Rais Samia: Jengo la Kariakoo kulikuwa na mchanga mwingi kuliko nondo na saruji

Rais Samia: Jengo la Kariakoo kulikuwa na mchanga mwingi kuliko nondo na saruji

Viongozi wetu wanaongea kama wanaota. Sasa soko na janga vinahusiana vipi?
Bila kujifagilia bibi yenu hajisikii raha. Kesho utasikia atasema anaagiza ndege mbili kuubwa za kozoa taka Tanzania nzima na kuzipeleka china wakahangaike nazo.
Halafu, Soko unajenga jangwani ili mafuriko yakija yasaidie kuwasafirisha wamachinga hadi mtwara bila serikali kuwalipia nauli?
 
Tuwe serious watanzania.
Wakati wanajenga hapakuwa na serikali?.
Kuna mahali huko kusini nilikuwa najenga petrol station,pamoja na kuwa na vibali vyote na kufuata taratibu zote, Afisa Mtendaji Kata wa eneo hilo alikuja na kuomba kuthibitisha kama nyaraka zote kweli ninazo na akawapigia simu mshauri mwelekezi pamoja na mkandarasi (hawa namba zao zipo kwenye bango la ujenzi) na kuthibitisha kuwa kweli nimekamilisha taratibu zote.

Nilimpongeza sana na kujiuliza, inakuwaje sehemu ambapo uongozi wa serikali upo lakini uholela unaendelea!!??

Ni nini maana ya kuwa na huu msururu wa maviongozi ambao hawajui kipi kinaendelea hata mtaani pake!!???
 
KASSIM MAJALIWA - WAZIRI MKUU WA TANZANIA

"Mheshimiwa Rais ulinielekeza kuunda kamati maalum ya kufanya uchunguzi wa kuporomoka kwa jengo na kufanya ukaguzi wa kina wa majengo mengine yalioko kwenye eneo la Kariakoo

"Napenda kukufahamisha kuwa kamati hiyo, wajumbe wake wote wako hapa ndani na imehitimisha kazi yake na kwa sasa nakamilisha taratibu za kuiwasilisha kwako nikiwa pamoja na timu nyingine iliyoundwa kwa kadri itakavyokupendeza siku yoyote na wakati wowote tunaomba utupangie muda pamoja na kamati kwa ajili ya kufanya mawasilisho mbele yako
Hiyo kauli ya KM mbona kama ina ukakasi?
 
Back
Top Bottom