Ninakushukuru Mhe. Rais kuhusu ushauri ulioutoa kuhusu vitendo vya Maaskari traffic pindi wanapotekeleza majukumu yao. Kazi yao kubwa iwe ni elimu na siyo kukimbilia kuongeza mapato. This is big NO. Mimi ni muhanga wa Maaskari wanaofanya shughuli zao barabarani. Tarehe 11.5.2021 nilisafiri kwenda Tarime na nilipofika Kiabakari nikapigwa mkono. Kwa utaratibu nikasimama na ukaguzi ukaanza.
Kwanza wakaanza na bima ikawa hakuna kasoro, Pili wakamuuliza dereva wangu leseni yake ikawa hakuna kasoro, tatu wakakagua matairi ya gari ikawa hakuna kasoro, nne wakakagua taratibu zote kuanzia breki, indicator kama taa zinaonyesha ikawa hakuna kasoro. Mwisho wakamuomba dereva reflector na akawapa.
Yule mkaguzi akamuuliza dereva mbona reflector yako inaonekana ni ya kizamani lakini dereva akamwambia lakini si inafanya kazi?. Yule askari akang'ang'ana kuwa reflector ni ya kizamani ili tuandikiwe faini hapo ndo nikaja juu na mabishano haya yalikuja kusuluhishwa na askari mwenzake kwa kumwambia kuwa kwa kosa hilo basi anatuonea. Baada ya mabishano ya muda mrefu ndo tukafikia muafaka na sikuandikiwa faini.
Nilichotaka kueleza hapa ni kuwa Maaskari barabarani kazi yao kubwa iwe ni ushauri, maelekezo na tozo ya faini kiwe ni kitu cha mwisho. Nimewahi kuelezwa sijui kama ni kweli kuwa kila siku askari anayesimama barabarani hupewa lengo la makusanyo ya kuwasilisha baada ya kazi. Maaskari wa barabarani msikimbilie kwenye tozo, toeni elimu na ushauri katika kutekeleza majukumu yenu.