Rais Samia: Inashangaza kifo cha Kibao kimeibua wimbi kubwa, hii sio sawa, kifo ni kifo

Rais Samia: Inashangaza kifo cha Kibao kimeibua wimbi kubwa, hii sio sawa, kifo ni kifo

Mama anapelekewa umbeya wanaita iteligensia😂 eti Chadema wapange mbinu za fujo kwa ngulelo Arusha kule kwa machuga wanao vuta bangi. Mama umewahi kufika kwa ngulelo hizo report za makonda kuwa nazo makini wanapandikiza watu wao wanasema ni Chadema. Kwa akili ndogo tu Lissu hawezi kupanga kitu cha siri na mtu ni mwazi sana, Mbowe sio mtu wa fujo! Mtu pekee ambaye watu hawamuamini ni wewe na sio chadema
 
Hata mtu mzima mpumbavu naye huzeeka.

Hivi Mwanasiasa, na Tena wa CHAMA kikubwa, Tena katika Nchi iliyoingia mikataba ya kimataifa kuhusu Siasa ,, AUWAWE, yaan ichukuliwe kua ni Kifo Cha kawaida tu??.

Mpumbavu anatolea mfano Trump, Trump si Dunia nzima kila Chombo Cha habari kilisimama kazi zake na kuanza kufatilia habari za Trump?.kwann wasingempuuza tu kua ni mtu wa kawaida??.

Anashangaa nini Kwa Mzee Kibao??.

Kwann Mataifa yasiingilie Kati katika bara hili la kijinga ambalo víongozi ni madikteta?.
Tujiulize wanaitaka kumuua Mzee Trump ni jeshi? Au watu binafsi ,naona maza anachanganya statement
 
Mtaani maisha ya wananchi ni magumu, ajira hamna + kutekana bila sababu za maana na kuuliwa juu, wananchi wamechoka.

Raisi wananchi hawampendi kutokana hali ya maisha kitaa pamoja na tabia chafu zilizoingia ambazo raia wanajua serikali ndio inahusika.

Kama huyu mama akiendelea kukaa madarakani miaka ijayo basi nina uhakika hii nchi haitakalika tena maana tegemeo la wananchi ni huyu Raisi atoke angalau wana amini ugumu wa maisha utapungua.

Matukio kama haya yanachochea hasira kwa wananchi na hatujui tabia gani nyengine itatokea baada ya suala la utekaji na mauaji.
 
Leo katika maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Polisi Tanzania mjini Moshi mheshimiwa rais amezungumzia vitendo vya mauaji ya watu vilivyokithiri nchini kwa kusema kifo ni kifo na akaonesha kushangazwa na watu waliochukulia kifo cha kiongozi wa CHADEMA mzee Ally Mohamed Kibao kwa uzito wa pekee. Mheshimiwa rais amehoji vimetokea vifo vingi lakini mbona watu wanakuza kifo cha mzee kibao pekee? Je, unaichukulia vipi kauli hii ya rais Samia?
 
Huyu mwanamke aambiwe kila kitu kina mwanzo wake! Wananchi wamefikia ukomo wa uvumilivu!
Ni hatari pasipotafutwa ufumbuzi. Ndiyo Kifo ni Kifo ila kuna Kifo kinaweza kikatokea kikawa ndiyo spark ya kuwasha moto ambao unakuwa mgumu kuuzima, endapo matukio kama hayo yanakuwa ni mwendelezo. Huko TunisIa, kifo cha Kijana muhitumu wa Chuo Kikuu liyekuwa amajiajili kwa kujenga kibanda cha kuuzia matunda kando ya barabara jijini Tunis, wenye mamlaka ya Jiji walipokuja na kukibomoa kwamba hakipaswi kuwepo pale, yule Kijana kwa uchungu wa kukosa ajira muda mrefu na sasa amejiajili lakini sasa wenye mamlaka yao wamebomoa Kibanda chake ambacho ndicho chanzo cha ajira yake, aliamua kujimwagia mafuta na kujiunguza. Kifo chake kiliamusha hasira za vijana waslokuwa na ajira na kuchangiwa na masiha magumu ya wananchi, Taifa la Tunis liliwaka moto kupitia Arab Spring , ambayo ilimuondoa mdaraka Rais Ben Ali mwaka 2011 , na kumaliza kipindi cha utawala wake wa almost 30 years in power. So tukio moja na Kifo cha Mtu mmoja kinaweza kikaleta matokeao yasiyotarajiwa, kama kwa Rais Ben Ali ambaye hakuona kama Kifo cha Kijana mmoja tu asiyekuwa na ajira aliyebomolewa kibanda chake na mamla ya jiji kuwa ni cha kawaida kama vifo vingine. Vifo vingine siyo vya kawaida na vinatofautiana kulingana na nature ya vifo husika na muhusika. Nilikuwa nakumbushia Historia, nikitambua kwamba hakuna Kifo kidogo, ila Vifo vingine ni zaidi ya Vifo kwa namna vinavyovuta hisia na hasira za umma.
 
