Bulelaa
JF-Expert Member
- Jun 28, 2024
- 1,342
- 3,247
Miongoni mwa waliohudhuria kwenye mikutano ya Rais Samia huko Katavi na mimi nilikuwepo
Kwenda kwangu kwenye mikutano hiyo, siyo kwamba ndio namkubali Rais katika utendaji wake, hapana
Nimepatwa na shida sana kichwani kuamini kwamba, huyo ndiye aliyezunguka na JPM kuomba kura huku wakituahidi maisha chipa pindi mitambo ya umeme ya JKHNP itakapokamilika na kuanza kutumika
Cha kushangaza ni kwamba, baada tu ya kukamilika na kuanza kutumika tukaanza kushuhudia Luku inawekewa tozo za ajabu ajabu zisizoeleweka,
Mbali na hilo, kipindi cha nyuma, Aliyekuwa aliyekuwa waziri wa Nishati bwana Januar Makamba, alitoa tamko mapema kuhabarisha kwamba, umeme hautashuka bei kama ilivyowahi kusikika kipindi cha viongozi hao wawili walipokuwa wakieleza manufaa ya kuwa na mradi wa JKNHP, hii ni kwa sababu walizozijuwa wao kina Makamba
Kwa maana hiyo, yawezekana kabisa kwamba, wapo na wananchi maelfu kwa maelfu waliohudhuria mikutano hiyo kwenda kumshangaa Rais huku wakiwa na maswali kama niliyonayo mimi,
Maana inakuwa ngumu sana kuamini, mtu aliyezunguka nchi nzima kutueleza umeme utashuka bei mara tu baada ya kuanza uzalishaji wa umeme kwenye mradi wa JKNHP kule rufiji leo amegeuka hivihivi yaani, uungwana ni tabu sana
Leo kageukaje? Licha ya hivyo, bado ameruhusu Luku iwe inatozwa fedha kibao mwisho wa mwezi wakati huo huo akijua walipaji wakuu wa tozo hiyo ni walala hoi waliopangishwa najumba na kundi la wenye kipato cha juu?
Siku mlala hoi atakapohitaji kuondokana na ulala hoi, shariti ajikatae, aseme yeye si yeye, bila shaka ndipo ataanza kuzisogelea ndoto zake
Mungu bariki nchi yangu Tanzania, Utupatie na viongozi makomando huwenda tutapa ahuweni!
Ameen
Pia soma: Magufuli aliondoa 'Service Charge' Tanesco ya 7,000 lakini Serikali ya sasa inazirudisha tozo kidogokidogo kupitia mfumo wa Luku