetu Butiku nae kasema, Wawakilishi wa Mataifa ya Nje hapa Nchini nao wametoa tamko, Jumuiya za Kiraia na Wananchi kwa ujumla na wenyewe wamesema waliyosema “
“Hisia za makundi yote niliyotaja zikiibuliwa na kifo kimoja tu cha Ndugu yetu Kibao lakini kuna vifo vinasemwa muda baada ya muda, Watoto Albino wanauliwa, Watoto wadogo wanauliwa, sijui Mzee kahisiwa uchawi kauliwa mpaka leo Watoto watatu wamekutwa wameuliwa huko Dodoma”
“Inashangaza kifo cha Ndugu yetu kibao kimeibua wimbi kubwa, kulaani, kusikitika, kulaumu kuita Serikali ya wauaji, kufanyaje, hii sio sawa, kifo ni kifo, tunachotakiwa kufanya Watanzania wote tukemeeane, tusimame imara kukemea mambo haya, damu ya Mtanzania ituume tusiwe tunamwaga damu bila sababu” —— Rais wa Tanzania, Dkt. Samia kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro leo September 17,2024
Ajabu kabisa hii.🤔Chief Comforter anapogeuka Chief Mabezo na nadharau
Poor reasonings,mbowe aliyelikomalia jambo hili ni mvaaa vipedo ,lissu je!? Nyie watu ambao mko obsessed na dini ni wajinga sana.Walibofya pabaya,marehemu angekuwa mgalatia hakuna ambaye angestuka
Yeye anaona Tanzania ni mali yake binafsiHuyu mwanamke aambiwe kila kitu kina mwanzo wake! Wananchi wamefikia ukomo wa uvumilivu!
Wananchi watajilindaKuna hatari kubwa mbeleni, kuna dalili watu wataumizwa na kuumia.
Masikini Tanzania.
Kwanini CCM hawatekwi?Kifo ni kifo kama kimetokea kwa natural causes, sio kifo hiki cha mtu kunyakuliwa kwenye basi mchana kweupe na asubuhi yake maiti inaokotwa. Hii kauli ya kifo ni kifo ina tia mashakla sana kwa ulinganifu wa vifo.... kwa kweli haikupaswa kutolewa kwa staili hii... hakikuwa ajali, hakikuwa ugonjwa, hakikuwa kujitakia kwa kunywa sumu, bali kilikuwa ni kwa baadhi ya ndugu zetu kujitwalia madaraka mikononi mwao na kudhurumu uhai wa msafiri yule wa basi, hivyo hakiwezi kuwa kwamba , kifo ni kifo, kamwe....na kisilinganishwe kwa style hiyo... mjadara wa ulinganifu na makelele yote yanatokana na uhalari huo wa watu fulani kunyakua uhai wa wengine.. tatizo ndio hapo.