Kifo ni kifo kama kimetokea kwa natural causes, sio kifo hiki cha mtu kunyakuliwa kwenye basi mchana kweupe na asubuhi yake maiti inaokotwa. Hii kauli ya kifo ni kifo ina tia mashakla sana kwa ulinganifu wa vifo.... kwa kweli haikupaswa kutolewa kwa staili hii... hakikuwa ajali, hakikuwa ugonjwa, hakikuwa kujitakia kwa kunywa sumu, bali kilikuwa ni kwa baadhi ya ndugu zetu kujitwalia madaraka mikononi mwao na kudhurumu uhai wa msafiri yule wa basi, hivyo hakiwezi kuwa kwamba , kifo ni kifo, kamwe....na kisilinganishwe kwa style hiyo... mjadara wa ulinganifu na makelele yote yanatokana na uhalari huo wa watu fulani kunyakua uhai wa wengine.. tatizo ndio hapo.
Na akumbuke tukio la Yule Simba Lisu, yeye akienda kumuona Nairobi, lakini sio watu wote wenye kuumizwa anakwenda kuwaona , Pia akumbuke Lisu alivyo lala ubalozi wa ujerumani na kusindikizwa eapoti
 
Na akumbuke tukio la Yule Simba Lisu, yeye akienda kumuona Nairobi, lakini sio watu wote wenye kuumizwa anakwenda kuwaomba. Pia akumbuke Lisu alivyo lala ubalozi wa ujerumani na kusindikizwa eapoti
Pale alikuwa bado hajawa Commamder in Chief ! Alienda kumuona TL kwa kuguswa kama mwanadamu mwenzake aliyeumizwa. May be alikuwa by then tofauti na wa sasa.
 
“Siku kadha zilizopita Ndugu zangu Nchi yetu imepata msiba wa kuuawa kwa mmoja wa Kiongozi wa CHADEMA, kifo kilichosisimua miili na akili za Watanzania na kuibua hisia kali hasa kwa Wafuasi wa Chama hicho, katika hali ya kushangaza kifo hicho kimeleta hisia kali pia kwa Wawakilishi wa baadhi ya Mataifa ya Nje wanaowakilisha Nchi zao hapa kwetu, nataka niungane nao na niseme kwamba kwasababu yoyote ile mauaji haya hayakubaliki na ndio maana Serikali tuliyalaani na kutaka uchunguzi wa haraka ufanyikke na ndivyo inavyofanyika Duniani kote”

“Nadhani nyie ni Mashahidi kule kwa wenzetu kulikoendelea kuna Mwanasiasa amekoswa kuuawa mara mbili (Trump) lakini tulichokisikia ni Serikali kutaka uchunguzi ufanyike kwahiyo si ajabu na kwetu baada ya tukio kutaka uchunguzi ufanyike na kazi nimeambiwa inaendelea vizuri”

“Baada ya tukio la Mzee Kibao nimekuwa nikiangalia maoni ya Viongozi mbalimbali wa kisiasa, Viongozi wa Dini baadhi yao wakiniomba nikemee mambo hayo, maoni ya Wazee mashuhuri nimemsikia Mzee wetu Butiku nae kasema, Wawakilishi wa Mataifa ya Nje hapa Nchini nao wametoa tamko, Jumuiya za Kiraia na Wananchi kwa ujumla na wenyewe wamesema waliyosema “

“Hisia za makundi yote niliyotaja zikiibuliwa na kifo kimoja tu cha Ndugu yetu Kibao lakini kuna vifo vinasemwa muda baada ya muda, Watoto Albino wanauliwa, Watoto wadogo wanauliwa, sijui Mzee kahisiwa uchawi kauliwa mpaka leo Watoto watatu wamekutwa wameuliwa huko Dodoma”

“Inashangaza kifo cha Ndugu yetu kibao kimeibua wimbi kubwa, kulaani, kusikitika, kulaumu kuita Serikali ya wauaji, kufanyaje, hii sio sawa, kifo ni kifo, tunachotakiwa kufanya Watanzania wote tukemeeane, tusimame imara kukemea mambo haya, damu ya Mtanzania ituume tusiwe tunamwaga damu bila sababu” —— Rais wa Tanzania, Dkt. Samia kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro leo September 17,2024

My Take
Mautekaji ni kama yamechochewa tu, kutoka "drama"" mpaka "mtu mmoja tu"
PIA SOMA
- TANZIA - Dar: Ali Mohamed Kibao, kiongozi wa CHADEMA auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana
Huyu mwanamke aambiwe kila kitu kina mwanzo wake! Wananchi wamefikia ukomo wa uvumilivu!
Naona kama amevuka mstari mwekundu kwa kauli yake hii.

Ajifunze kupitia historia waliyopitia wenzake wengine waliomtangulia kwenye cheo Kama hiki cha kwake. Rais Dikteta Samuel Doe alikuwa na kiburi kama hiki hiki alichonacho yeye, lakini alijitokeza mbabe mmoja Bw. Prince Johnson alimnyoosha Samuel Doe hadi dunia yote ilitikisika kwa kishindo cha kunyooshwa kwake.
 
Hivi familia ya Ali Kibao inayachukulia namna gani maneno kama haya? Baba ambaye ndio bread-winner, anauawa kikatili namna hiyo halafu mtu anasema kifo ni kifo tu! Kijeli za aina hii ziliwahi kuangusha falme: Aulize historia ya Ufaransa: Marie Antoinette aliangusha ufalme wake kwa kijeli akisababisha mapinduzi ya Ufaransa.
 
Back
Top Bottom