Rais Samia: Inashangaza kifo cha Kibao kimeibua wimbi kubwa, hii sio sawa, kifo ni kifo

“Siku kadha zilizopita Ndugu zangu Nchi yetu imepata msiba wa kuuawa kwa mmoja wa Kiongozi wa CHADEMA, kifo kilichosisimua miili na akili za Watanzania na kuibua hisia kali hasa kwa Wafuasi wa Chama hicho, katika hali ya kushangaza kifo hicho kimeleta hisia kali pia kwa Wawakilishi wa baadhi ya Mataifa ya Nje wanaowakilisha Nchi zao hapa kwetu, nataka niungane nao na niseme kwamba kwasababu yoyote ile mauaji haya hayakubaliki na ndio maana Serikali tuliyalaani na kutaka uchunguzi wa haraka ufanyikke na ndivyo inavyofanyika Duniani kote”

“Nadhani nyie ni Mashahidi kule kwa wenzetu kulikoendelea kuna Mwanasiasa amekoswa kuuawa mara mbili (Trump) lakini tulichokisikia ni Serikali kutaka uchunguzi ufanyike kwahiyo si ajabu na kwetu baada ya tukio kutaka uchunguzi ufanyike na kazi nimeambiwa inaendelea vizuri”

“Baada ya tukio la Mzee Kibao nimekuwa nikiangalia maoni ya Viongozi mbalimbali wa kisiasa, Viongozi wa Dini baadhi yao wakiniomba nikemee mambo hayo, maoni ya Wazee mashuhuri nimemsikia Mzee wetu Butiku nae kasema, Wawakilishi wa Mataifa ya Nje hapa Nchini nao wametoa tamko, Jumuiya za Kiraia na Wananchi kwa ujumla na wenyewe wamesema waliyosema “

“Hisia za makundi yote niliyotaja zikiibuliwa na kifo kimoja tu cha Ndugu yetu Kibao lakini kuna vifo vinasemwa muda baada ya muda, Watoto Albino wanauliwa, Watoto wadogo wanauliwa, sijui Mzee kahisiwa uchawi kauliwa mpaka leo Watoto watatu wamekutwa wameuliwa huko Dodoma”

“Inashangaza kifo cha Ndugu yetu kibao kimeibua wimbi kubwa, kulaani, kusikitika, kulaumu kuita Serikali ya wauaji, kufanyaje, hii sio sawa, kifo ni kifo, tunachotakiwa kufanya Watanzania wote tukemeeane, tusimame imara kukemea mambo haya, damu ya Mtanzania ituume tusiwe tunamwaga damu bila sababu” —— Rais wa Tanzania, Dkt. Samia kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro leo September 17,2024

My Take
Mautekaji ni kama yamechochewa rasmi
PIA SOMA
- TANZIA - Dar: Ali Mohamed Kibao, kiongozi wa CHADEMA auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana

Kifo kimetokana na watu wanaolipwa na kodi zetu!
 
Kuna kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu, hizi hisia zilizoibuka kuhusu tukio hili ni sauti ya Mungu maana Mungu husema na mioyo, ni heri leo tusikie sauti yake na turekebishe, kinyume na hilo tutashangazwa na njia zake za kufanya mambo maana njia zake si sawa na njia zetu.
 
Mna uhakika hayo maneno yametamkwa na Rais wa nchi?
Yaani hata yeye mwenyewe samia akikaa baadaye akayasikiliza maneno yake atakataa kama kayasema....inabidi in future awe anasoma script neno kwa neno....hana kabisa kipaji cha free style... ChoiceVariable naona rais amevibubujisha machozi ya furaha vyombo vya ullinzi...4Rs
 
Kwakweli kauli hii SI mjalabu kabisa kwahiyo serikali inaunga mkono matendo ya utekaji na wanajua kina nani wanausika ndio maana anato kauli za hovyo kama hizi
 
“Siku kadha zilizopita Ndugu zangu Nchi yetu imepata msiba wa kuuawa kwa mmoja wa Kiongozi wa CHADEMA, kifo kilichosisimua miili na akili za Watanzania na kuibua hisia kali hasa kwa Wafuasi wa Chama hicho, katika hali ya kushangaza kifo hicho kimeleta hisia kali pia kwa Wawakilishi wa baadhi ya Mataifa ya Nje wanaowakilisha Nchi zao hapa kwetu, nataka niungane nao na niseme kwamba kwasababu yoyote ile mauaji haya hayakubaliki na ndio maana Serikali tuliyalaani na kutaka uchunguzi wa haraka ufanyikke na ndivyo inavyofanyika Duniani kote”

“Nadhani nyie ni Mashahidi kule kwa wenzetu kulikoendelea kuna Mwanasiasa amekoswa kuuawa mara mbili (Trump) lakini tulichokisikia ni Serikali kutaka uchunguzi ufanyike kwahiyo si ajabu na kwetu baada ya tukio kutaka uchunguzi ufanyike na kazi nimeambiwa inaendelea vizuri”

“Baada ya tukio la Mzee Kibao nimekuwa nikiangalia maoni ya Viongozi mbalimbali wa kisiasa, Viongozi wa Dini baadhi yao wakiniomba nikemee mambo hayo, maoni ya Wazee mashuhuri nimemsikia Mzee wetu Butiku nae kasema, Wawakilishi wa Mataifa ya Nje hapa Nchini nao wametoa tamko, Jumuiya za Kiraia na Wananchi kwa ujumla na wenyewe wamesema waliyosema “

“Hisia za makundi yote niliyotaja zikiibuliwa na kifo kimoja tu cha Ndugu yetu Kibao lakini kuna vifo vinasemwa muda baada ya muda, Watoto Albino wanauliwa, Watoto wadogo wanauliwa, sijui Mzee kahisiwa uchawi kauliwa mpaka leo Watoto watatu wamekutwa wameuliwa huko Dodoma”

“Inashangaza kifo cha Ndugu yetu kibao kimeibua wimbi kubwa, kulaani, kusikitika, kulaumu kuita Serikali ya wauaji, kufanyaje, hii sio sawa, kifo ni kifo, tunachotakiwa kufanya Watanzania wote tukemeeane, tusimame imara kukemea mambo haya, damu ya Mtanzania ituume tusiwe tunamwaga damu bila sababu” —— Rais wa Tanzania, Dkt. Samia kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro leo September 17,2024

My Take
Mautekaji ni kama yamechochewa tu, kutoka "drama"" mpaka "mtu mmoja tu"
PIA SOMA
- TANZIA - Dar: Ali Mohamed Kibao, kiongozi wa CHADEMA auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana
Msiba kwa JIRANI....
 
Back
Top Bottom