Lord OSAGYEFO
JF-Expert Member
- Feb 19, 2021
- 3,085
- 4,890
Rais Samia Suluhu Hassan kwanza nakupongeza sana kwa hatua mbalimbali unazochukua baada ya kuondokewa na Magufuli Mhe. Rais kama lilivyo jina lako wewe ndio Suluhu ya suala la Katiba mpya.
Haya yote unayohangaika nayo kuyaweka sawa ni kutokana na Mwendazake kuona mapungufu yaliyopo kwenye katiba iliyopo ndio ikawa rahisi kwake kuyafanya aliyoyafanya. Nadhani hata wewe utakumbuka hayati Baba wa Taifa aliwahi kusema Katiba hii ilimpata rais dikteta atawaonea wananchi na hilo limetimia kwa Mwendazake.
Rais samia "legacy" yako pekee sio kujenga zahanati au kupandisha mishahara bali ni kuwapatia wananchi katiba mpya nakuhakikishia rais samia utakumbukwa kwa miaka hata 50 ijayo rais mstaafu Jakaya Kikwete pamoja na kuwa hakufanikiwa kutupatia katiba mpya lakini vizazi vinamkumbuka kwa uthubutu wake wa kuanzisha mchakato kwani alisema katiba iliyopo ina miaka 50 na mambo mengi yamebadilika.
Mungu ambariki sana.