Rais Samia: Jeshi la Polisi msitumie Sheria kama 'Kitega Uchumi'

Rais Samia: Jeshi la Polisi msitumie Sheria kama 'Kitega Uchumi'

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
RAIS AWATAKA POLISI WASITUMIE MAKOSA KAMA KITEGA UCHUMI

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewataka Polisi wasitumie makosa kama kitega uchumi kwa kutoza faini mbalimbali badala yake wajikite kwenye kudhibiti makosa

Ameyasema hayo alipokuwa katika Ziara ya Kuzindua Kiwanda cha Ushonaji cha Jeshi la Polisi, Bohari Kuu Kurasini ambapo Polisi waliliripoti kupungua kwa mapato kutokana na kupungua kwa makosa

Rais Samia amewataka wajikite zaidi kwenye kuelimisha Umma ili kupunguza makosa na sio wao kutegemea kukusanya fedha kutoka kwenye makosa mbalimbali.

jordansmoke.png
Asante Mama ilikuwa tunapigwa Faini za Ajabu Ajabu
 
Rais Samia amelitaka Jeshi la polisi kutumia sheria kwa ajili ya kudhibiti na siyo kama kama kitega uchumi cha kujiingizia mapato mfano utozaji wa faini za makosa ya barabarani

Source: TBC
Mwambie mama asahau kabisa hio haipo
 
Leta leseni kimashine kinachomolewa unanipa ten au nikuchoree. Askari barabarani kwa rushwa nimewavulia kofia.
 
Rais Samia amelitaka Jeshi la polisi kutumia sheria kwa ajili ya kudhibiti na siyo kama kama kitega uchumi cha kujiingizia mapato mfano utozaji wa faini za makosa ya barabarani

Source: TBC
Tuna sheria za kipumbavu sn za barabarani, faini ya pikipiki inalingana na V8 zote elfu 30 kweli?
 
Rais Samia amelitaka Jeshi la polisi kutumia sheria kwa ajili ya kudhibiti na siyo kama kama kitega uchumi cha kujiingizia mapato mfano utozaji wa faini za makosa ya barabarani

Source: TBC
RPC arusha, fuatilia kituo cha polisi Usa River . Traffic pale ni changamoto na watu wananunua utrafic na kununua kituo ili apangwe Usa River.
 
Huku Kigamboni - Kimbiji traffic wanajificha na kuchomoza ghafla wanakubambikia overspending
 
Jiwe (r.i.h) alikuwa anafurahi sana anaposikia mapato yameongezeka bila kujali pesa ni ya dhuluma au ya heri.
 
Rais Samia amelitaka Jeshi la polisi kutumia sheria kwa ajili ya kudhibiti na siyo kama kama kitega uchumi cha kujiingizia mapato mfano utozaji wa faini za makosa ya barabarani

Source: TBC
Dah polisi wakifuata hili kwa 50% tutashuka kiuchumi maana moja ya chanzo kikubwa cha mapato cha mwendazake ilikua ni fine za Barabarani
 
Back
Top Bottom